Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 30 July 2012

GERRY TEGETE, NGASA WASHEREHEKEA UBINGWA PAMOJA NDANI YA WHITE HOUSE KIMARA KOROGWE.!!!!!!


Mwanamuziki nguli wa Bendi ya Mashujaa Musica Chaz Baba akiimba kwa furaha kubwa ndani ya Ukumbi wa White House Kimara Korogwe usiku wa kuamkia leo.

Kutoka kulia Chaz Baba, Mrisho Ngasa Mchezaji wa Azam na Gerry Tegete Mchezaji wa Yanga wakiwa ndani ya viunga vya White House Kimara Korogwe jana baada ya kutoka kwenye Mechi kali baina ya timu zao, ya kombe la Kagame ambayo Yanga waliibuka mabingwa kwa mabao 2 kwa bila.

Kulia Gerry Tegete akishoo luv na Mchezaji mwenzake Mrisho Ngassa anayechezea club ya Azam.

Rapa maarufu wa Bendi ya Mashujaa Fagasoni akiimba ndani ya ukumbi wa White house Kimara Korogwe.


Mpiga tumba namba moja Afrika mashariki MCD akiwakimbiza washabiki wao ndani ya White house Kimara.

Mrisho Ngassa na Chaz Baba wakifurahia kwa pamoja Ushindi waYanga, Mrisho ngassa ni Mshambuliaji mahiri wa Club ya Azam.

Tegete, Henry na kulia Mrisho Ngassa ndani ya White House Kimara.

 kulikulikuwa na mechi ya fainali ya kombe la Kagame kati ya Yanga afrikani na Azam FC ndani ya uwanja wa Taifa ambapo Yanga waliibuka mabingwa

Ngassa na Tegete kwa kuonyesha mpira sio ugomvi walisherehekea pamoja ushindi wa Yanga baada ya mechi katika viwanja vya White House Kimara korogwe wakati bendi ya Mashujaa ilipokuwa inatumbuiza

Sunday, 29 July 2012

Nawatakieni J'Pili Njema;Burudani- Kwaya kutoka Mbeya na Iringa!!!!!!!!!

Nawatakia J'Pili yenye Baraka, Amani,Fadhili na Shukrani.
 Mungu na Atufadhili na kutubariki,Na kutuangazia Uso wake.
Njia yake ijulike Duniani,Wokovu wake katikati ya Mataifa Yote.

Neno la Leo;Zaburi:67:1-7...

Saturday, 28 July 2012

Chaguo la Mswahili Leo; Kagera Mpoo? NgojaTatuNane Wawasaidie!!!!!

Waungwana "CHAGU LA MSWAHILI LEO" ngoja niwapeleke Kagera,
 wanakwambia Mapenzi Kizunguzungu...Nshomileeeeee........

Sina Mengi leo Uwanja wako.
 Unalolote kuhusu Burudani ya Leo?
 Jimwage sasa.

mimi siimbi Natifuka tuu Twende Sote sasa............."Swahili NA Waswahili"!!!!!!! Pamoja Daima.



Tuesday, 24 July 2012

Kundi la watu wanaodhaniwa majambazi wamevamia baa ya Chonya...

Kundi la watu wanaodhaniwa majambazi wamevamia baa ya Chonya eneo la River Side jijini DSM, leo asubuhi na kupora fedha..




Wakazi wa Ilala Sharifu Shamba Wamebaki wana shangaa na Kuogopa, Baada ya kusikia milio ya risasi!!!


 Poleni sana.




Shukrani; ITV.

ENGINEER WA VODACOM JOSEPH MWAPINGA APATA PIGO: AFIWA NA MKEWE.




Marehemu Belinda J. Mwapinga enzi za uhai wake.

Mwili wa Belinda ukiwa katika kanisa la roman katoliki extenal.

Baba Padre akitoa heshima yake ya mwisho kwa mwili wa Belinda. J. Mwapinga jana katika Kanisa la Katoliki Extenal Dar es salaam

Joseph Mwapinga mwenye suti nyeusi akiwa na watoto wake alio achiwa na mke wake kipenzi Belinda.


Wafanyakazi wa VODACOM Tanzania wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Belinda wakiufikisha katika makaburi ya Kinondoni.

Hawa ni baadhi ya waombolezaji waliohudhuria kwenye safari ya mwisho ya Belinda.


Mwili wa Marehemu Belinda ukiwa umewekwa juu ya nyumba yake ya milele katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.

Mhandisi Joseph Mwapinga akiweka shada la mauwa kwenye kaburi la Mke wake.



Baba Padre akisali sala ya mwisho kwa ajili ya kumuombea Marehemu Belinda J. Mwapinga katika makaburi ya Kinondoni.
kulia kwa Padre ni Joseph Mwapinga na mwenye Tshirt nyekundu ni rafiki wa karibu wa familia, Ndugu Stephen Mapunda.

Marehemu Belinda J. Mwapinga alifariki tarehe 20/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili na mazishi yake kufanyika tarehe 23/07/2012 katika makaburi ya Kinondoni.

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIBARIKIWE.


"Swahili NA Waswahili" Tunawapa pole wafiwa. 

Monday, 23 July 2012

Jikoni Leo;Maidana-na JIKO LANGU,Mapishi-Maandazi ya Yogurt!!!!!!!!!

MAHITAJI
yogurt vijiko 2vya chakula
sukari 1/4 mug
hamira kijiko kimoja cha chai
iliki kijiko kimoja cha chai
samli kijiko kimoja cha chakula
unaweza tumia,maji/maziwa/nazi yapime katika mug uliyopimia sukari
ponda hadi unga wako uwe mlaini kiasi,katakata matonge,sukuma kata maandazi yako
yaache yaumuke yachome.
unaweza kutumia maharage,mchuzi wa nyama,maini,samaki kama kitoeo.





Waungwana Mapishi yapo Mengi haya "JIKONI LEO" ni Maandazi ya Yogurt ,Siyo Nazi kaazi kwako kama wewe Mpishi au Muonjaji!!!!


 Mpishi si Mwingine ni da'MAIDANA na "JIKO LANGU"  [LAKE].
kwa Maelezo Zaidi ingiahttp://jiko-langu.blogspot.co.uk/




"Swahili NA Waswahili" inawatakia Ramadhani Njema Waislam woote Dunia.

Sunday, 22 July 2012

J'Pili ya Leo Tumsikilize;Masanja Mkandamizaji - Albam Hakuna Jipya, Zaburi ya Wani Fifte!!!!!

Masanja ndiye anayetupa Neno na Burudani J'pili ya leo.
Neno la Leo zaburi :150;1-6;Haleluya.Msifuni MUNGU katika Patakatifu pake;Msifuni katika anga la uweza wake,Endelea...

Nawatakia J'Pili yenye Baraka,Amani,Furaha,Upendo,Unyenyekevu na Fadhili!!
Na kila Mwenye pumzi na  amsifu BWANA.
HALELUYA!!!!!!!