Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 5 August 2012

Nawatakia J'Pili yenye Furaha;Burudani- PARAPANDA VOICE CHOIR!!!!!!!

Taa ya Mwili ni Jicho;basi jicho lako likiwa safi,Mwili wako wote utakuwa na Nuru.
Lakini jicho lako likiwa bovu,Mwili wako wote utakuwa na giza.Basi ile Nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza;Si giza hilo!!!!!


Neno la Leo;Mathayo Mtakatifu:6:22-23.
MUNGU NA AZIDI  KUTUBARI SOOOTE!!!

Saturday, 4 August 2012

Chaguo la Mswahili Leo;Extra musica,Bisso Na Bisoo,Loi na Koffi,Gaou!!!!!!

Waungwana "Chaguo la Mswahili Leo" Twende sote sasa Bisso Na Bisso,Gaou na nyingine....
.
Kunakitu unakumbuka? Pamoja sana....

 Tiririririii Extra Musicaaaa, hyeeeeeeee!!!
Shamukwale  yako pesa mbongooooo.....Chivunduuuu!!!hahahaha
"Swahili NA Waswahili" Ah ah ah ah ah ah ahhhhhh  eeeeeeeeeeh!!


Thursday, 2 August 2012

OFFICIAL VIDEO-LEKA DUTIGITE VIDEO-KIGOMA ALL STARS!!!!!!

Kigomaaa Leka Dutigiteee!!!


Haya Waungwana mambo ya Kigoma hayo.Jee nawengine mnakuja kama hivyo?
Dar,Iringa,Tanga,Mwanza,Mbeya na.....................


Waungwana mna  Maoni,Ushauri,Mawazo Gani katika hili?


 LEKA DUTIGITEEE!!!!!!


"SWAHILI na WASWAHILI" Pamoja Daima.


Ngoma Africa Band to perform at International African Festival,Tubingen,Germany!!!!!!!!

Ngoma Africa Band to perform at International African Festival,Tubingen
Ngoma Africa Band, a German based Tanzanian band will headline the International African Festival Tubingen 2012, Germany, on 12th August 2012.

The band leader, Ebrahim  Makunja aka Ras Makunja will receive the International Diaspora Award (IDA) on behalf of the band for their commitment to promote East African music throughout Europe.

Ebrahim Makunja aka Ras Makunja, leader of Ngoma Africa Band
Ms. Susan Muyang Tatah, CEO of the International African Festival Tubingen 2012 said Ngoma Africa Band was chosen for the award because of their creative performance on stage. It's difficult to resist dancing at their concerts, she said.

Ngoma Africa Band will also perform on 26th August 2012 at the Alafia Festival Hamburg; on 12th September 2012 at Bremahaven City; and on 15th September 2012 at Africa Trade Fair Expo (Afrika-Messe), Bremen City.

The band has just released a new CD titled "Bongo Tambarare" featuring hits including "Supu ya Mawe" and "Uhuru wa Habari". The new release is already dominating air waves in Tanzania.


For further information about Ngoma Africa Band and to listen to their music, please visitwww.ngoma-africa.com.

Sorce:Africa News EU
http://theafricanews.com/entertainment/44-entertainment/4427-ngoma-africa-band-to-perform-at-international-african-festival-tubingen.html 

Wednesday, 1 August 2012

Siku Kama ya Leo da'Rachel-siwa Alizaliwa!!!!!MUNGU yu Mwema Kwanguuuuuuu

Siku kama ya Leo Familia ya M.S.Kiwinga walipata Mtoto wa kike!!!!
Mimi Rachel-siwa NaMshuru sana Mungu kwa Mema Yooote Maishani Mwangu.
Kwangu hakuna baya na nilipo hisi baya Nafuta na Kusema ni MAPITO[MITIHANI]TUU.WEWE UNATOSHA BABA!!!.

 Mtoto  kwa Wazazi atabaki kuwa mtoto hata kama ana Watoto.
Ninawashukuru sana Wazazi wangu kwa yooote mliyojaaliwa kunipatia kulingana na Uwezo wenu,
Nawapenda,Nitaendelea Kuwapenda mpaka mwisho wa Maisha Yangu.
BABA najua hayupo nami kimwili lakini Kiroho nipo nawe na nitaendelea kukumbuka Daima.

Nikushukuru UBAVU wangu ISAAC,Asante sana kwa yooote,MUNGU Azidi kutusimamia katika Maisha yetu.Mimi Penda sana wewe Mubena yangu!!!!!

Niwashuru sana Kaka,Dada,Watoto  Zangu woote Nawapenda.

Pia Niwashukuru Ndugu,Jamaa,Marafiki,Majirani na Wooote wanaonifahamu kwa njia moja au nyingine.

Kamwe Sijutii kufahamiana nanyi, Basi Nirudishe Shukrani kwa MUNGU najua ni mpango wake kuniunganisha nawe.

Nanilipo kosea/kukukosea Naomba Nisamehe,Kwani Nami ni Bin'Adam Sijakamilika.

Nawapenda woote wakubwa kwa watoto,Wake kwa Waume.

MUNGU TUBARIKI SOOOOTE.
AMEEN.

Tuesday, 31 July 2012

Wanawake na Mitindo;Leo Mashungi/Kujitanda!!!!!!


Waungwana Leo Tuangalie Uvaaji huu Sijui kama ni Mwezi huu wa Ramadhani au Msibani/Hitimani au.....


Ukienda Rumi Fanya kama Wafanyavyo Warumi, Ukikuta Wenyeji Wanakunja Miguu nawe Kunja yako!!!!!


Kwenye Picha hizi si Woote waavaaji hivyo kila siku Waliheshimu Sehemu Husika.


Wewe unamawazo,Maoni,Ushauri Gani katika hili?


Jee nawe unapicha yako Umevaa hivi?Ruksa kushiriki Nasi, Unaweza kututumia rasca@hotmail.co.uk


Jimwage mwanakwetu!!!!" "
RAMADHANI NJEMA KWA WOOOTE"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Monday, 30 July 2012

GERRY TEGETE, NGASA WASHEREHEKEA UBINGWA PAMOJA NDANI YA WHITE HOUSE KIMARA KOROGWE.!!!!!!


Mwanamuziki nguli wa Bendi ya Mashujaa Musica Chaz Baba akiimba kwa furaha kubwa ndani ya Ukumbi wa White House Kimara Korogwe usiku wa kuamkia leo.

Kutoka kulia Chaz Baba, Mrisho Ngasa Mchezaji wa Azam na Gerry Tegete Mchezaji wa Yanga wakiwa ndani ya viunga vya White House Kimara Korogwe jana baada ya kutoka kwenye Mechi kali baina ya timu zao, ya kombe la Kagame ambayo Yanga waliibuka mabingwa kwa mabao 2 kwa bila.

Kulia Gerry Tegete akishoo luv na Mchezaji mwenzake Mrisho Ngassa anayechezea club ya Azam.

Rapa maarufu wa Bendi ya Mashujaa Fagasoni akiimba ndani ya ukumbi wa White house Kimara Korogwe.


Mpiga tumba namba moja Afrika mashariki MCD akiwakimbiza washabiki wao ndani ya White house Kimara.

Mrisho Ngassa na Chaz Baba wakifurahia kwa pamoja Ushindi waYanga, Mrisho ngassa ni Mshambuliaji mahiri wa Club ya Azam.

Tegete, Henry na kulia Mrisho Ngassa ndani ya White House Kimara.

 kulikulikuwa na mechi ya fainali ya kombe la Kagame kati ya Yanga afrikani na Azam FC ndani ya uwanja wa Taifa ambapo Yanga waliibuka mabingwa

Ngassa na Tegete kwa kuonyesha mpira sio ugomvi walisherehekea pamoja ushindi wa Yanga baada ya mechi katika viwanja vya White House Kimara korogwe wakati bendi ya Mashujaa ilipokuwa inatumbuiza