Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 22 August 2012

Miss East Africa Belgium 2012Juliana Pierre!!!!!!!



Miss East Africa Belgium 2012
Mwakilishi wa Tanzania kwenye fainali Miss East Africa Belgium yatakayofanyika tarehe 1 September 2012, Miss Juliana Pierre

Muunge mkono mwakilishi wetu huyu kwenye Fainali husika kwa kuongeza  idadi ya kufahamika kwake.
Juliana anaomba uingie kwenye ukurasa wake wa (Face book) na kubonyeza kitufe cha “like” kwa anuani hii: https://www.facebook.com/JulianaPierreFinalisteMissEastAfricaBelgium2012

Sunday, 19 August 2012

Nawatakia Eid Mubarack na J'Pili Njema!!!!!!!


Waungwana nawatakia "EID MUBARACK" na J'Pili Njema!!Ndugu,Jamaa,Marafiki na Watu Woote.MUNGU awalinde katika Siku hii na Siku zote.
Iwe siku ya Upendo,Amani,Fadhili,Kusaidia Yatima,Wajane,Wagonjwa ,Wenye Shida na Tabu.Ili nao wapate Faraja na kujiona wapo na watu wanaowajali.

Nami Mwezi  wa Ramadhani haukupita hivi hivi niliungana na Familia  ya  Mkulu "Mama Miriam"   kwa FUTARI. Shukrani sana. 

MUNGU Atubariki Sooote!!!!

"JIKO LA MAMA MIRIII"






        Jee unapenda kutuambia EID Yako imekuwaje,kutuma ujumbe,salaam au picha? Usisite kututumia kupitia;rasca@hotmail.co.uk.Karibuni Wooote!!!!

 "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Saturday, 18 August 2012

Chaguo la Mswahili Leo; Q chief-Si Ulinikataa,Ninachokipata,Wiper,Namtafuta Kule alipoooo!!!!!

Waungwana "Chaguo LA Mswahili Leo"Leo ni Mswahili Q CHIEf.
Vipi Nyimbo zake zinakubamba/unazipenda?Jee kunakitu unakumbuka kupitia Nyimbo hizi?

Twende soote sasa..Kosa langu kosa langu ni lipi baba? ulinikana Tangu tumboni, Ulimkana mama yanguu...Si ulinizaa wewe Ukanikataa sasa iweje unaona mi Nafaaaaaaaa.... Endeleaa...

Jee vipi kama mtoto alikataliwa na BABA Yake ni Vyema nae MtotoKumtosa/kumkataa baba au...Jee Ingekuwa Wewe Ungefanyaje?.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

MASHUJAA MUSICA NA RATIBA YAO YA SIKUKUU YA IDD EL FITR!!!!!


Martin Sospeter Luhangisa, Meneja wa Mashujaa Bendi
BAADA ya kukamilisha ziara ya kutambulisha wanamuziki wake wapya wa Mashujaa Band, sasa ni zamu ya kuwapa burudani wapenzi wa bendi hiyo kwa siku ya Idd Mosi na Idd Pili.
Meneja wa Bendi hiyo Martin Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd mosi watakuwa Msasani kwenye ukumbi wa Emirates.
Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd pili watakuwa Mjini Mtwara katika ukumbi wa Makonde Beach ili kuwapa radha wakazi wa huko.
Bendi hiyo ambayo hivi sasa ipo hivi chini ya Rais wake Chalz Baba, itatoa burudani hiyo kwa ajili ya kutangaza kazi zao mpya kwa wapenzi wa nyimbo zao na Bendi yao kwa ujumla.
Alisema, pia kwa wale wanaoisikia Bendi ya Mashujaa kwenye vyombo vya Habari, sasa ndiyo wakati wao wa kuiona bendi hiyo laivu katika Sherehe za Eid El Fitri.
"Kama tulivyowapagawisha wakazi wa Songea na Mbeya wiki iliyopita, sasa ni zamu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Mtwara," alisema Sospeter.

Friday, 17 August 2012

SAUTI Ya ILALA na Mikakati Yake; Pata Video!!!!!



Waungwana ni "SAUTI YA ILALA"sina mengi ya Kuelezea Wenyewe wamemaliza yooote.Tunasubiri Utendaji Tuu.Kila la kheri Hon;Jerry Silaa na Kamati Yako.
Unalo la Kuongezea Muungwana? haya Tunasubiri Maoni/Ushauri.

kwa Mawasiliano Zaidi: DAVIS MWIJAGE
 PHONE: +255712847881
 EMAIL: davis@361tanzania.com
ILALA MUNICIPAL RE INAUGURATES “ SAUTI YA ILALA MAGAZINE” 
Shukrani;Mustafa Hassanali

Kisa cha Leo ni Emu-Three na Mbio za Sakafuni,Huishia Ukingoni!!!!


Mbio za sakafuni,huishia ukingoni 4

Waungwana leo nimewaletea Mswahili; Emu-Three na Diary Yangu[Yake]
ANASEMA;Hii ni blog maalum kwa kumbukumbu za maisha 
(diaries), 
visa na matukio na yale unayopenda kuchangia na wenzako (mijadala),
 maneno ya hekima,
 kusaidiana na pia kutoa dukuduku lako (kilio chako). 
Soma na uchangie chochote kwa 
kutoa maoni (comments) yako,
 au tutumie kisa chako, au lolote lenye mafunzo ili tuliweke hewani.

Tupitie Kisa hiki kidogo, hii ni Sehemu ya 4:Kila mfanyakazi tunayemchukua hakai hapa nyumbani, sasa nimechoka kabisa kutafuta mfanyakazi wa nyumbani, naona ni heri nijifanyie kazi zangu mwenyewe, kwanza nililelewa kama mfanyakzia wa nyumbani…’akasema mke wangu.

Kipindi hicho maisha yetu yapo juu, tuna kila kitu, …lakini maisha ya ndani yalikuwa na mitihani yake, na ilionyesha wazi kuwa tulihitaji msaidizi, ili na yeye apate muda wa kufuatilia miradi yetu.Niliinuakichwa na kumtizama kwa macho ya huruma,maanaalikuwa mtu wa pilikapilika, shughuli zandani, shughuli zamiradi, shughuli za kijamii, zote alikuwa akijitahidi kujumuika nazo.

Nilimwangalia na kutabasamu, na hapo nikakumbuka siku za nyuma, wakati akiwa binti, wakati nampigania kumpata, ilikuwa kama kampeni za siasa ambazo nilikuwa nikipambana nazo, na hata siku anaingia kwangu kama mke wangu sikuamini.
‘Unanikumbusha mbali sana mke wangu, sijui kama ningekukosa ingelikwuaje…’nikasema.Inaendelea;kuanzia Sehemu ya 1-hii ya 4 na Kuendelea na Kisa hiki ingia;http://miram3.blogspot.co.uk
Mpendwa Unalolote la kuongezea kwa mwandishi huyu?Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.Karibu sana.


Hongera sana Emu-Three kwa Kazi zako,Mungu Azidi kukubariki sana sana kwa Kazi za Mikono yako na kila lililo Jema.Tunakutakia Swaumu Njema!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Thursday, 16 August 2012

FFU wa Ngoma Africa band na Mashambulizi yao Tubingen,Ujerumani!!!!!













FFU wa Ngoma Africa band  imewasha moto,TUBINGEN
  
Wamechukua Tuzo ya "IDA-International Diaspora Award"

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya,Ngoma Africa Band
Siku ya Jumamosi 11.8 .2012 walishambuli jukwaa na la
International Africa Festival 2012,Tubingen,Ujerumani,
na kuhakikishia washabiki kuwa FFU ni tishio la kimataifa !
Kiongozi wa bendi Ras Makunja alikabidhiwa Tuzo ya kimataifa ya
"International Diaspora Award" kwa niaba ya bendi hiyo.

The Ngoma Africa Band