Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 26 August 2012

Mario Van Peebles Exclusive Interview - Tanzania Films Critics Associati...!!!!!!


Mario Van Peebles interview with Tanzania Films Critics Association (TFCA 


The link above is about 15 Question and Answer of video Insightful interview with Film maker/Director/Producer, Actor Mario Van Peebles and Michael Cohen, talk about their new Movie "We the Party" and general view of Tanzania Film Industry in including Copyright aspects in combating piracy problems and their view of films activities here in Tanzania.
Tanzania Films Critics Association (TFCA)
----------------------------------------------

Nawatakia J'Pili yenye baraka na Amani.Burudani- Mwamba Rock Choir!!!!


Wapendwa Nawatakia J'Pili yenye Baraka,Upendo,Umoja, Amani na Malezi mema.

Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse;Wanafunzi wake wakawakemea.Ila YESU alipoona alichukizwa sana,akawaambia,Waacheni Watoto wadogo waje kwangu,msiwazuie;Kwamaana Watoto kama hawa Ufalme wa MUNGU ni wao.

Neno La Leo:Marko Mtakatifu:10:13-16

"Swahili NA Waswahili" MUNGU ATUBARIKI SOTE.

Saturday, 25 August 2012

Chaguo La Mswahili Leo;Bob Rudala,Ali Kiba,,2berry,20 Percent!!!!!!!

Waungwana "Chaguo La Mswahili Leo" ni Kina Kaka hao wakilalamika juu ya Mapenzi.
Kwa Mtazamo wangu naona kama Tanzania[bongo]Nyimbo nyingi zinazungumzia Mapenzi.Jee ndizo Zinawapenzi wengi,Rahisi Kutunga na Kuimba,Au...?

Mpenzi mimi sina Mengi Zaidi ni kutoka kwako.
Karibuni sana Kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Friday, 24 August 2012

Waswahili na Maisha Yao-TX Seleleka in Mgama Tanzania 1981,Makassy CCM,Mwendo Mdundo-CHADEMA!!!!!

Waungwana sina la kusema nimekumbuka Nyimbo hizi  za Zamani za Chama Tawala na nikaona niweke na Nyimbo ya sasa ya CHADEMA. Nimeshindwa kupata ule chama chetu cha mapinduzi lakini utausikia kidooo hapo kwenye Video hiyo ya Mgama IRINGA.Hii nimeipata:http://watafiti.com.

Waswahili wakitimbwilika/kucheza, wengine huku wananyonyesha baasii ahhh.

Unalo la kuongezea hapo Muuungwa? Karibu sana kwa 
Upendo na Amani.

MUNGU IBARIKI TANZANIA. "Swahili NA Waswahili" 
Pamoja sana.

Thursday, 23 August 2012

DR JANETH MANDEPO AMEREMETA NDANI YA MWIKA HALL - SINZA USIKU WA JANA.!!!!!


Dr. Janeth Mandepo akiwa amesimama kwa furaha ndani ya Ukumbi wa mwika katika sherehe yake ya Sendoff usiku wa kuamkia leo.
Dr. Janeth (kulia) akiwa na mpambe wake
Baba na Mama Mandepo wakiwa na nyuso za furaha katika sherehe ya kumuaga binti yao Dr. Janeth iliyofanyika katika ukumbi wa Mwika - Sinza.
Wakwe watarajiwa wa Dr Janeth wakifuatilia kwa umakini sherehe ya kupongezwa kwa mkwe wao.

Dr. Janeth akipiga picha ya kumbukumbu na Madaktari na wafanyakazi wenzake kutoka Hospitali ya Mwananyamala.
Dr. Janeth akipiga picha ya kumbu kumbu na wanakamati waliomfanyia sherehe yake ya kumuaga (Sendoff) wakiongozwa na kaka yake Mh. Mtarajiwa George Mandepo wa pili kulia.
Makaka wa Dr Janeth wakiwa na nyuso za furaha huku wakiwa na Mzee Maarufu wa nyimbo za zamani aliyewahi kuibuliwa na channel ya ITV miaka kadhaa iliyopita katika kipindi cha HAWAVUMI LAKINI WAMO (Mzee Chengula) aliyevaa Suti ya Bluu na Kofia.


Dr Janeth akitoka ukumbini kwa furaha baada ya sherehe yake kuisha.

Dr. Janeth Mandepo aliagwa usiku wa jana wa tarehe 22/08/2012 katika Ukumbi wa Mwika Sinza.

Wednesday, 22 August 2012

Miss East Africa Belgium 2012Juliana Pierre!!!!!!!



Miss East Africa Belgium 2012
Mwakilishi wa Tanzania kwenye fainali Miss East Africa Belgium yatakayofanyika tarehe 1 September 2012, Miss Juliana Pierre

Muunge mkono mwakilishi wetu huyu kwenye Fainali husika kwa kuongeza  idadi ya kufahamika kwake.
Juliana anaomba uingie kwenye ukurasa wake wa (Face book) na kubonyeza kitufe cha “like” kwa anuani hii: https://www.facebook.com/JulianaPierreFinalisteMissEastAfricaBelgium2012

Sunday, 19 August 2012

Nawatakia Eid Mubarack na J'Pili Njema!!!!!!!


Waungwana nawatakia "EID MUBARACK" na J'Pili Njema!!Ndugu,Jamaa,Marafiki na Watu Woote.MUNGU awalinde katika Siku hii na Siku zote.
Iwe siku ya Upendo,Amani,Fadhili,Kusaidia Yatima,Wajane,Wagonjwa ,Wenye Shida na Tabu.Ili nao wapate Faraja na kujiona wapo na watu wanaowajali.

Nami Mwezi  wa Ramadhani haukupita hivi hivi niliungana na Familia  ya  Mkulu "Mama Miriam"   kwa FUTARI. Shukrani sana. 

MUNGU Atubariki Sooote!!!!

"JIKO LA MAMA MIRIII"






        Jee unapenda kutuambia EID Yako imekuwaje,kutuma ujumbe,salaam au picha? Usisite kututumia kupitia;rasca@hotmail.co.uk.Karibuni Wooote!!!!

 "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.