Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 25 August 2012

Chaguo La Mswahili Leo;Bob Rudala,Ali Kiba,,2berry,20 Percent!!!!!!!

Waungwana "Chaguo La Mswahili Leo" ni Kina Kaka hao wakilalamika juu ya Mapenzi.
Kwa Mtazamo wangu naona kama Tanzania[bongo]Nyimbo nyingi zinazungumzia Mapenzi.Jee ndizo Zinawapenzi wengi,Rahisi Kutunga na Kuimba,Au...?

Mpenzi mimi sina Mengi Zaidi ni kutoka kwako.
Karibuni sana Kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Friday, 24 August 2012

Waswahili na Maisha Yao-TX Seleleka in Mgama Tanzania 1981,Makassy CCM,Mwendo Mdundo-CHADEMA!!!!!

Waungwana sina la kusema nimekumbuka Nyimbo hizi  za Zamani za Chama Tawala na nikaona niweke na Nyimbo ya sasa ya CHADEMA. Nimeshindwa kupata ule chama chetu cha mapinduzi lakini utausikia kidooo hapo kwenye Video hiyo ya Mgama IRINGA.Hii nimeipata:http://watafiti.com.

Waswahili wakitimbwilika/kucheza, wengine huku wananyonyesha baasii ahhh.

Unalo la kuongezea hapo Muuungwa? Karibu sana kwa 
Upendo na Amani.

MUNGU IBARIKI TANZANIA. "Swahili NA Waswahili" 
Pamoja sana.

Thursday, 23 August 2012

DR JANETH MANDEPO AMEREMETA NDANI YA MWIKA HALL - SINZA USIKU WA JANA.!!!!!


Dr. Janeth Mandepo akiwa amesimama kwa furaha ndani ya Ukumbi wa mwika katika sherehe yake ya Sendoff usiku wa kuamkia leo.
Dr. Janeth (kulia) akiwa na mpambe wake
Baba na Mama Mandepo wakiwa na nyuso za furaha katika sherehe ya kumuaga binti yao Dr. Janeth iliyofanyika katika ukumbi wa Mwika - Sinza.
Wakwe watarajiwa wa Dr Janeth wakifuatilia kwa umakini sherehe ya kupongezwa kwa mkwe wao.

Dr. Janeth akipiga picha ya kumbukumbu na Madaktari na wafanyakazi wenzake kutoka Hospitali ya Mwananyamala.
Dr. Janeth akipiga picha ya kumbu kumbu na wanakamati waliomfanyia sherehe yake ya kumuaga (Sendoff) wakiongozwa na kaka yake Mh. Mtarajiwa George Mandepo wa pili kulia.
Makaka wa Dr Janeth wakiwa na nyuso za furaha huku wakiwa na Mzee Maarufu wa nyimbo za zamani aliyewahi kuibuliwa na channel ya ITV miaka kadhaa iliyopita katika kipindi cha HAWAVUMI LAKINI WAMO (Mzee Chengula) aliyevaa Suti ya Bluu na Kofia.


Dr Janeth akitoka ukumbini kwa furaha baada ya sherehe yake kuisha.

Dr. Janeth Mandepo aliagwa usiku wa jana wa tarehe 22/08/2012 katika Ukumbi wa Mwika Sinza.

Wednesday, 22 August 2012

Miss East Africa Belgium 2012Juliana Pierre!!!!!!!



Miss East Africa Belgium 2012
Mwakilishi wa Tanzania kwenye fainali Miss East Africa Belgium yatakayofanyika tarehe 1 September 2012, Miss Juliana Pierre

Muunge mkono mwakilishi wetu huyu kwenye Fainali husika kwa kuongeza  idadi ya kufahamika kwake.
Juliana anaomba uingie kwenye ukurasa wake wa (Face book) na kubonyeza kitufe cha “like” kwa anuani hii: https://www.facebook.com/JulianaPierreFinalisteMissEastAfricaBelgium2012

Sunday, 19 August 2012

Nawatakia Eid Mubarack na J'Pili Njema!!!!!!!


Waungwana nawatakia "EID MUBARACK" na J'Pili Njema!!Ndugu,Jamaa,Marafiki na Watu Woote.MUNGU awalinde katika Siku hii na Siku zote.
Iwe siku ya Upendo,Amani,Fadhili,Kusaidia Yatima,Wajane,Wagonjwa ,Wenye Shida na Tabu.Ili nao wapate Faraja na kujiona wapo na watu wanaowajali.

Nami Mwezi  wa Ramadhani haukupita hivi hivi niliungana na Familia  ya  Mkulu "Mama Miriam"   kwa FUTARI. Shukrani sana. 

MUNGU Atubariki Sooote!!!!

"JIKO LA MAMA MIRIII"






        Jee unapenda kutuambia EID Yako imekuwaje,kutuma ujumbe,salaam au picha? Usisite kututumia kupitia;rasca@hotmail.co.uk.Karibuni Wooote!!!!

 "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Saturday, 18 August 2012

Chaguo la Mswahili Leo; Q chief-Si Ulinikataa,Ninachokipata,Wiper,Namtafuta Kule alipoooo!!!!!

Waungwana "Chaguo LA Mswahili Leo"Leo ni Mswahili Q CHIEf.
Vipi Nyimbo zake zinakubamba/unazipenda?Jee kunakitu unakumbuka kupitia Nyimbo hizi?

Twende soote sasa..Kosa langu kosa langu ni lipi baba? ulinikana Tangu tumboni, Ulimkana mama yanguu...Si ulinizaa wewe Ukanikataa sasa iweje unaona mi Nafaaaaaaaa.... Endeleaa...

Jee vipi kama mtoto alikataliwa na BABA Yake ni Vyema nae MtotoKumtosa/kumkataa baba au...Jee Ingekuwa Wewe Ungefanyaje?.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

MASHUJAA MUSICA NA RATIBA YAO YA SIKUKUU YA IDD EL FITR!!!!!


Martin Sospeter Luhangisa, Meneja wa Mashujaa Bendi
BAADA ya kukamilisha ziara ya kutambulisha wanamuziki wake wapya wa Mashujaa Band, sasa ni zamu ya kuwapa burudani wapenzi wa bendi hiyo kwa siku ya Idd Mosi na Idd Pili.
Meneja wa Bendi hiyo Martin Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd mosi watakuwa Msasani kwenye ukumbi wa Emirates.
Sospeter alisema kuwa, siku ya Idd pili watakuwa Mjini Mtwara katika ukumbi wa Makonde Beach ili kuwapa radha wakazi wa huko.
Bendi hiyo ambayo hivi sasa ipo hivi chini ya Rais wake Chalz Baba, itatoa burudani hiyo kwa ajili ya kutangaza kazi zao mpya kwa wapenzi wa nyimbo zao na Bendi yao kwa ujumla.
Alisema, pia kwa wale wanaoisikia Bendi ya Mashujaa kwenye vyombo vya Habari, sasa ndiyo wakati wao wa kuiona bendi hiyo laivu katika Sherehe za Eid El Fitri.
"Kama tulivyowapagawisha wakazi wa Songea na Mbeya wiki iliyopita, sasa ni zamu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na Mtwara," alisema Sospeter.