NYOTA TUMAINI LETU
Jina: AikaRose Mwasha
Jinsia:Kike
Miaka:12
Utaifa:TANZANIA
Mchezo: Taekwando
KILO: 28 kg- beginners FEMALE
Club: Nong Jang
MAKAZI: Leuven Belgium
MAFANIKIO: MEDALI YA FEDHA
& DHAHABU
Kijana wa kitanzania
mwenye ndoto ya kuwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa hapo usoni
kwa kupitia mchezo wa mbinu za kujihami wa TAEKWANDO ,anamapenzi makubwa na
mchezo huu aliouanza angali mdogo akiwa na umri wa miaka 9 ,ameshashiriki mashindano madogo
madogo nchini Belgium na kupata mafanikio makubwa kufikia medali ya fedha. Hivi
karibuni alifanikiwa kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olympic open
Brussels yaliyofanyika Rue Du Lombartzyde
Brussels Belgium
tarehe 27 May 2012.
Sasa hivi anajiandaa na
team yake kwenda Copenhagen
kwenye mashindano ya Wonderfull
Copenhagen yatakayofanyika mwezi ujao.
Wito wake hasa kwa vijana
wadogo akitilia mkazo jinsia ya kike ni kujifunza michezo mbalimbali na kuwa na
ndoto ya kuwa mabalozi kwa taifa lao la TANZANIA.
VIPAJI HUINUA TAIFA
"Swahili NA Waswahili" Tunakutakia kila la kheri.