Sunday, 2 September 2012
Friday, 31 August 2012
Watoto na Malezi;Mtoto na Commando na Mtoto na Wachezaji!!!
Waunngwana Wazazi/Walezi;"Watoto na Malezi" Huyu anacheza na wachezaji,huyu anatupatia Picha la Commando!!!.
Duhh Huyu wa Commando kiboko...........Wewe unasemaje kuhusu mtoto mdogo na Wachezaji? na wa Commando jee? Kipaji,Ufuatiliaji mzuri au..
Vipi wewe ulikuwa wapenda nini Utotoni?
Tunasubiri Mtazamo wako.Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
Thursday, 30 August 2012
Jikoni Leo ni Tupike Pamoja-Mapishi ya Creme Caramel - Recipe of (Swahili)!!!!
Waungwana ni "Jikoni Leo" na da'Sophi wa "Tupike Pamoja" Mapishi ya Leo ni Creme Caramel. Maneno yasiwe meengi, angalia hiyo Video.
kama unaswali au Ushauri unakaribishwa.
pia ukitaka kujua Zaidi ungana naye kupitia;www.tupikepamoja.com au unaweza kuungana naye You TubeTupike Pamoja.
"Swahili NA Waswahili" Karibuni Wooote.
Tuesday, 28 August 2012
Pitapita ya Mswahili Mitaani-Coventry!!!!
Alikutana na Wapiga Ngoma
Ikapigwa na Akacheza
Banda la M'SENEGAL,Ameshona hizo Nguo na hivyo vidude wanatengeneza.
Waungwana ni "Pitapita ya Mswahili Mitaani" Ilikuwa Coventry. kulikuwa na Mabanda mbalimbali ya Bidhaa , Vyakula na Michezo.
Kwabahati mbaya WaTanzania hatukuwa na Banda.
Nimatumaini yangu siku/wakati mwingine tutakuwa na Banda hata la Mchezo wa Bao,Kijiwe cha Kahawa ile Chunguu yanywewa kwa Vikombe Vidoogo na Kashata.
Ndugu wa mimi/Blogger Mwenza EMU wa Three.Mmmhhh Ushauri wako Naufanyia Kazi.Hahahaha Eti Ndugu wa mimi ananishauri nijiunge na Michezo kama Miereka,Judo,Sarakasi ,Kuogelea na.........Uwiiii Kweli umenichoka, Sikuweza Mikundeni itakuwa Michorokoni? hhahaha na Uzee huu mwili umekomaaa.Hahah Usichekeshe walionuna.
Sina Meengi,Unalolote la kuongezea,Maoni,Ushauri?
Pamoja sana "Swahili NA Waswahili"
Ikapigwa na Akacheza
Mswahili mtoto akapiga ngoma nae |
Banda la Wazungu, wanauza vitu kutoka kwa Waswahili wa KENYA |
Banda la M'SENEGAL,Ameshona hizo Nguo na hivyo vidude wanatengeneza.
Waungwana ni "Pitapita ya Mswahili Mitaani" Ilikuwa Coventry. kulikuwa na Mabanda mbalimbali ya Bidhaa , Vyakula na Michezo.
Kwabahati mbaya WaTanzania hatukuwa na Banda.
Nimatumaini yangu siku/wakati mwingine tutakuwa na Banda hata la Mchezo wa Bao,Kijiwe cha Kahawa ile Chunguu yanywewa kwa Vikombe Vidoogo na Kashata.
Ndugu wa mimi/Blogger Mwenza EMU wa Three.Mmmhhh Ushauri wako Naufanyia Kazi.Hahahaha Eti Ndugu wa mimi ananishauri nijiunge na Michezo kama Miereka,Judo,Sarakasi ,Kuogelea na.........Uwiiii Kweli umenichoka, Sikuweza Mikundeni itakuwa Michorokoni? hhahaha na Uzee huu mwili umekomaaa.Hahah Usichekeshe walionuna.
Sina Meengi,Unalolote la kuongezea,Maoni,Ushauri?
Pamoja sana "Swahili NA Waswahili"
Sunday, 26 August 2012
Mswahili Wetu Leo;AIKAROSE MWASHA-Anaishi BELGIUM;NYOTA TUMAINI LETU!!!
NYOTA TUMAINI LETU
Jina: AikaRose Mwasha
Jinsia:Kike
Miaka:12
Utaifa:TANZANIA
Mchezo: Taekwando
KILO: 28 kg- beginners FEMALE
Club: Nong Jang
MAKAZI: Leuven Belgium
MAFANIKIO: MEDALI YA FEDHA
& DHAHABU
Kijana wa kitanzania
mwenye ndoto ya kuwakilisha nchi yake kwenye mashindano ya kimataifa hapo usoni
kwa kupitia mchezo wa mbinu za kujihami wa TAEKWANDO ,anamapenzi makubwa na
mchezo huu aliouanza angali mdogo akiwa na umri wa miaka 9 ,ameshashiriki mashindano madogo
madogo nchini Belgium na kupata mafanikio makubwa kufikia medali ya fedha. Hivi
karibuni alifanikiwa kupata medali ya dhahabu katika mashindano ya Olympic open
Brussels yaliyofanyika Rue Du Lombartzyde
Brussels Belgium
tarehe 27 May 2012.
Sasa hivi anajiandaa na
team yake kwenda Copenhagen
kwenye mashindano ya Wonderfull
Copenhagen yatakayofanyika mwezi ujao.
Wito wake hasa kwa vijana
wadogo akitilia mkazo jinsia ya kike ni kujifunza michezo mbalimbali na kuwa na
ndoto ya kuwa mabalozi kwa taifa lao la TANZANIA .
VIPAJI HUINUA TAIFA
"Swahili NA Waswahili" Tunakutakia kila la kheri.
Mario Van Peebles Exclusive Interview - Tanzania Films Critics Associati...!!!!!!
Mario Van Peebles interview with Tanzania Films Critics Association (TFCA
The link above is about 15 Question and Answer of video
Insightful interview with Film maker/Director/Producer, Actor Mario Van Peebles
and Michael Cohen, talk about their new Movie "We the Party" and
general view of Tanzania Film Industry in including Copyright aspects in combating
piracy problems and their view of films activities here in Tanzania.
Tanzania Films Critics Association
(TFCA)
----------------------------------------------
Nawatakia J'Pili yenye baraka na Amani.Burudani- Mwamba Rock Choir!!!!
Wapendwa Nawatakia J'Pili yenye Baraka,Upendo,Umoja, Amani na Malezi mema.
Basi wakamletea watoto wadogo ili awaguse;Wanafunzi wake wakawakemea.Ila YESU alipoona alichukizwa sana,akawaambia,Waacheni Watoto wadogo waje kwangu,msiwazuie;Kwamaana Watoto kama hawa Ufalme wa MUNGU ni wao.
Neno La Leo:Marko Mtakatifu:10:13-16
"Swahili NA Waswahili" MUNGU ATUBARIKI SOTE.
Subscribe to:
Posts (Atom)