Wednesday, 12 September 2012
Monday, 10 September 2012
KHADIJA MNOGA AKA KIMOBITEL AWABIP WAPENZI NA WASHABIKI WA EXTRA BONGO KWA WIMBO WAKE MPYA ALIOUPA JINA LA "MGENI" NDANI YA MEEDA.!!!
Kimobitel akiimba wimbo wake aliyeutunga mwenyewe unaojulikana kwa jina la "MGENI" ndani ya Meeda Sinza Usiku wa kuamkia leo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba wimbo mpya wa Kimobitel ndani ya Meeda Sinza
Banza Stone AKA Generale akifurahi pamoja na Khadija Mnoga AKA Kimobitel wakati wa utambulisho usio rasmi wa ujio wa Kimobitel
Kushoto ni Athanas mwanamuziki anayekuja kwa kasi ndani ya Extra Bongo, akishoo luv na Kimobitel ndani ya Meeda Sinza.
Safu ya wanamuziki nguli wa Extra Bongo walioimba wimbo mpya wa Kimobitel (Mgeni) wakiongozwa na Ally Choki wa pili kutoka kushoto, wa kwanza kulia ni Rogert Hega Katapila, anafuatiwa na Banza Stone na Kushoto ni Kimobitel.
Kimobitel akiwa na nyuso ya furaha baada ya wapenzi na wadau mbali mbali kumpongeza na kumpokea kwa mikono miwili ujio wake.
Khadija Mnoga "Kimobitel" hivi majuzi alitangaza rasmi kuihama Bendi yake ya Twanga Pepeta ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa na kuhamia Extra Bongo, sababu za kuhama Kimobitel alisema ameamua kurudi Extra Bongo kwa sababu kuna mipango yake ambayo aliianzisha kwa hiyo amekuja kuimalizia kama wimbo ambao aliwahi kuimba wakati anaiimbia bendi hiyo unaotambulika kwa jina la "MJINI MIPANGO" kwa hiyo ameamua kurudi kuja kuikamilisha mipango hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki amesema KIMO KIMO kama wengine wanavyomuita atatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 14/09/2012 katika ukumbi wao wa nyumbani New White House uliyopo Kimara Korogwe jijini Dar es salaam.
Sunday, 9 September 2012
Saturday, 8 September 2012
Siku kama ya Leo da'Sabrina Kiwinga Alizaliwa!!!
Bint Kiwinga kapoziii!!! |
Mhhhh Shangazi langu hiloo,Anatafakari miaka 2. si mchezo!!
OOhh yahh ndiyo mimi Sabrina[SAB'K]!!! |
Siku kama ya Leo Familia ya Bibi na Bwana H.S.KIWINGA wa HOLLAND walipata mtoto wa Kike wakamwita SABRINA!!! da'Sabrina Leo Ametimiza miaka 2.Familia inamshukuru sana MUNGU kwa Yoote,Wanakutakia kila la kheri maishani,Uwe Baraka kwetu na watu wote.
"Swahili NA Waswahili" Tunakutakia Baraka,Amani, Upendo na Makuzi mema.MUNGU awe nawe kila iitwapo Leo.
Burudani ya Leo mambo ya ki DUTCH tuu, hahahaah wapi shangazi Rabia. watachekea kwao....................
Waungwana;Kama unapenda kutuma picha za Sherehe na Mengineyo tumia.rasca@hotmail.co.uk
Pamoja Daima
Thursday, 6 September 2012
Wanawake na Mitindo;Ya Kale ni Dhahabu!!!!!!
Waungwana; Wanawake na mitindo,"Ya Kale ni Dhahabu" Umemuona Mrembo wa zamani?nini Unakumbuka kupitia picha hizi na nini kimekuvutia?
Huo unywele wa kwenye picha ya juu sijui aliweka dawa gani,Zazuu,Alizichoma au........
Huo Unywele wa kwenye Picha ya chini hakuna Dawa hapo.
Unalolote unaweza kuongezea katika Picha hizi? Karibu sana.
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
Yanayoendelea baada ya mauaji ya mwandishi wa channel Ten
Tuesday, 4 September 2012
Waswahili na Maisha Yao;Leo Tupo IRINGA-Village Schools International-Shamba Darasa!!!!!!!!!
"Waungwana, Waswahili na Maaisha Yao". Leo tupo IRINGA.
Watu wa vijijini wengi wao bado ni wanyeyekevu kwa Wageni,Shukrani na Kujitoa.
Hapo wakiimba kwa Sauti Taaamu. Pamoja na Mgeni wao,Wakimshuruku MTALAAMU.
Wewe unafikiri kwanini watu wa Vijijini wengi wao bado wanaukarimu,Shukrani na Unyeyekevu?
Hawajafunguka,Hawaendi na Wakati,Hawajaumizwa au Mazingira yanachangia?
Jee Vipi watu wa Mjini?Yaani ukiachana na mtu mwaka mmoja tuu baadhi yao inabidi Utulize Akili na kuchunguzana upya, kwani Wengi Tabia imebadilika.
Jee Washalizwa sana/kutapeliwa,Ugumu wa Maisha, Waelevu au Wajanja Au.......?
Karibuni sana kwa Maoni/Mawazo,Ushauri na Tuelimishane kwa Amani na Upendo.
[KILIMO KWANZA AU...?]
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.
Subscribe to:
Posts (Atom)