Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 16 September 2012

Nawatakia J'Pili Njema;Burudani-Mamajusi Choir !!!!!!!!!!

Wapendwa nawatakia J'Pili yenye Amani,Baraka,Shukrani na Upendo.
Ondoka,Uangaze;kwa kuwa nuru yako imekuja,Na utukufu wa BWANA umekuzukia.
Neno La Leo;ISAYA:60;1-6.

"Swahili NA Waswhili" MUNGU ATUBARIKI SANA.

Saturday, 15 September 2012

Chaguo La Mswahili Leo;Dully Sykes : Lady Jaydee,Banana Zoro na Papii Kocha!!!!!!


Mabibi wa [doti com] Kileo na Mambo Yao!!!!!!Mama Erik/Kadala.Ndugu wa mimi na Waungwana woote, hapo vipi? bibi katupiaaa.........Mabibi wa leo hawataki,Sangula,Vanga,Mganda,Lizombe,Mbeta, Mdumange. Nao wanaungana na mangoma ya sasa. Vipi ndiyo maendeleo au?
Waungwana; "Chaguo La Mswahili Leo"ni mambo Mchanganyiko.
Hunifahamu sikufahamu iweje leo unipakazie!!!........mambo ya Dully....Banana nae na mambo ya oohh oohh Nzela mwanamama!!!
mmhh ngoja nikanywe Maziwa kwanza...

Waungwana  sina Meengi Twende sotee sasa, kuna lolote unalo lakuongezea,kukumbuka katika nyimbo za Leo?Tuhabarishe/tuelezee!!!!!

"Swahili NA Waswahili" PamojaDaima.

Friday, 14 September 2012

Those Crazy East Africans-Stand up Comedy!!!!!!!!!!!



Naomba niwaletee kwenu link ya Documentary interview iliyofanyike baada ya onyesho kubwa la vichekesho lililohusisha Even 
Bukuku na kundi lake la Vuvuzela akishirikisha wasanii kutoka Kenya na Uganda.


 http://youtu.be/j-BQHJnRfdA

Post documentary interview to the biggest ever Stand up Comedy Show of the Year 2011, happened at The Golden Tulip Hotel 
on FRIDAY the 16th December 2011 in  "Those Crazy East Africans" - Evans Bukuku and his Vuvuzela crew Featuring 
Comedians from East Africa: Mdomo Baggy from Kenya, Uncle Bob from Uganda & Evans Bukuku, Dogo Pepe and Songbird 
ENIKA from Tanzania!!!

Shukrani Sana.

Wasalaam
Emmanuel.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday, 12 September 2012

Tujikumbushe;Baraza la Watoto - Mahojiano na Rais, A,B,,C..!!!!!!!!


Waungwana; Tujikumbushe na kama hujaona,Baraza la Watoto,Mahojiano na Rais wa Jamuhuri ya Tanzania.Muheshimiwa .JAKAYA  KIKWETE.
Kuna lolote,Umejifunza/ unataka kutueleza kupita Video hizi?Karibu sana Tuelimishane kwa Upendo.Video hizi zinaendelea, kuona zaidi na kujifunza meengi ingia;CreativeGenesTZ pia unaweza kufuatana nao kupitia; twitter@creativegenesTz.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Wana habari walipoandamana kwa amani!!!

Habari hii kutoka StarTv, ShukraniTangibovu  

Monday, 10 September 2012

KHADIJA MNOGA AKA KIMOBITEL AWABIP WAPENZI NA WASHABIKI WA EXTRA BONGO KWA WIMBO WAKE MPYA ALIOUPA JINA LA "MGENI" NDANI YA MEEDA.!!!


Kimobitel akiimba wimbo wake aliyeutunga mwenyewe unaojulikana kwa jina la "MGENI" ndani ya Meeda Sinza Usiku wa kuamkia leo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba wimbo mpya wa Kimobitel ndani ya Meeda Sinza
Banza Stone AKA Generale akifurahi pamoja na Khadija Mnoga AKA Kimobitel wakati wa utambulisho usio rasmi wa ujio wa Kimobitel
Kushoto ni Athanas mwanamuziki anayekuja kwa kasi ndani ya Extra Bongo, akishoo luv na Kimobitel ndani ya Meeda Sinza.
Safu ya wanamuziki nguli wa Extra Bongo walioimba wimbo mpya wa Kimobitel (Mgeni) wakiongozwa na Ally Choki wa pili kutoka kushoto, wa kwanza kulia ni Rogert Hega Katapila, anafuatiwa na Banza Stone na Kushoto ni Kimobitel.

Kimobitel akiwa na nyuso ya furaha baada ya wapenzi na wadau mbali mbali kumpongeza na kumpokea kwa mikono miwili ujio wake.

Khadija Mnoga "Kimobitel" hivi majuzi alitangaza rasmi kuihama Bendi yake ya Twanga Pepeta ambayo aliitumikia kwa miezi kadhaa na kuhamia Extra Bongo, sababu za kuhama Kimobitel alisema ameamua kurudi Extra Bongo kwa sababu kuna mipango yake ambayo aliianzisha kwa hiyo amekuja kuimalizia kama wimbo ambao aliwahi kuimba wakati anaiimbia bendi hiyo unaotambulika kwa jina la "MJINI MIPANGO" kwa hiyo ameamua kurudi kuja kuikamilisha mipango hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki amesema KIMO KIMO kama wengine wanavyomuita atatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 14/09/2012 katika ukumbi wao wa nyumbani New White House uliyopo Kimara Korogwe jijini Dar es salaam.

Sunday, 9 September 2012

Nawatakia J'Pili yenye Baraka;Burudani-Angela Chibalonza na Franck Mulaja!!!!!!

WapendwanawatakiaJ'PiliyenyeBaraka,Upendo,Uvumilivu,Msamaha na Kujitoa.
MUNGU asimama katika kusanyiko la MUNGU;katikati ya MIUNGU anahukumu.
Neno la Leo;Zaburi:82:1-8.

MUNGU atubariki soote.

"Swahili NA Waswahili"
Pamoja Daima.