Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 25 September 2012

Siku kama ya Leo Madame,Nounou Alizaliwa;Burudani-Women Burundi Drummers!!!!!!!

Siku kama ya Leo miaka kadhaa iliyopita da'Nounou[Madinna]Alizaliwa.
Madame ya Billy uwe na wakati mwema Leo na sikuzote,Uzidi kuwa Baraka kwa Familia,Majirani, Marafiki na watu woote.MUNGU azidi kukulinda na Akupe sawasawa na Mapenzi yake.
Kwangu Nounou  ni zaidi ya Rafiki.MUNGU anakila sababu ya kutukutanisha.MUNGU amekujalia Wema,Upendo,Kusamehe na Upole kiasi.Ngoja niishie hapa kwani nina Mengi ya Kusema kupitia Wewe.Nimejifunza meengi sana kupitia wewe.Mimi na Familia Yangu Tunakupenda sana MADAME!!!!!!

Waungwana;Undugu si Kufanana au Kuzaliwa Tumbo Moja..Unasemaje Kuhusu Hili?
 Madame-Nounou ni Mswahili wa Burundi.Madame- Rachel-Siwa Mswahili wa Tanzania,TUMEKUWA PAMOJA MIAKA MINGI SASA,MUNGU TUBARIKI SANA!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Shindalo la Uchoraji Kwa Taasisi za Kielimu!!!!!



Image Profession ikishirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kwa mara nyingine inatangaza kuanza kwa muhula mpya wa pili wa Shindano ya Uchoraji maalumu kwa Taasisi za elimu.
Shindano ambalo pia linajulikana Kama: Educational Drawing Competition au Image Profession Educational Drawing Competition, lina malengo ya kuibua vipaji katika fani ya uchoraji kwa kuzingatia uwekezaji kwa watoto na vijana.
Theme/Wazo kuu la mwaka huu: ART IMITATES LIFE au SANAA HUFUATISHA MAISHA
Makundi ya ushiriki
´   Chekechea,
´   Elimu ya Msingi,
´   Elimu ya Sekondari na  
´   Elimu  ya Juu
Kwa maelezo na taratibu za Shindano tembelea Facebook Page/Group “Tanzania Drawing Competition” au wasiliana na BASATA au
DRAWING COMPETITION – IMAGE PROFESSION,
P O BOX 92 DAR ES SALAAM.
SIMU: +255 222 664 740 / +255 713 484 040
/ +255 714 676 217 / +255 716 430 084

Monday, 24 September 2012

Wanaume na Mitindo;-Burudani-P-Square ft. Akon & May D - Chop My Money!!!!







Waungwana;"Wanaume na Mitindo"Mambo hayo!!Vipi wewe Baba/Kaka Vivazi hivi vinakugusa/vipenda? Jee unapenda kuvaa Saresare na Mke/Mchumba,Dada...wako?
Na kina Mama/Dada jee ungependa Mumeo/Mchumba,Kaka na.. wakitinga/kuvaa hivi? jee Saresare vipi?

Jee Wanawake mnakawaida ya kuwanunulia Waume zenu Zawadi au mmezoea kupokea tuu?.

Karibuni sana kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.Mambo haya kutoka kwa Rafiki wa Mswahili;
Thanks my love Tarou:http://www.tarou.sn "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima........


Sunday, 23 September 2012

Nawatakia J'Pili yenye furaha;Burudani-Yu mwema Mungu yu mwema,karen men's Chorate na Gael!!!!


Wapendwa nawatakia J'Pili yenye furaha,Kusifu,kuabudu,kusamehe na kusahau.....Je! waweza wewe kumvua mamba kwa ndoano? Au,kuufunga ulimi wake kwa kamba?
Neno La Leo;kitabu cha Ayubu;41:1-34........Yeye hutazama kila kilicho juu;Ni mfalme juu ya wote wenye Kiburi!!!

"Swahili NA Waswahili"MUNGU NA ATUBARIKI SOOOTE.

Friday, 21 September 2012

Waswahili Wetu Leo-Ilava,Wanawake na Mitindo!!Unapenda Shanga??Jimwage!!!!!!!!!












Waungwana,"Wanawake na Mitindo" Leo Tupo Kinyumbani nyumbani,Si wengine ni Wswahili hawa  Waishio Nje lakini hawasahau ya Kwao.ni Ilava............

Ilava: It Can Be Done


Nisimalize Uhondo wooote, unaswali,Unataka Utoke Ki-

Afrika?Usisite kuwasiliana nao kupitia
Shopping & retail
Chicago, Illinois 60653



+1 773-805-0704
 
 Pia unawezakuwapata Facebook.
Mwanamke mwenzio/Mswahili mwenzio akifanya kitu kizuriri lazima umpe sifa yake!!!!
Wanawake wa Swahili na Mitindo/Majukumu.
Unalolote la kuongezea hapo?
Karibu sana Tunasubiri Maoni,


Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.


"Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima.

Wednesday, 19 September 2012

Wanawake na Mitindo,Leo Tupo Senegal;Burudani-2face - African Queen!!!!!!!!






Waungwana;"Wanawake na Mitindo".leo Ki-dada/mama-Ki Afrikaaaa!!!!!
kwakweli mavazi haya hayamchukii mtu kwa Mtazamo wangu,kila Anayevaa anapendeza,tena Vazi hili linaupa mwili Nafasi na Kujiamini, Au.. weweee unaonaje?
Vipi wewe Dada/Mama ni Mpenzi wa Mavazi haya? wewe Kaka/Baba ungependa Dada/Mkeo au Rafiki yako Atinge hivi?
kwanini Unapenda na kwanini Huyapendi?

Funguka/Tuambiazane..........Mmmmhhh nisimalize Uhondo ngoja nisikilize na wengine...........
Picha hizi nimetumiwa na Rafiki yangu Tarou,yeye si Mswahili bali ni Rafiki wa "Mswahili" kina kaka/baba nanyi nitawarushia Msikonde wala nini.
Thanks so  Much lovely Tarou.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Monday, 17 September 2012

Wanawake na Urembo;Ya Kale ni Dhahabu,Burudani-LES WANYIKA BARUA YAKO!!!!!!


 Waungwana; "Ya Kale ni Dhahabu" Alikuwa kabin'ti Enzi hiizo, sasa ni mama .
 Kuna kitu chochote unakumbuka katika picha hizi? Hizi nguo sijui zilikuwa zinaitwa Bahama au.......?

Karibuni sana Waungwana katika Yoote.kama Unapicha  za  Zamani unataka tuzirushe hapa, Usikonde Tuma;rasca@hotmail.co.uk. 

"Swahili  Na Waswahili" Pamoja Daima.