Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 9 October 2012

Kisa cha Leo na Mswahili;Emu-Three-Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi;Sehemu ya 5!!!!!


Maua alikuwa katulia kwenye chumba huku akimuomba mungu wake, mwanzoni alikuwa anashindwa hata aombe nini. Akawa anajiuliza je nimuombe Mungu  anisamehe kwa hayanmakosa niliyofanya, lakini akajiuliza kichwani makosa gani, na kama ni makosa mbona ni yeye peke yake ndiye anayeadhibiwa, mbona mwenzake waliyeshirikiana naye , hayupo, je na yeye hastahili kuadhibiwa.

Alipowaza hilo akamkumbuka mwenzake, akakumbuka jinsi walivyokuwa wakiandikiana barua, lakini ghafla akawa hamjibu barua zake tena, hasa pale alipoandika kumuelezea jinsi gani anavyojisikia,na kumwambia anaogoa isije ikawa ni mimba. Ilikuwa barua ya mwisho kumwandikia, na hakuweza kupata jibu, na hata alipoandika nyingine, na nyingine, hakiweza kupata jibu kwa mtu aliyetokea kumpenda sana.

‘Hivi huyu mtu yupo aua kapotolea nchi gani, nakumbuka mara kwa mara anakwenda Arusha kwa mjomba wake, ambaye ni tajiri mmoja wa madini,na nia na lengo lake na yeye ni kujiunga kweney biashara hiyo, lakini kwanini asimwambia, au kumjibu baraua zake,lazima nimtafute tusaidiane hili tatizo’akasema huku akiangalia nje kwa kupitia dirishani.

Akawa bado anawaza ni mambo gani kwasasa anahitajika kumuomba Mungu wake, `Au  nimuombe Munguwangu anisaidie nisiweze kuangukia kwenye mikono ya baba, baba ambaye anataka kuitoa roho yangu, bila makosa, ‘ akasema na alipofikia kuwaza hili akatikisa kichwa na akili yake ikawa anajiuliza ‘Ina maana kweli mimi sio mkosaji,hivi kweli sistahili kuadhibiwa kwa kosa hili?’akatulia na kujarabi kutafakari zaidi. Hapo akakumbuka kauli ya baba yake, ambaye kila mara wakiwa naye alipenda kumuasa nayo;

‘Binti yangu nakupenda sana, na jinsi ninavyo kupenda,  nisingelipenda ukaja kuvunja huu upendo nilio nao juu yako, nakuomba  sana usije ukaniangusha, maana kila mtu hapa kijijini anakuona kama mtoto wa mfano, na mimi huwa natamba kwao kuwa  wewe ni binti mwenye akili, binti mwenye nidhamu, binti ambaye hakuna anayeweza kumfikia kwa jinsi ulivyo hapa kijijini’ilikuwa sauti ya baba yake.

Baba yake kweli alikuwa akimpenda, lakini sio ule upndo wa kumdekeza, kwani akifanay kosa alikuwa akiadhibiwa, mpaka anawaza vibaya kuwa baba yake anataka kumuua, na sio kweli anampenda kiasi hicho. Lakini kaam hajafanay kosa, baba yake alikuwa akribu sana na yeye na kila mwaka wakifanya sherehe za shule anakwenda kushuhudia mtoto wake akipewa zawadi ya kuwa mtoto wa kwanza, na wakirudi nyumbani huchinjiwa kuku kama zawadi maalumu. Na alipofaulu kwenda sekondari, baba alimnunulia zawadi nyingi sana.

`Sasa huyu ndiye binti , binti ambaye baba alikuwa akitamba kuwa ndiye binti wa mfano..’, Maua akajikuta akifuta machozi, akaliangalia tumbo lake, ambalo bado lilikuwa halijaonyesha dalili yoyote kuwa kuna kiumbe ndani , akakunja uso na kuanza kujpiga piga tumboni huku akilaani,i hicho kiumbe kilichopo tumboni,utafikiri ndicho chenye makosa akasema;Inaendele ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

Diary 

Yangu

Yakeeeeeeeee!!!!!

"Swahili NA Waswahili"Pamoja Daima...

Monday, 8 October 2012

Mpigie kura Jestina mwana wa George!!!!!!


JESTINA-GEORGE.COM HAS BEEN NOMINATED FOR BLOG OF THE YEAR 2012 @ THE PRESTIGIOUS BEFFTA AWARDS. VOTING HAS NOW STARTED & WILL CLOSE ON THE 22ND OF OCTOBER. IT'S EASY AND IT'S ONLINE JUST VISIT http://www.beffta.com/voting.htm FILL IN YOUR NAME, EMAIL ADDRESS, UNDER CATEGORY CLICK NEWS 4. BLOG OF THE YEAR AND UNDER NOMINEE CLICK AND VOTE FOR JESTINA-GEORGE.COM THEN CLICK SUBMIT YOUR VOTE.

PLEASE VOTE FOR YOUR BLOG, OUR BLOG, MY BLOG TO WIN BLOG OF THE YEAR 2012.

Thank you for your support & God bless you.


LOVE YOU ALL
Jestina George

xoxox

PERFECT LADY SALON YADHAMINI SHINDANO LA BONGO STAR SEARCH 2012!!!!!!



 Mkurugenzi wa Perfect Classic Salon (kati mwenye nguo nyeusi) Bi. Ester Kiama akitoa maelekezo kwa mmoja ya wafanyakazi wa Salon yake jinsi ya kumtengeneza mshiriki wa Epiq Bongo Star Search (EBSS 2012). Perfect Classic Salon imedhamini shindano hilo kwa kuwapendezesha washiriki na kuwapa muonekano mpya wanapokuwa wakiimba stejini.
 Wafanyakazi wa Perfect Classic Salon wakiwasuka na kuwapamba washiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 katika jumba lao lililopo jijini Dar.
 Mwanadada Kulwa ambaye ni mtaalamu wa kusuka kutoka Perfect Classic Salon akiwajibika.
 Gabriel ambaye ni mtalaamu wa make up, kucha, kusuka na kuwasokota wale wenye rasta original.
Nae mwanadada Sabrina ambaye ni mtaalamu wa kushona nywele za akina mama (Weaving) akiwajibika.
---
Na Mwandishi Wetu.
 Perfect Lady Salon yadhamini shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 kwa kuwapamba na kuwapa muonekano mpya washiriki wote walio katika kinyanga'anyiro hicho.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kuwatambulisha wadhamini uliofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa Perfect Lady Salon Bi. Ester Kiama alisema kuwa ikiwa yeye ni mtanzania anayependa maendeleo ya vijana ameona ni vyema kujitoa kudhamini shindano hilo kwa kuwapa washiriki muonekano mpya.

"Nafurahi sana kuungana na Bi. Ritta Poulsen kudhamini shindano hili linalovumbua vipaji vya vijana ambapo mimi, nimechukua upande wa kuwapamba washiriki na kuwapa muonekano mpya wawapo stejini," alisema Ester Kiama.

Hata hivyo aliongeza kuwa wakati umefika kwa Watanzania kuungana mkono pale unapoona mtu anafanya jambo linaloleta maendeleo katika nchi yetu.


Pia Bi. Ester Kiama alisema, Perfect Lady Salon imefungua milango kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya kazi na nao, asisite kuwasiliana nao wanapatikana Kinondoni mkabala na Chuo Kikuu Huria.

Shindano la EBBS linaendelea ndani ya Stesheni ya ITV na sasa wapo katika hatua ya mtoano

Sunday, 7 October 2012

Nawatakia J'Pili Yenye Kheri;Burudani-Nzambe Malamu"Franck Mulaja ,Solomon Mukubwa na Gael.!!

Wapendwa nawatakia J'Pili yenye Upendo,Amani,Umoja na Kweli Daima.
Lakini,kama ilivyo andikwa,Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,[Wala hayakuingia katika Moyo wa mwanadamu;]Mambo ambayo MUNGU aliwaandali Wampendao.

Neno la leo;1 Wakorintho:2;9-16.

"Swahili NA Waswahili"
Neema ya BWANA YESU na iwe Pamoja nanyi nyote. AMINA.

Saturday, 6 October 2012

Chaguo La Mswahilli Leo;Lady Issa-Dunia inamambo na nyingineee.. Anasaidiwa Na Nguza Viking;Ni wewe Pekee!!!!!

Waungwana;"Chaguo La Mswahili Leo"Mambo hayo ya Zilipendwa..Unakumbuka Nyimbo hizi ?Ulikuwa  wapi na Umri Gani weee..Uliziimba na kuongezea maneno yako pale usipoelewa?Bado Zinakubamba/Kuzipenda?Enzi hizo Ulikuwa Unavaajeeee? Kama si Mwaka Wa Watoto Viatu Kutoka BORA au MORO Shuzzzzz..
Kaka Yangu Chacha o'Wambura ananiambia ukisikiliza nyimbo hizi Unajiona KIJEBA...Hahaah.......

Twende Sote  sasa Jua Maisha ni  Mulima eee, Kuna Kupanda na kushuka eee...Bali Kuteleza si kwanguka eee Mtoto wa Mama....Mmmmhhh ngoja niendelee kunywa Mayai Mabichi!!

"Swahili NA Waswahili" Karibu Wooote!!!!

Friday, 5 October 2012

Jikoni Leo-Mitaani-Hot Dog...!!!

Waungwana; "Jikoni Leo" lilikuwa Mtaani, haya jiko hilo moto ukiwa mwingi unapandisha juu kama bembeaaaa..
Vipi Jiko hili kwa Kuchomea Mahindi,Mihogo,Mishikaki/Nyama Choma  na ............
 Mambo ya Hot Dog hayooo mitaani...Vipi wewe kilaji hiki kinapanda/unakipenda?

 Ahh Wadhungu kwa mikate wanaibadili Jina tuu na kuweka vitu tofauti lakini ni Mkate tuu.
 Hahhaha tena Nyumbani wanywaji Bia kwenye Bar wanakula Nyama choma au Michemsho..Wao Ngano kwa Ngano, Bia kwa Mkate.....

Jee Wanywaji mliokuwa Nje ya Bongo/Tanzania Nanyi mnaweza kunywa Bia kwa Mkate?....

Tunasubiri Maoni,Ushauri na Kuelimisha kwa Upendo..!!  

"Swahili na Waswahili" Pamoja Daima.

Tuesday, 2 October 2012

Kisa cha Leo na Mswahili ,Emu-Three;Uchungu wa Mwana Aujuaye Mzazi!!!!!!




Katika maisha haya, unaweza ukakutwa na majanga na kufikia hata kukufuru, ukizania wewe tu ndiye unayeonewa, lakini ugumu na matatizo ya kimaisha yapo katika watu wengi, ila ni kwasababu tu hujawahi kusikia au kukutana na watu kama hao. Nalisema hili pale nilipokumbuka kisa cha huyu mwanadada ambaye nilimkuta akiwa kainama upembezoni mwa nyumba huku kashika shavu na michirizi miwili ya machozi ikiwa imeshajichora mashavuni.

Niliingiwa na huruma nilipoona ule ukaaji aliokuwa kaka huyo binti, hasa kwa binti mkubwa kama yule, na ile nguo nyepesi aliyovaa asubuhi kama ile licha ya baridi kali.  Pembeni yake kulikuwa na ndoo ya maji, iliyo tupu. Niliingiwa na moyo wa huruma nikamsogelea kwa tahadhari, kwani dunia hii haina wema, unaweza ukajitia una huruma, na huruma hiyo ikakutokea puani.

Wakati namsogelea kwa tahadhari,nilikumbuka kisa cha jamaa yetu mmoja, ambaye alienda kusota jela, baada ya kujifanya msamarai mwema, kwa kumoenea huruma binti kama huyu. Yeye alimkuta huyo binti  njiani, akiwa analia, na hali aliyomkuta nayo, ilikuwa ya kusikitisha, kwani kama alivyodai, ana siku mbili , kula hali, anachoambulia ni makombo. Yule jamaa yangu alipomuona kwenye hiyo hali akamchukua kwake, lakini  kabla hajatahamaki polisi hawa wapo mlangoni pake.

‘Tumeskilia wewe umemchukua msichana  wa watu, umemficha hapa kwako , yupo wapi?’ akaulizwa.

‘Afande, mimi nimemuona huyu binti njiani, akiwa analia, nikajaribu kumuuliza ana tatizo gani, akawa hanijibu, lakini kwa hali aliyokuwa nayo ilionyesha dhahiri kuwa ana njaa, nikaona nimchukue kwangu, ili anywe chai, halafu atanielekeza kwao, au polisi ikibidi, kwani hali aliyokuwa nayo hata wewe ungelimuonea huruma, inaonyesha wazi ana njaa, na pia mahala kama pale nilipomkuta hapana usalama’akajitetea huyo jamaa yangu.

Wale maaskari wakaangua kicheko, na kusema;
‘Hivi wewe kweli una akili, ukutane na binti wa watu,tena msichana, badala ya kwenda naye polsi unampeleka kwako, kwanza wewe una mke, au ndio ulitaka awe mkeo wa muda baadaye umeshamuharibia maisha yake unamtelekeza!’ akasema yule askari  huku akiangalia huku na kule kama ataona mke wa jamaa yangu huyo.

‘Mimi ninaye mke, na kwasasa hayupo kaenda kwao,  hivi sasa nipo peke yangu, alikwenda kwao kusalimia.’akajitetea jamaa yangu huyo

‘Kwahiyo ukaona uchukue mwanya huo, kutorosha mabinti za watu,wewe huoni hilo ni kosa kubwa, linalinganishwana kuteka nyara. Na wewe hujui kuwa utakuwa na mtoto kama huyo siku za baadaye? 

’akasema yule askari huku akitikisa kichwa na mwenzake akatikisa kichwa kukubaliana naye.

‘Jamani, huyu binti wala sijamtorosha, sivyo kabisa mnavyozania nyie, kwanza yupo hapo ndani anakunywa chai, hebu ingieni mumuhoji wenyewe‘akasema na wale maaskari wakaingia ili kuhakikisha, na wakamkuta yule binti akiwa anakunywa chai, na alipowaona wale maaskari, akakurupuka pale mezani akitaka kukimbia, wakamshika.

‘Wewe ulikuwa wapi muda wote huo, ulikuwa na huyu muhuni, ndiyo yeye anayekuhadaa kila siku ehe, utatumabie vyema?’akasema yule askari huku kamkazia macho yule binti.

Inaendelea....Kusoma zaidi ingia;
http://www.miram3.blogspot.com


Kwa Visa vya kusisimua na kufundisha, Ungana na EMU-Three... Na;
Diary Yangu.
Yakeeeee!!!!!!!!!

"Swahili NA Wswahili" Pamoja Daima