Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 28 October 2012

Tumalize J'Pili kwa Amani na Upendo;Burudani-Atta Boafo - Double Double na Nyingine Nyingii!!!!

Wapendwa; Tumalize J'Pili hii Vyema,Tuwe na Amani,Upendo,Umoja,Msamaha,Uvumilivu na Shukrani.
Neno la Leo.Mithali;29:7-9 Mambo haya mawili nimekuomba;Usininyime[matatu]kabla sijafa.Uniondelee ubatili na Uongo;Usinipe umasikini wala Utajiri;Unilishe chakula kilicho kadiri yangu.............

"Swahili NA Waswahili" MUNGU Atubariki Soooote

Thursday, 25 October 2012

TANZIA!!!!!



FAMILIA YA  MAREHEMU MCHUNGAJI MWAKIPUNDA WA NGAMANGA IPINDA KYELA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MZEE NSUBISI SAMUEL MWAKIPUNDA (MKURUGENZI WA ZAMANI WA IDARA YA MAELEZO)  KILICHOTOKEA SIKU YA JUMATANO TAREHE 24/10/2012.

MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA NYUMBANI KWA MAREHEMU PUGU KINYEMWEZI DAR ES SALAAM.
HABARI ZIWAFIKIE NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.

KWA MAWASILIANO ZAIDI
+255655994499
BWANA AMETOA BWANA, AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

AMEN

Tuesday, 23 October 2012

Mswahili Wetu Leo; Arba Manillah wa Kukaye Motooooooo!!!!!!!


 Waungwana;MSwahili Wetu Leo ni  Kaka ARBA  MANILLAH.
Ni mwanamuziki anayeishi na kufanya kazi zake Nchini Ujerumani[Chemnitz, Germany].
Arba Alizaliwa na kukulia IRINGA,TANZANIA.
Bendi yake inaitwa "KUKAYE MOTO"
Kujua zaidi kuhusu kaka huyu ingiaKukaye Moto na www.kukayemoto.de Twende sote sasa....
 "WANYALUKOLO"......Kihesa,Mkimbizi,Semtema,Ruaha,Ipogolo,Kigonzile,Ilala,Lugalo.....................Dar-es-salaam,Ilala,Mabibo....

"Swahili NA Waswahili" IRINGA TO GERMANY.




Sunday, 21 October 2012

Tumalizie J'Pili hii Vyema;Burudani-Wagogo mass singing

Wapendwa;Tumalizie J'Pili hii kwa Amani,Baraka,Utuwema,Upendo na Fadhili.
Nchi na vyote viijazavyo ni Mali ya BWANA,Dunia na Wote wakaao ndani yake
.
Neno La Leo;Zaburi;22:1-10.

BWANA wa Majeshi,Yeye ndiye Mfalme wa Utukufu....


MUNGU Azidi kutubariki sana


"Swahili NA Waswahili"
Pamoja Daima

Saturday, 20 October 2012

Chaguo La Mswahili Leo,Mdumange,Chiwoda,Sindimba,Wamasai na Wagogo.Kiasili Zaidi!!!!!

Waungwana;"Chaguo La Mswahili "Leo kinyumbani/Kiasili Zaidi.
Haya twende sote sasa,Lakini wewe unajua kucheza Ngoma za Asili au Unajua Ndombolo tuu?
Unafikiri ipi Ngoma Nzuri zaidi ya Zote Tanzania?
Ngoma ya kwenu Inaitwaje?
Utamaduni Tanzania unaendelea au Unakufa?...

Mtu Kwao Ungana Nami........"Swahili NA Waswahili" Mkataa  Kwao Mtumwa!!!!!!

Thursday, 18 October 2012

Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, Nd Omary Mjenga akutana na Balozi wa Marekani Nchini Siera Leone leo.!!!




Mwakilishi Mkazi wa UNOPS Nchini Sierra Leone, Nd Omary Mjenga, akipiga picha ya kumbukumbu Pamoja na Balozi wa Marekani Nchini Sierra Leone Bw Michael Owen, alipomtembelea leo na kufanya mazungumzo naye.

Bwana Omary Mjenga akiagana na Mh. Balozi wa Marekani Nchini Siera Leone baada ya kumaliza mazungumzo.

Balozi Michael Owen, aliwahi kuwa Naibu Balozi wa Marekani Nchini Tanzania mnamo mwaka 2001 hadi 2004.

Wednesday, 17 October 2012

Wanaume na Mitindo ya Nywele!!!!!!!!




Waungwana
"Wanaume na Mitindo" Leo tuangalie Mitindo ya Nywele, ki-Leo/kisasa..haya Wewe unaionaje? Inakubamba/kuipenda au...

 Jee Wanawake mnasemaje baba watoto, Mchumba,Kaka,Mwanao na Mitindio hii, upi umeupenda zaidi?...
Wenyewe Jee kina Kaka,Baba,Mojomba mnatuambiaje?

 Mengi sina Nawasikilizawenzangu....

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima...

Kuona picha zaidi, ingia kwenye Kibaraza chetu kipya;http://mitindoafrica.blogspot.co.uk/