Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 12 November 2012

Da'CHIKU ETUTU'S BABY SHOWER,Waalikwa[2]!!!!


                                          Da'Chiku MUNGU alikuingiza vyumba vyote....Mrembo mke wa Etutu!!

















Wapendwa mmetokelezea/Pendeza sana na MUNGU awape Moyo wa ushirikiano Daima na Mapenzi.
                                        Swahili na Waswahili Tunakutakia kila lililo Jema na Baraka.MUNGU azidi kuwabariki  katika Uzao wenu.
Bibi na Bwana ETUTU..Wanawashukuru Wooote.
         Picha na Mpiga wetu Bai mwana wa Mussa,Shukrani Mingi.

Mapenzi Na Wapenzi;Burudani-Ali Kiba-MAPENZI YANA RUN DUNIA - Diamond na KIZAIZAI!!!!

Waungwana;" Mapenzi na Wapenzi".Mapenzi ni Raha Karaha?  jee Unampenda uliye naye au Unajikaza tuu ili siku ziende?

 kwanini  baadhi ya Wanawake wengi wanalaumiwa na baadhi ya waume zao eti wakisha zaa/kupata mtoto Mapenzi yanapungua kwa MUME?

 Jee kuna ukweli au Wanaume wanawivu hata kwa Watoto wao?

Karibu sana kwa Maoni/Ushauri na kuelimishana kwa Upendo.

Diamond anasema.....Kizaizai oohh Mapenzi yanauma eee nyie Mapenzi karahaaa Kizaizai.........
Ali Kiba anatuambia
......aaa aEeehhh eeeooohh ....Unatema BIG kwa Karanga za Kuonjeshwaaaa..Mapenzi yana Run Duniaaaaaa..

Mhhhhhh wewe UNASEMAJEE........

 
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima
.
S n W

Sunday, 11 November 2012

Wanawake Waswahili Wa Coventry Wamtakia Kheri na Baraka;Mpendwa wao-Chiku Etutu's Baby Shower!!!!!![1]

           Mwenyewe da'Chiku katika pozi mwanana.



Pozi tofauti mama Kitumbo!

              Mikeki 
                  Kula baba kama si wewe nisingeitwa mama..
                        Kula mama kama si wewe nisingekuwa baba......






                      Zawadi na mkono wa kheri na baraka kutoka kwa Waungwana.....[Eeehh dada yangu unavisa wewee wapi Nana]hahahaaaa
k
Kamati ya Shughuli hii,Mnatishaaaa Cov Mamazzzzzzzz[WWWCUK]
              Picha na Mpiga Picha wetu BAI Mwana wa Mussa mamaaa ya Cov..

Usicheze mbali picha zitaendeleaa nani kavaa nini na nani alikuwepo nani katokelezeaaaaa?

       "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Nawatakia J'pili yenye Baraka;Burudani-Solomon Mukubwa-Uwe nami,wastahili na nyingine!!!!!!!

Nawatakia J'Pili yenye Kheri,Baraka,Amani,Upendo na Umoja.

[1]Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa MUNGU;Maana ni heri kukaribia ili usikie,Kuliko kutoa kafara ya Wapumbavu;Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.
Neno la Leo;MHUBRI:5:1-7.[2]Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako,wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za MUNGU;Kwa maana ,MUNGU yuko mbinguni, na wewe upo chini, kwa hiyo maneno yako na yawe machache.
"Swahili NA Waswahili"
MUNGU yu Mwemaaaa.

Saturday, 10 November 2012

Chaguo La Mswahili Leo;Jagwa Music - Mwana wa Kitwana,Kichwa cha Nyoka na Lady jaydee kitu Mtarimbo!!!!!

Waungwana;"Chaguo la Mswahili Leo" Mambo ya Mnanda/Mchiriku na hii ya JIDE sijui niiteje Chakacha au........Naomba mnisaidie.

 Sina Meengi saana.Kama Umeguswa au unalolote unalokumbuka jimwage tuu.....


Twende Soote sasa. Ilala salamu zao...Migomigo salamu zao Temeke wasalimieeee  oohh...
Mmmhh huu Mnanda ukipigwa kigogo watu Ilala hamlali.. 

 "Swahili NA Waswahili" Sereeeeebukaa.