Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 7 December 2012

Nderemo Na Vifijo kwa Kaka Frank Mungo'ngo' Na da'Levina Kimwaga!!![2]





































Waungwana;ni Bwana na Bibi Mungo'ngo' sasa......

Picha za pamoja na Wazazi,Ndugu,Jamaa na Marafiki.

Bwana na Bibi Mungo'ngo' wanasema Asanteni woote, kwa Maombi/Sala,Michango,Kujumuika na katika Yooote.

Hawana cha kuwalipa bali ni kuwaombea kwa MUNGU awaongezee pale palipopungua na awalinde kila iitwapo Leo.........

Mtawasamehe kama kulikuwa na makwazo/kukosea,Haikuwa kusudi lao.  kwani Binadamu hatujakamilika.

Wanawapenda  Wooote!!!!!!!!!

       
 Timu Nzima ya "Swahili Na Waswahi" na Wapenzi/Wadau Tunawatakia Masiha Mema.
                                            Pamoja Daima.

Thursday, 6 December 2012

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-Mapishi ya Meat Roll - Recipe of (in Swahili subtitled in english)!!!!!



Waungwana;"Jikoni Leo" ni Tupike Pamoja wametuletea............

Mapishi ya Meat Roll.....


Hakuna kinachoshindikana Kujaribu ndiyo kujifunzaaa...pia usisite kuuliza.

Kujua Meengi ungana na da'Sophi kupitia;
www.tupikepamoja.com/Tupike Pamoja


Mhhhhh Tamu saaaaaana!!!!!!!!!
             
"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana. 

Wednesday, 5 December 2012

Nderemo Na Vifijo kwa;Kaka Frank Mungo'ngo' Na da'Levina Kimwaga!!!!![1]

           Da'Levina na Mpambe wake  wakielekea Kanisani.
         kaka Frank na Mpambe wake wakisubiri
  Mmmhhh mmependeza sana
      Wametulia ndani ya Nyumba ya Ibada
   Yaanii wee acha tuu!!!!
        Tuependezaaa Hahahaahaa 
             Viapo..
             Mmmmhhh Mke Mkeo kaka Frank......
   Naona Mchungaji Hiza yupo makini....
                Pingu/Pete...........
         Hahahahah Busu la kwanzaaaaaaa..
   Hahahahahhhhh   Mr&Mrs Mungo'ngo......MUNGU asimamie Ndoa yenu!!!!!!!
     MmePendeza sana Wapendwa... 
Mchungaji Hiza,Wapembe na Ma-Arusi MUNGU  awe nanyi...
     Furahaaaaa
  Mmmhhhh Mmependezaaaaaaaaaaaa...
   Uwiiiiii Tumemalizaaaaa sasa...

      Haya Mr&Mrs Mungo'ngo'
    Nzuriiiiiiii kupita Maelezooooooo...
                 Da'Levina na Wapambe....
      Umenoga dadake!!!!
Pendeza mnoo babake!!!
                   Mapoziii kwa Raha zako.....
          Sasa lazima ujidai babake!!!!!!!
         Safari ya kuelekea Kwenye Ukumbi sasa.....
         Ukumbini.......
    Hapo vipi...Hapo sawa sawiaaaa...Mr&Mrs Mung'ngo'.

Waungwana;Wapendwa wetu kaka Frank na da'Levina, Wameungana kuwa kitu kimoja/Kufunga Ndoa.
Alichokiunganisha MUNGU  Binadamu hawezi kukitenganisha. Sasa ni Bwana na Bibi Mungo'ngo'.


Mimi na Familia Yangu,Tunawatakia kila lililo jema,Baraka,Amani,Upendo,Huruma,Samahani,Asante,Uvumilivu, Muwe Pamoja kwa kila Shida na Raha.Mkazae Matunda Mema.

Picha Zitaendelea Usicheze mbali...

"Swahili NA Waswahili" Pamoja saaaana.

Friday, 30 November 2012

Kisa Cha Leo; na Mswahili Emu-Three-Uchungu-wa-mwana-aujuaye-ni-mzazi-31!!!!



Waungwana; Si Mwingine ni Emu wa 3. "Kisa cha Leo" ni Uchungu wa Mwana.....Inaendelea,Si mimi ni yeye  na 

DiaryYangu [Yakeeeee!!!!]



Marejeo: Tukumbuke hiki kisa alikuwa akisimulia yule binti niliyekutana naye akiwa kajiinamia kashika shavu, ….akiwa kasimuliwa na mama yake. Huyu binti kwa hali aliyokuwa nayo, alifikia hadi kukusudia hata kujiua.

Binti aliona kabisa , kuwa maisha kwake hayana thamani tena. Na binadamu anapofikia hapo, ujue kweli kuna jambo…nani asiyependa kuishi, hata yule anayekusudia kujiua, muda roho ikitaka kutoka, huwa anajitahidi kuiondoa ile kamba shingoni, lakini anakuwa keshachelewa, siku yake imeshafika, inabidi aonje umauti…na jamani kutoka kwa roho sio kitu cha mchezo.

Katika kisa hiki utagundua kuwa kuna mwanamama hapo ambaye ana jina hilo hilo, …jina ambalo nilisikia akiitwa huyu binti na mama yake mdogo, wakati namuulizia kuhusu maisha yake, kwanini imetokea hivyo, sasa tuendelee na kisa chetu, ………….

*********

‘Mimi sikujua kabisa huyo baba mlevi ninayeishi naye sio baba yangu wa kunizaa, kumbe alikuwa ni baba wa kufikia, hayo niliyajua baadaye, wakati najiandaa na safari ya kuja kuishi huku Dar, mji ambao kila mmoja kule kijijini alitamani kuja kuishi.

Mama yangu aliniambia huyo baba ndiye aliyekuja kumuokoa pale alipoachwa pale porini…..ili wenzake wafike huko wanapohitajika kwa wakati muafaka, na baadaye watarejea kumchukua, au kumtafutia sehemu ya kumuhifadhi.

Wakati kaachwa pale, akiwa kachoka, kwani mwili ulikuwa hauna nguvu, baada ya safari ndefu, baada ya mapigano, na yeye kujitolea kumsaidia huyo jamaa aaliyeficha sura yake kwa kofia ya ngozi ….na haat kujeruhiwa tena…akawa anatamani kulala tu.

‘Wewe pumzika hapa, na utakula nyama hii…mimi nahitaji huko kwetu haraka, leo najua inawezekana ikawa siku ya mwisho, nimeota kuwa nahitaji haraka sana….na kama ulivyoona, hawa watu walikuja kuniua, lakini tumeweza kuokoka…..ngoja nifike huko nyumbani haraka, halafu nitarudi kuhakikisha kuwa upo mikono salama….’akasema.

‘Sawa wewe nenda tu, na nakutakia mafanikio mema, mungu yupo pamoja na wewe, ila ninachokuomba ni kuhusu mtoto wangu…..naomba siku ukija, uje na mtoto wangu, usije bila ya kuwa na mtoto wangu….’akasema huyo mwanamama.

‘Naahidi nitafanya hivyo…na wewe hakikisha unakuwa salama, usiondoke, hapa, …hapa ni salama zaidi’akasema na akambusu kichwani na kuondoka. Huyu mwanamama alikaa pale kwa muda, halafu akaona akatafute maji ya kuoga, maji yaliyokuwepo pale yalikuwa ni machache, ….........
Endelea kusoma Zaidi,Ingia;http://miram3.blogspot.co.uk/

                           "Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaaana.