Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 31 December 2012

Shukrani Zangu na Nawatakia mwisho wa Mwaka,Uwe Mwema na Mwanzo Mzuri kwa Mwaka Ujao;Burudani-Sarah K - Niinue (Mbele Ninaendelea)na Nyingine Nyingi!!!!!!

Namshukuru sana MUNGU kwa yote katika mwaka huu,Yeye ni kila kitu Maishani mwangu.....
Neno;Zaburi:111;1-10;
Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,Wote wafanyao hayo wana akili njema,Sifa zake zakaa milele!!!!.

Nawashukuru Familia Yangu,Ndugu,Jamaa,Marafiki,Ma-blogger,Wapenzi/Wasomaji/Wafuatiliaji[Wapendwa/Waungwana]wa Swahili NA Waswahili  na Mitindo Afrika .Wote wanaonifahamu kwa Namna moja au Nyingine.

Nikutake Radhi/kukuomba Msamaha wewe niliyekukosea/kukukwaza kwa namna yoyote ile,Haikuwa kusudi langu kusababisha hayo ni Hali ya Kibinadamu tuu.Nami nichukue anafasi hiiKusamehe/ kusahau Makwazo, Mapito yote ni Changamoto za kimaisha na Tuanze Upya

.MUNGU azidi kukubariki wewe unayesoma hapa na Wengine woteee!!!!

"Swahili NA Waswahili"
MUNGU atubariki Sote na Pamoja Daima.
S n W

Friday, 28 December 2012

Jikoni Leo,Afya na Jamii; Na Kaka John Haule-Jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya.


Jinsi ya kutengeneza maziwa ya soya.

Baba karudi ni makala fupi fupi ambazo zitakuwa zinatoa mwanga kwa jamii kujifanyia mambo yahusuyo afya na maisha bora kwa ujumla wa ustawi wa jamii ya watanzania kila wiki katika uwanja huu. Lakini la kufurahisha zaidi ni kuwa, hata kama unakusudia kufanya kitu Fulani lakini hujui namna ya kufanya basi kutakuwa na fursa kwako msomaji kutuletea maswali ambayo naahidi yatajibiwa yote ili kuharakisha maendeleo ya Taifa letu. Uwanja huu utaitwa “Baba Karudi” ukiwa na maana nitakuwa natoa kile nilichopata katika safari zangu duniani kote ambako shughuli yangu kubwa ni kukutana na wataalamu wa mambo mbali mbali na kufanya mahojiano nao halafu nakuja kuwaletea watanzania wangu hapa vile vile nitakuwa nayapeleka maswali yenu wasomaji juu ya yale mnayotaka kuyafanya lakini hamjui yanafanywaje.. Nakuomba usiende mbali.
Leo nimekutana na Bi Carole Bruzzano toka www.eHow.com. Nimefunga safari kuja Canada kupata ukweli juu ya Soya kuwa maziwa safi na bora kwa afya za walaji. Yeye anasema:

Soya inatumika duniani kote katika mapishi mengi mbalimbali ikiwemo kutengeneza maziwa na kuungia kitoweo kama nyama na samaki au kama mbadala wa vitoweo hivyo kiafya kwa mlaji.
Anasema kutengeneza maziwa ya unga ya soya ni kazi ndogo sana ambayo inaweza kukugharimu kama dakika 60 tu. Wenye viwanda vikubwa hupitia hatua nyingi kutengeneza maziwa hayo ya unga ya soya. Lakini wewe unaweza tu ukatengeneza mwenyewe nyumbani kwako tena kwa kutumia vifaa rahisi vinavyopatikana bila kuazima kwa jirani.
Wewe unatakiwa uanze na kuzisafisha soya kwanza, halafu weka juani zinyauke kidogo ili ngozi ya soya ilegee na kasha umenye ngozi zote, uoshe tena na uzikaushe mpaka zikauke kau! Hapo tayari utakuwa umeshaandaa soya kusagwa na kuwa maziwa ya unga tayari kupeleka mahotelini na majumbani kwa matumizi.
Bi Carole anasema unahitaji kuwa na vifaa hivi:
1.     Lazima uwe na kikaango ili uzikaange soya zako kabla ya kusagwa.
2.     Unatakiwa pia uwe na blenda au kinu cha kutwangia na chekecheke ili soya iwe unga laini sana
3.     Mwisho tayarisha vikombe viwili au vitatu vya soya
4.     Maziwa halisi japo nusu kikombe kwa ladha na harufu.
Kaanga soya yako katika kikaango angalia zisiungue.zikaange kwa dakika 10 hadi 15 na utaona kuwa zimeiva kwa kubadilika rangi na kuwa kahawia basi ipua na ziache zipoe kidogo kabla ya kuanza kuzisaga.
Saga soya zako, chekecha mpaka upate unga laini sana, ukimaliza weka katika chombo kikavu na kisafi. Sasa chukua maziwa HALISI nusu kikombe na tia katika soya halafu changanya na anika mpaka mchangavyiko huo umekauka.
Mwisho utaona unga umekauka lakini bado una madonge. Yapukuchue kwa mikono safi  halafu tia soya katika mkebe safi tayari kwa matumizi kama maziwa halisi.
Faida za Maziwa ya soya
Unaweza kuanzisha biashara ya kuuza maziwa kama wewe ni mama ntilie au una hoteli au aina zingine za biashara ya vyakula na ukapata faida kubwa bila kuwa na wasiwasi wa kupata hasara.
Maziwa ya soya ni mazuri ukilinganisha nay a wanyama kwa kuwa hayana sukari asilia iitwayo Lacoste ambayo sio nzuri kwa afya hivyo wenye aleji na maziwa ya kawaida basi ndio muda wao wa kujidai na maziwa haya.
Maziwa ya soya yana protini karibu sawa kabisa na ya wanyama lakini haya yana protini ya mimea tofauti na ile ya wanyama ambayo si nzuri kwa afya. Protini ya mimea ni nzuri mwilini kwa kuzuia upotevu wa calsiam kwenye mkojo na kukusaidia usipatwe na magonjwa ya maumivu ya mifupa. Wenye kisukari ndio maziwa yao haswa.
Maziwa ya soya hayana mafuta yenye sumu (saturated fats) wala lehemu. Hivyo ni maziwa yanayowafaa wagonjwa wenye maradhi ya moyo sana.
Maziwa haya bado Bi Carole anadai kuwa ni kinyonya sumu mwilini kijulikanacho kama “isoflavones” ambacho huzuia uzee wa kizembe, maraghi ya mifupa na kansa za aina nyingi mwilini.
Mtu akinywa kikombe kimoja cha maziwa ya soya basi ajue kuwa ana 20%ya isoflvones ambayo katika maziwa ya wanyama hamna!
Hivyo leo tunaishia hapa kwa kuwaasa kujitengenezea maziwa ya soya badala ya kuharibu pesa ambayo ni ngumu sana hasa kwa kipindi hiki. Lakini pia tumefungua rasmi ukurasa ambao tutautumia wasomaji kuuliza namna ya kufanya jambo lolote ulitakalo. Wiki ijayo nitakuja na “JINSI YA KUJITENGENEZEA SODA YOYOTE” au kwa lugha ya wataalamu ni “how to carbonated drinks” ambayo itatusaidia kupunguza manunuzi ya soda kipindi hiki cha jua kali na pia tutaongelea faida na hasara za kunywa soda pia.
Asanteni kwa kunisoma na tuonane juma lijalo.

John Haule ni mpelelezi binafsi (Private investigator) anayejihusisha na tafiti zenye suluhisho kwa matatizo ya kijamii. Unaweza kumpigia kwa miadi ya ushauri juu ya tatizo lolote linalokusumbua kibinadamu. Anapatikana Car Painters - Temeke Stereo, Sandawe Street, jirani na Dr. Massawe. Simu: 0768 215 956 au email rumoursafrica@gmail.com


        "Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Wednesday, 26 December 2012

Mfululizo wa Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics:John F Kitime (2)!!!


 Muendelezo wa 147 Critics ambapo leo tunamsikiliza mdau muhimu na makini kwenye Muziki wa Dansi na kwa 
upande mwingine kwenye Filamu akielezea kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147 
yanayogusa Muziki na Filamu.

Tusikilize 147 Critics:John F Kitime (2)  akiwa ni mtu wa pili kuelezea maoni yake.


Msikilize vyema John F Kitime uweze kufahamu vyema yale anayoyajuwa na anayodhani ni muhimu kuwa sawa katika mabadiliko ya sheria hii!






Mahojiano haya na Ndg John F Kitime yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali
mapato.

kwa Maelezo zaidi ingia;TheImageProfession 

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Sana.

Monday, 24 December 2012

Nawatakia Kheri na Baraka;Christmas Njema!!!!!!!

Wapendwa/Waungwana,Ndugu,Jamaa na Marafiki;
Nawatakia  Christmas Njema,Kheri,Baraka,Amani,Upendo,Furaha,Umoja,Fadhili,Shukrani,Msamaha na Upole Kiasi.
MUNGU awe Nanyi/Nasi Daima!!!!

"Swahili NA Waswahili"
Tunawapenda Woooote.

Jikoni Leo;Tupike Pamoja-Recipe of Chicken Wings with Homemade Barbecue sauce - Mapishi ya (In Sw...!!!!!!



This is a video showing how to cook Chicken wings with Homemade Barbecue sauce, for East-African users and all the swahili speakers all around the world. It's also subtituled in English. Please, subscribe to our channel if you like it. We are working to offer you more video-recipes in swahili, in our Youtube channel and in our web-site www.tupikepamoja.com

Mmmmhhhhh Tamu Saaaana.

                "Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaaana

Sunday, 23 December 2012

Nawatakia J'Pili Njema na Maandalizi Mema ya Christmas na Mwaka Mpya;Burudani-Upendo Group Kijitonyama - Hallelujah Tunaimba na Nyingine Nyingi!!!!!!




Wapendwa;Nawatakia J'Pili Njema,Upendo,Baraka,Amani na Maandalizi Mema ya Christmas na Mwaka Mpya.
Ndugu zangu nawasihi,Waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza;Mkajiepushe nao.

Neno La LeoWarumi:16:17-20 Naye  Mchungaji wa Amani atamseta Shetani chini ya Miguu yenu.Neema ya BWANA wetu YESU Kristo na iwe Pamoja nanyi.[AMINA].

                                      "Swahili NA Waswahi" Mbarikiwe Sana.

Saturday, 22 December 2012

Mahojiano ya Wadau wa Filamu na Muziki;147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1)


 Mfululizo wa 147 Critics ambayo ni  mahojiano ya wadau wa Filamu na Muziki yaliyofanywa na TFCA-
Tanzania Film Critics Association(On line Platform) kuhusiana na marekebisho ya sheria ya ushuru wa bidhaa Sura 147
ambayo yatapelekea kuanzia mwezi wa January 2013 bidhaa zote za Filamu na Muziki zilizopo hapa Tanzania kuwekewa 
Stamp/Sticker kwa ajili ya Kurasimisha,Kumpatia kipato halali msanii na Kukusanya mapato ya serikali yanayotokana na 
uuzaji wa kazi husika.
Sheria hii ina changamoto nyingi ambazo kama hazitatatuliwa zinaweza kuifanya sheria husiaka isfikie malengo yake,Je 
wadau wanasemaje kuhusiana na hilo?

Tusikilize 147 Critics : Dr. Vicensia Shule (1)  akiwa ni mtu wa kwanza kutupa maoni yake kupitia Video hii;


Mahojiano haya yametokana na
-C. Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147
98. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho
katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
ii. Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda
mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na
kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya. Ili kutatua tatizo
hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza
kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa
nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na
hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of
artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na
vipaji hapa nchini. Aidha, Mamlaka ya Mapato itaweka
stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji wa kazi hizo uwe
rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili
kutokana na kazi zao. Vilevile hatua hii itaiingizia serikali
mapato.
80
Kwa kuwa yanahitajika maandalizi ya kutosha ikiwa ni
pamoja na kurekebisha sheria na kanuni mbalimbali,
utekelezaji wa hatua hii utaanza rasmi tarehe 1 Januari,
2013.

Tunaangalia uelewa wa wadau kuhusiana na hili na nini kifanyike ili kuweza kuboresha sheria husiaka ili iendane na taratibu na miongozo itakayoweza kuleta ukombozi wa kweli.
           

 Kujua Zaidi Ungana na mwenzangu;TheImageProfession
              
  "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.