Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 20 February 2013

Jikoni Leo;Tupo Ghana- How to make Fu Fu!!!

w


Waungwana;"Jikoni Leo"..Tupo Ghana!!!!!!Unajua kupika FU FU wewee..kazi kwako..ukitaka Kujua Uhondo wa ngoma ......................

"Swahili Na Waswahili" Karibu Saaana.


Tuesday, 19 February 2013

Mapenzi na Wapenzi;Mr and Mrs - Nollywood Movie,Umefanikiwa kuiona hii?



Waungwana;Mliokuwa  na Ndoa na Mnaotarajia na Mnaofikiria na Mliofikia na.........

Kama hujabatika kuina hii..Naomba upatapo muda kidogo ichungulie.....
Na kama wewe ulibahatika kuiona..Jee umejifunza nini? nawe ukishaiona  Tunaomba utuambie nini umejifunza?.

Swali la Kizushi;Ndoa ni NINI?

Karibuni sana katika Yote!!!!!

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Saaana.

Sunday, 17 February 2013

TAARIFA YA INSPEKTA JENERALI WA POLISI SAID A. MWEMA KWA UMMA KUHUSU TUKIO LA KUUWAWA KWA PADRE EVARISTI MUSHI ZANZIBAR TAREHE 17 FEBRUARI, 2013


Padre wa Kanisa la Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Marehemu Evarist Mushi.


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema akitoa taarifa ya jeshi hilo mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi hilo leo mchana.
 
 
……………………………………………………….
Ndugu Wanahabari,
Nimelazimika nizungumze nanyi kuhusu tukio la kuuwawa kwa Padre Evaristi Mushi wa Kanisa Katoliki Zanzibar lililotokea leo asubuhi tarehe 17 Februari, 2013 eneo la Mtoni mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo watu wasiofahamika walimpiga risasi Padre huyo alipokuwa anaenda kusalisha ibada katika kanisa la Betras. Baada ya tukio hilo kutokea alikimbizwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja, ambapo baadae alifariki dunia. Tukio hili ni baya na la kusikitisha.
2 Kufuatia kutokea kwa tukio hilo na kujirudiarudia kwa vitendo vya kuwashambulia na kuwadhuru viongozi wa dini na uchomaji wa nyumba za ibada, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tumeanza uchunguzi wa kina wa kuwatafuta wanaohusika na matukio hayo.
3Hivyo, nimetuma timu ya wataalam waliobobea kwenye masuala ya upelelezi na oparesheni kutoka Makao Makuu ya Polisi, kwenda kushirikiana na timu ya wataalam iliyoko Zanzibar. Hadi sasa watu watatu wananshikiliwa kwa mahojiano.
Jeshi la Polisi limeimarisha doria maeneo yote hapa nchini na tunafuatilia mienendo na kuakamata watu wote wanaochochea, kufadhili, kuhamasisha na kushiriki katika vitendo vya uhalifu, vurugu na fujo.
Tukiwa katika kipindi hiki, nawaomba wananchi wote hapa nchini kuwa watulivu wakati suala hili linaposhughulikiwa kuhakikisha kwamba wahalifu hao wanakamatwa na sheria inachukua mkondo wake.
Naomba nitumie fursa hii pia, kuwasiliana na wananchi wenzangu wenye taarifa zitakazosaidia wahalifu hao kukamatwa kutupa ushirikiano kupitia namba zetu maalum za simu zifuatazo 0754785557 au 0782417247 na namba za makamanda wa mikoa na vikosi, ili kuhakikisha kwamba amani, usalama na utulivu vinadumishwa hapa nchini.
Nawashukuru wananchi wote ambao wamekuwa wakitupa ushirikiano.
AHSANTENI SANA.

Habari na;KapingaZ blog
Asante.

Thursday, 14 February 2013

Siku kama ya Leo da'Nadia Nyembo Alizaliwa[miaka 3]!!!!

Mwenyewe da'Nadia..

Ndiyooo nina miaka 3 sasa wapendwa...

Hata mimi ninamapothiii si Naomi peke yake..hapa vipi Waungwaaaa?

Kama kuna mtu kakosaa nyingine hiiiiiiiiii

Wakitafakari jambo.....

Tabasamu mwanana na Mwalimu...

Mmmh inapendezaa..
Duhh mwalimu wangu mimi nilikuwa namuogopaje? kwanza muda wa kukupakata anao?
Hahahhaa hapana chezeyaST.Government.........

Eti mlikuwa mnasema  mimi Nadia huwa si cheki....sasa manasemaje na mapothii ndiyo hayooo chachaaaaa!!!

Waungwana da'Nadia Nyembo alizaliwa siku kama ya leo ya WAPENDANAO!!!
Ni miaka 3 leo ametimiza...Nadia na Naomi ni Mtu na dada yake,Wamezaliwa mwezi mmoja wamepisha Tarehe kidogo tuu.

Wazazi/Familia..wanaMshukuru sana MUNGU kwa zawadi hii na meengi aliyowatendea..Nadia MUNGU akubariki na kukulinda siku zako zote,Uwe mtoto mwema kwao na kwajamii pia.

Nasi Tunakutakia Maisha/Makuzi mema,Baraka na Amani kila iitwapo Leo.
Uwe Baraka na Neema kwa Wazazi na watu wote..Uwe Kichwa na si Mkia.
Grote moeder houdt van te.
Gezegend worden!!!!!!!!!!!


 hahahhha Oiiii[Mevrouw Mija,U ook lachen!!!!]

Waungwana kaazi kwelikweli...Mambo ya Lugha haya..
tunarudi palepaleeeee mtoto kujua Lugha ya wazazi ni Muhimu?

Sasa tutashindwa hata kuwasiliana mwehhh...
[Niwashukuru wazazi hawa.hata nikipiga simu naamkiwa..Shikamoo ma'Mkubwa]


Lakini kila mtu ana maamuzi yake kwenye malezi yake au....

Nini  Maoni/Ushauri  wako?
Karibuni sana Tuelimishane kwa Upendo.


"Swahili NA Waswahili"Amani na Upendo.

Jikoni Leo, na Tupike Pamoja;Recipe of Baked sea bass with potatoes - Mapishi ya (In Swahili, subtitl...!!!!!!





This is a video showing how to cook a baked sea bass or any kind of fish with potatoes, for East-African users and all the swahili speakers all around the world. It's also subtituled in English. Please, subscribe to our channel if you like it. We are working to offer you more video-recipes in swahili, in our Youtube channel and in our web-site http://www.tupikepamoja.com/

Mmhhhhh Tamu Saaana!!!!!!!!!!!!

                 "Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday, 13 February 2013

Da'Naomi Nyembo Atimiza miaka 5.!!!!!!!!

Mwenyewe da'Naomi Nyembo..
 
Ahhh..ndiyo nina miaka 5........

Mapothii na Rafiki.....

Urafiki hauchagui Rangi,Utaifa, Dini wala kabila..mbele za MUNGU wote ni watoto wake....

Zawadi kwa Wapendwa Marafiki na Wanafunzi wenzie..Tujifunze kushirikisha watoto katika Utoaji na si Kupokea tuu.


Ahhhhh mwenyewe  da'Rabiah..Mzaa Chemaaaa..mamake Naomi na Nadia..Muke ya Nyembo ...Mutoto ya Abuu Jumaa Mujukuu wa Tuwa!!!!

Waungwana Mtoto wetu
NAOMI NYEMBO..Ametimiza miaka 5..

Wazazi/Familia.Inamshukuru sana MUNGU kwa zawadi ya kuwa na NAOMI..MUNGU azidi kumlinda na kumbariki kwa kila jambo.Awe Baraka kwao na kwa Jamii Pia.

Da' NAOMI nasi tunakutakia kila lililojema naAmani kila iitwapo Leo, Uwe mtoto mwema  na Ufanikishe Malengo yako.
Uwe Kichwa na si Mkia,Ukue na Kuongezeka Imani.


Wazazi/walezi hatua gani ya makuzi ya mtoto wako huwezi kuisahau?
Alitambaa/hakutambaa,Alichelewa kutembea,Alikuwa Mlizi/kulia sana,Kutokulala,Utundu,Kupenda/kutopenda Kula na...............

"Swahili NA Waswahili"Upendo na Umoja.

Sunday, 10 February 2013

Natumaini mlikuwa na J'Pili Tulivu..Pole kwa Wote waliopatwa na Msiba;Burudani - Ambassadors of Christ Choir Rwanda, Ni Kwanini? na Nyingine Nyingii!!!!

Wapendwa J'Pili ya Leo tuwaombee wenzetu waliopatwa na Misiba shida na Tabu..MUNGU awape Nguvu kwa wakati huu Mgumu kwenu..

Kuna mwenzetu Amefiwa na MUME na Mwingine Amefiwa na BABA yake Mdogo Na Wengine wote waliopoteza Wapendwa wao.....

Tumshukuru MUNGU  siku zote kwa ajili yenu  nyote,tukiwataja katika maombi yetu.

Neno La Leo;Waraka wa Kwanza wa Paulo Mtume kwa WATHESALONIKE:1:1-7
.Wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya imani, na taabu yenu ya upendo, na saburi yenu ya tumaini lililo katika BWANA wetu YESU Kristo, mbele za MUNGU Baba yetu.....Endelea....

"Swahili NA Waswahili"
Mbarikiwe Sana.