Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 10 March 2013

Tumalize J'Pili Vyema na Happy Mothers Day;Burudani-MIRIAM- anaitwa kila mtu na Mt.Cesilia!!!!!


Wapendwa/Waungwana..Leo Tumesheherekea/Tunasheherekea Siku Ya MAMA[MOTHERS DAY]..!!!!Niwatakie kila la kheri na Baraka kina MAMA Wote!!!!!!!

Na Wasiokuwa Mama lakini wanahitaji kuwa MAMA .MUNGU awajaalie   nanyi...Mtaitwa MAMA.

Pia Ahsanteni Sana Kina BABA Kwa  Yote,Kwani Pasipo Nyie Tusinge itwa MAMA!!!!.

Tumalize  J'Pili  hii Vyema na Kumshukuru MUNGU.... [1].BWANA akasema na Musa, akamwambia,[2]Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote,kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli,Wa binadamu na wa Wanyama; ni wangu huyo..

Neno La Leo;KUTOKA:13:1-16.Jambo hilo litakuwa ishara mkononi mwako,na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri, kwa  uwezo wa mkono wake.

"Swahili NA Waswahili"
Mbarikiwe Saaana.

Friday, 8 March 2013

Leo ni Siku Ya Wanawake Duniani;Wanawake Tusiogope!!Leo Tumuangalie da'Mwandale!!!!!!!





Waungwana; Leo ni Kilele cha Siku ya "WANAWAKE DUNIANI" Nami nichukue Nafasi hii kuwatakia Mafanikio,Ubunifu,Uwezo,Maarifa na Baraka katika Utendaji na Maisha  Mema...

WANAWAKE TUSIOGOPE,Kujaribu,Kutenda,Kuamua,Kuuliza/Kujiuliza,Kuchekwa na Kufanikisha Malengo/NdotoZetu.....

Hakuna aliyezaliwa anaweza..wote walijifunza na kulikuwa na Chanzo/Mwanzo mpaka Wale Waliofanikiwa kutimiza Ndoto zao zikawa kweli.....Na kwenye Safari ya Maendeleo kuna Mapito/Changamoto nyingi sana mpaka ufikie Malengo...
Kuna kukatishwa Tamaa,Kuchekwa na Kubezwa.....

Pia ni Vigumu kwa walio wengi kujitambua Yeye anakipaji,Mzuri kwa kufanya nini na Kujikubari au Kukubarika kwa Siku za Mwanzo..Lakini hakuna linaloshindikana mbele za MUNGU..Kama ni Safari uendayo ni yako au si yako Itajulikana Tuu...Hakuna cha Kazi hizi za KIUME au KIKE..
WANAWAKE wa LEO Wanajitahidi Sana Sana  Kujitoa/ Kujihusisha na Mambo mbalimbali ili kufanikisha NDOTO zao na Kuleta Mabadiliko,Katika Utendaji,Kujitafutia Kipato na Kusaidia Familia na Jamii Pia.Wengi wao Wamekuwa si WAOGA !!!!!!!!!!

Nisi watenge/Kuwasahau MAMA zetu, Hasa wa KIJIJINI, Pia nao kwa sasa Wanasonga Mbele..Japo bado wanapitia changamoto nyingi sana....Lakini Wengi wao WANAJITAMBUA.

Basi kwa Leo niishie hapa kwani Maneno yanakuwa Meeengi Sana..
Mimi huwa Navutiwa Sana na WANAWAKE Wanaojichanganya na Mambo Tofauti Kama DADA/MWANAMKE HUYU;MWANDALE MWANYEKWA!!!!!!!!!!!!!!

Vipi Mwenzangu dada Huyu anakuvutia? Karibuni kwa Maoni/Ushauri na Tuelimishane kwa Upendo!!!

AFRIKA BARA LETU,TANZANIA NCHI YETU,KISWAHILI LUGHA YETU!!!!!!

   "Swahili NA Waswahili "Wanawake Tusiogope!!!!!!

Wednesday, 6 March 2013

Kuelekea Siku Ya Wanawake Duniani;Leo Tunae Da'Mija[Mwanamke wa Shoka]Alianzia Hapa Ku-Blogu Na Kwa Nini Alijiita Hivi?


DadaMija[Mwanamke wa Shoka] si Jina Geni sana kwa Wanaopenda kufuatilia Mitandao ya Kiswahili..
Kwa Wale Blogger Familia  wanamwita Dada Mkuu msaidizi....kwa Wengine Mama, Ma'Mkubwa, Dadake na Majina meengiii..
Hii kwa Sababu ya Upendo,Ucheshi,Kujitoa,Utundu kiasi,Upole Kiasi na Menginee Bila Kusahau [MAMA AFRIKA].

Dada huyu ni Mjuzi wa Mambo Mengi sana hasa ni MSANII waNguvu.
Lakini Leo tuweke Kando hayo Mengine na Tumuangalie katika KU-BLOGU[BLOGGER]Ni mwana Blogu wa kitambo sana Alianza Tarehe
08 May 2005.Wakati huo alikuwa akiandika na kuanzisha Mada nyingi tena zenye kuvutia sana sana.....Hasa zenye mambo ya  Harakati za Mwanamke/WANAWAKE.

Hakuwa Mvivu kabisa...Siku hizi haweki sana na amekuwa si mwandikaji saaana.. Sijui sababu ya Majukumu ya Umama,Ukubwa,Kachoka,Mazoea au......


Karibu Upitie Maandiko yake/Post zake za Zamani..na Unaweza kutuambia nini kimepungua kwa sasa na nini kimeongezeka..

Zaidi tunahitaji Uhondo Uendelee dada MIJA!!!!!

Kaa Tayari kwa Kumsikiliza siku nyingine nitawawekea  Video yake nini anasema!!!


Unamaoni/Ushauri?Karibuni sana Tuelimishane kwa Upendo!!!



 Post yake ya Kwanza


08 MAY 2005


Ngo...ngo...ngo..hodiii!

Ngo...ngo..ngo... hodiii, jamani wenyewe mpoo?...inaelekea wametoka, ngoja niache ujumbe mlangoni.

Wanablogu,
Nilipita kwenu lakini inaelekea hamkuwepo, nia hasa ilikuwa nikuwapa taarifa kwamba nami nimeingia katika ulimwengu wa blogu. Blogu yangu itajulikana kwa jina la Da'Mija, Da mija atakuwa akizungumzia masuala ya jamii na mabadiliko yake ya kila siku. Atafundisha atakapoona panafaa kufundisha, atajadili pale atakapoona panafaa kujadili, atatoa mawazo pale atakapoona panafaa kutoa mawazo na mengine mengi yatajitokeza kulingana na siku zitakavyokuwa zikienda.

Asanteni.


20 MAY 2005

Huyu ndiye mwanamke wa shoka.

Sifa hizi za mwanamke wa shoka nimezipata katika maandiko matakatifu ya wakristo katika kitabu cha Mithali 31:10-31. Zinasema hivi:-

Mke mwema ni nani awezaye kumwona?
Maana kimachake chapita kima cha marijani.
Moyo wa mumewe humwamini,wala hatakosa kupata mapato.
Humtendea mema wala si mabaya, siku zote za maisha yake.
Hutafuta sufu na kitani,hufanya kazi yake ya mikono kwa moyo.
Afanana na merikebu za biashara,huleta chakula chake kutoka mbali.
Tena huamka kabla haujaisha usiku,
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula, na wajakazi wake sehemu zao.
Huangalia shamba akalinunua, kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu.
Hujifunga nguvu viunoni kama mshipi, hutia mikono yake nguvu.
Huona kama bidhaa yake ina faida, taa yake haizimiki usiku.
Hutia mikono yake katika kusokota, na mikono yake huishika pia.
Huwakunjulia maskini mikono yake, naam huwanyooshea wahitaji mikono yake.
Hawahofii theluji watu wa nyumbani mwake, maana wote wa nyumbani mwake huvikwa nguo nyekundu.
Hujifanyizia mazulia ya urembo, mavazi yake ni kitani safi na urujuani.
Mume wake hujulikana malangoni, aketipo pamoja na wazee wa nchi.
Hufanya nguo za kitani na kuziuza, huwapa wafanyabiashara mishipi.
Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake, anaucheka wakati ujao.
Hufumbua kinywa chake kwa hekima, na sheria ya wema i katika ulimi wake.
Huangalia sana njia za watu wa nyumbani kwake, wala hawali chakula cha uvivu.
Wanawe huondoka na kumwita heri, mumewe naye humsifu na kusema,
Binti za watu wengi wamefanya mema, lakini wewe umewapita wote.
Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili,
Bali mwanamke amchaye Bwana ndiye atakayesifiwa.
Mpe mapato ya mikono yake, na matendo yake yamsifu malangoni.


27 SEPTEMBER 2005

Upendo ni kila kila kitu.

Upendo ni kupenda. Unapopenda kitu hutaki kitu kile kipate madhara ya aina yoyote yale, na pale inapotokea kitu hicho kukumbwa na tatizo basi utafanya juu chini kuhakikisha unatatua tatizo hilo. Mwanao akiumwa utafanya juu chini kuhakikisha anarudia afya yake ya kawaida, unapogombana na Joe Tungaraza wako (mwandani) basi utahakikisha mambo mnayaweka sawa muda si mrefu hii yote ni katika kutaka kuishi kwa raha. Waswahili husema "penye upendo hapaharibiki neno".

Siku zote nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini kuna vita, kwa nini kuna matabaka katika jamii zetu, kwa nini kuna rushwa, kwa nini kuna wivu usiokuwa wa maendeleo katika jamii zetu , kwa nini kuna migogoro isiyoisha.. Nimekaa nimefikiria sana na sasa nimepata jibu moja kwamba ni sababu ya ukosefu wa upendo.

Sisemi kwamba kwenye upendo migogoro haitokei hasilani..hapana migogoro hutokea lakini haidumu kwa muda mrefu na kuwa tatizo sugu. Sehemu yoyote yenye upendo watu hujaliana na kuthaminiana, humpenda mwenzie kama anavyojipenda yeye katu hatataka jirani yake apatwe na baya lolote na kama ikatokea mmoja akakumbwa na tatizo basi husaidiana kulitatua. Na huu ndio upendo wa kweli.

Sasa hivi tulio wengi hatuna upendo kabisaaa, si viongozi wa nchi, si raia si yeyote yule. Watu tumegeuka wabinafsi tunajipenda wenyewe tu, kama mtu mambo yako yakiwa swafi basi uhangaiki na mwingine kujua siku imemuendeaje, labda hakula au anauguliwa wewe hujui maadamu siku yako imepita vizuri yeye atajaza mwenyewe. Tukija kwa viongozi wetu....ma-ma-ma-maaa yaani hao ndio usiseme kabisa, kwa jinsi ninavyojua viongozi ndio kama wazazi wetu, husimama badala yetu sisi kama watoto wao na kuhakikisha hatupati matatizo yoyote kuanzia chakula, mavazi, malazi na mienendo ya tabia zetu. Lakini cha ajabu wazazi wetu hawa wamekosa upendo kabisa kwetu sisi watoto wao, wanakula wenyewe kwanza halafu ndio watoto, watoto wasiposhiba wenyewe hawajali, hawajui watoto wamelalaje au wameamkaje, wameenda shule au hawakwenda au wameacha kabisa hiyo wenyewe hawajui wanachojua ni kujishindilia wenyewe basi. Na mimi hili halinishtui kuona kwa nini watoto nao wanaamua kujiingiza katika makundi yaujambazi na unyakuaji au tabia zozote potofu yote hii ni katika kujaribu kujisaidia maana wazazi wao hawajali. Ndio ni kweli watoto hujifunza kutoka kwa wazazi wao na kama mzazi haonyeshi upendo kwa wanae, watoto watajifunzaje upendo wa kumjali jirani yake?

Tanzania tuna watoto wengi wenye vipaji vya hali ya juu sana, lakini tunashindwa kuwaendeleza watoto wetu kwa vile vipato vyetu viko chini, na hatuwezi kumudu gharama za kuwalipia masomo. Sawa ni kweli lakini bado najiuliza hawa viongozi wetu wenye akaunti zao nchi za ulaya wanashindwa nini kujitolea angalau kila mmoja achukue watoto wawili tu na kuwasomesha? nina hakika hawatapungukiwa na kitu na huo ndio upendo ninaouongelea, hebu fikiria hawa matajiri wote wa Tanzania unaowafahamu wajitolee kusomesha watoto wasio na uwezo wa kifedha katika mashule yao ya akademiki ingekuwaje, nina hakika hawa watoto wasingechezea bahati wangeitwa John visomo. Na ni katika watoto hawa ndio tungepata vijana madhubuti wa taifa la kesho, tofauti na wengi wa watoto wa matajiri waliokulia katika fedha hawana shida ya kujishughulisha sana na masomo kwani fedha ipo na wanafikiri itakuwepo milele.

Haya, mimi sina mengi ya kusema lakini akili yangu inanituma kusema kwamba kama watanzania tutarudisha upendo kati yetu basi mabalaa yooote yanayotufuata fuata yatatafuta njia ya kutokea.

07 DECEMBER 2005

Jamani ninaomba ruksa yenu!

Ndugu wasomaji, Kuna hili suala nyeti sana katika ulimwengu huu, suala la MAHUSIANO YA KIMAPENZI. Suala hili ingawa ni nyeti sana na linalomhusu karibu kila mtu mzima hapa ulimwenguni, lakini ni suala la mwisho kabisa katika kuzungumziwa kwa UWAZI, imekuwa ikioneka kama ni ukosefu wa adabu kulijadili hadharani, Matokeo yake watu tumekuwa tukilivamia tu bila kuchukua tahadhari zozote au bila kujua tunacho kihitaji hasa katika mahusiano hayo na hivyo kusababisha wengi wetu kuishia matatizoni.

Binafsi nimekaa nikaona si vyema kuendelea kulifungia macho suala hili, kuna haja ya kuanza kulizungumza kwa uwazi huku wote kwa pamoja tukishirikiana katika kubadilishana mawazo. Nia hasa ikiwa ni kufunguana akili ili tuweze kuwa makini zaidi wakati tunapoamua kuingia katika mahusiano hayo.

Hivyo basi sina budi kuomba ruksa yenu ili kwa pamoja tukubaliane kuliweka sebuleni jambo ambalo ambalo linaonekana ni la chumbani.

Kuna mambo mengi ya kuyajadili, lakini labda tuanze na hili dogo.

NI VITU GANI MWANAUME HUTEGEMEA KUVIPATA KUTOKA KWA MWANAMKE? NA MWANAMKE KUTOKA KWA MWANAUME?

Wasomaji, ninaamini mjadala huu utatusaidia katika kujitambua zaidi, na kuwa makini wakati tunapotaka kufanya maamuzi.


23 DECEMBER 2005


Viti Maalumu ...

Jamani sijui kama na wenzangu mnaliona hili, binafsi ninaona kuna njama za chini kwa chini zinazofanywa na wanaume kuwazima kabisa wanawake katika harakati za ukombozi. Kumkamilishia mtu mahitaji yake ni kumfanya mtu asipambane, na bila mapambano hakuna ushindi, ushindi utabaki kwa yule anayekupigania. Hii tabia ya kutoa viti maalumu kwa wabunge wanawake inatufanya tusiwajibike ipasavyo na kubakia pale pale. Viti hivi vilitakiwa vipiganiwe ili utakapokipata ujue kweli jinsi ya kukifanyia kazi na kukiwajibikia. Hii tabia ya kupewa-pewa ina mambo mengi ambayo wanawake tunatakiwa tuyajue...Kupewa kwa aina yoyote ile kunaendana na kulipa fadhira, kwa hiyo kupewa huku kwa viti maalum tusikuchukulie juu juu, wabunge hawa wajiandae kupangiwa ya kufanya na kuwekewa mipaka ya kufika. Na kama ukitaka kwenda kinyume na mipaka hiyo basi utakumbushwa jinsi ulivyokipata kiti, kwa hiyo itabidi ukubali yaishe.

Sasa wenzangu hali hii kweli itatufikisha tuendako? ..hili nalo ni lazima tulifanyie kazi. Wabunge wenyewe waliotangazwa hawa hapa chini.

2005-12-23 08:32:50
Na Mwandishi wetu.


Tume ya Taifa ya Uchaguzi, imewatangaza rasmi wanawake 64 wa Vyama vya CCM na CHADEMA kuwa wabunge wa viti maalum.
Wabunge 58 miongoni mwa hao ni wa CCM na wengine sita ni wa CHADEMA.

Hata hivyo taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ilisema tume imeshindwa kutangaza wabunge maalum kupitia chama cha CUF kwa sababu chama hicho hakijawasilisha majina.

Taarifa hiyo iliwataja wabunge wa viti maalum kupitia CCM kuwa ni Bi Anna Magreth Abdallah, Bi Faida Mohamed Bakari, Bi Martha Jachumbulla, Bi Elizabeth Nkunda Batenga, Bi Zainabu Matitu Vulu na Bi Cynthia Hilda Ngoye.

Wengine ni Bi Esther Kabadi Nyawazwa, Bi Mariam Salum Mfaki, Bi Anastazia James Wambura, Bi Gaudensia Mugosi Kabaka, Bi Sijapata Fadhili Nkayamba, Dk. Aisha Omari Kigoda, Bi. Salome Joseph Mbatia na Dk Lucy Sawere Nkya.

Hali kadhalika Bi Joyce Nhamanilo Machimu, Bi Eliata Ndumpe Switi, Bi Lediana Mafuru Mng’ong’o, Bi Diana Nkumbo Chilolo, Dk Batilda Salha Burian, Bi Asha Mshimba Jecha na Bi Fatma Othman Ali.

Katika orodha hiyo ya wabunge wa CCM pia kuna Bi Devota Mkuwa Likokola, Bi Bahati Ali Abeid, Dk Maua Abeid Daftari, Bi Fatma ABdallah Mikidadi, Bi Janet Bina Kahama, Bi Aziza Sleyum Ally, Dk Asha-Rose Migiro, Bi Shamsa Selengia Mwangunga, Bi Margreth Agnes Mkanga, Bi Zuleikha Yunus Haji na Bi Lucy Thomas Mayenga.

Wengine ni Bi Amina Chifupa Mpakanjia, Bi. Margreth Simwanza Sitta, Bi Felista Aloyce Bura, Bi Halima Mohamed Mamuya, Bi. Rosemary Kasimbi Kirigini, Bi Mwanne Ismail Mchemba, Bi Anna Richard Lupembe, Bi Halima Omari Kimbau, Bi Dorah Herial Mushi na Bi Mwantumu Bakari Mahiza.

Wabunge wengi wa CCM wa viti maalum vya wanawake ni Bi. Riziki Lulida Said, Bi Mariam Reuben Kasembe, Bi Mwanakhamis Kassim Said, Bi. Janeth Mourice Massaburi, Bi Benadetha Kasabogo Mushashu, Bi. Maida Hamadi Abdallah, Bi Mwaka Abdulrahman Mbaraka, Bi Kumbwa Makame Mbaraka, Bi Joyce Martin Masunga, Bi Josephine Johnson Ngenzobuke, Bi Kidawa Hamid Salehe, Bi Martha Moses Mlata, Bi Shally Joseph Raymond, Bi Maria Ibeshi Hewa, Bi Pindi Hazara Chana na Bi Stella Martin Manyanya.

Kwa upande wa CHADEMA waliotangazwa kuwa wabunge wa viti maalum vya wanawake ni Bi Grace Sindato Kiwelu, Bi Maulidah Anna Komu, Bi Mhonga Said Ruhwanya, Bi Lucy Fidelis Owenye, Bi Susana Anselm Jerome Lyimo na Bi Halima James Mdee
Kuhusu wabunge wa CUF Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema imechukua hatua za kukiomba chama hicho kuwasilisha majina.

’Baada ya CUF kuwasilisha majina na taratibu zinazotakiwakuzingatiwa Tume itawatangaza wabunge wa viti maalum kupitia chama cha CUF,’ilisema taarifa.




        "Swahili NA Waswahili na Wanawake Wa Shoka
                                     [MiRa]
                       

                                                                              Pamoja daima.



     

                                          

Tuesday, 5 March 2013

Wanawake wa Sasa na Maisha!!!!!!

Waungwana;kuelekea "SIKU YA WANAWAKE DUNIANI" Jee picha hii inakueleza nini..jee Wanawake Wamechoka kuonewa,Wababe,Wajasiri,Waonevu,Wanaweza,Hawana Heshima/Maadili,Maendeleo au?...............

Karibuni sana kwa Maoni/Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo

"Swahili NA Waswahili"Pamoja Sana.

Monday, 4 March 2013

Mswahili wetu Leo anejiita Roseline Sara Mpele;Msome mwenyewe- hujambo zaidi ya hapo leo swahili!!!!!!

Hii email nimetumiwa na huyo mtu anejiita Roseline sara Mpele...

Waungwana Kazi kwenu.Msome hapo chini.


Date: Mon, 4 Mar 2013 09:11:45 +0000
Subject: RE hujambo zaidi ya hapo leo swahili
From: mroseline2011@gmail.com
To:


   
     Ninaelewa kwamba Kiingereza na Kifaransa. Niliomba kila siku kwamba Bwana amemtuma mtu mzuri haki kusaidia katika hali yangu. Asante tena kwa majibu yako shauku.
  
     Mimi kwa muda wanaoishi katika utume Katoliki nchini Ivory Coast kundi mji Abidjan ya yatima kanisa katika nyumba ya watu wazima huduma. Wao kutoa yetu kupata mavazi, chakula na internet bure saa siku kwa ajili ya mtandao maktaba yako. kujua kwamba taarifa yangu kama vile tarehe ya kuzaliwa, anwani, jina, nk:
  
     Kwanza ya jina langu Roseline sara MPEL.
     hai wa pili katika mji wa Abidjan, Ivory Coast, mji mkuu wa kiuchumi
     tatu Mimi ni mwanafunzi kuhitimu, mji wa Abidjan Shule ya Tiba, Chuo Kikuu cha Cocody.
  
     Tangu mimi wamepoteza baba yangu, maisha ilikuwa vigumu sana kwa ajili yangu, lakini hawezi kumudu kuendelea na masomo yao kwa sababu ya maisha mjomba wangu ilikuwa ngumu kwa ajili yangu. Walichukua baba yangu, mali isiyohamishika ya nyumba, na biashara. Wao pia alifanya majaribio kadhaa zisizofanikiwa kuchukua faida ya vijana wangu, kurudisha pesa kutoka kwa baba yangu kushoto benki.
  
     Mimi kuuliza, tafadhali msaada ndani ya madaraka yao kwa kunisaidia kudai akaunti ya baba yangu, lakini pia husaidia mimi kwa mafanikio kukamilisha operesheni hii nyumbani baadaye.
  
     Kwa sasa siwezi kufanya wito umbali mrefu, kama ni ghali sana kwa ajili yangu, kwa sababu mimi si kuzalisha mapato. Hata mimi kuwa na idadi ya simu ambapo unaweza kuwasiliana na mimi na mimi hivyo itaendelea kuwasiliana kupitia barua pepe kwa wewe, kama muda kama kila kitu ni nzuri kusaidia mimi kwenda nyumbani.
  
    Hapa ni baadhi ya habari nahitaji kutoka kwenu kabla tunaweza kusonga mbele.
  
     Kwanza mimi kutuma jina lako, anwani, nk.
     pili namba ya simu na nchi ya makazi na kadhalika.
     theluthi moja ya taaluma yao / wavamizi.
     nne wa umri wake, dhidi ya sanamu
  
     Tangu sisi hawana fedha yangu marehemu baba katika akaunti yako, taarifa zako nipe fursa ya kutoa na kutoa kwa benki ambapo marehemu baba yangu zilizoingia hii pesa kama mpenzi wangu kigeni na mdhamini, ambaye kuhamisha pesa kutoka kwa baba yangu marehemu na kudumisha uwekezaji malengo ya nchi.
     Hatimaye, jaribu kuweka siri manunuzi na lazima si ni pamoja na vyama vya tatu. kati ya mimi na wewe
     Sisi kuelewa kwamba sisi kugeuka usikivu wetu kwa huduma ya 100% kwa ajili ya mafanikio ya shughuli hii. Tafadhali wala kuruhusu kitu chochote na kuvuruga mawazo yako, kwa sababu najua kwamba mawasiliano kati yetu, tutakuwa na uwezo wa kupata manunuzi imekuwa alihitimisha kwa wakati.
  
     Mara nyingine tena, asante. Mimi kusubiri kupata habari zako.
 yako Roseline sara mpele



;Mmmhh Kazi kwelikweli "Swahili NA Waswahili" Pamoja sana.

Sunday, 3 March 2013

Nawatakia J'Pili yenyeUshindi;burudani-Bahati Bukuku na Brown kyando - Unapojaribiwa na Nyingine..!!!!!!!

Wapendwa Muendelee kuwa na J'Pili yenye Baraka,Amani,Huruma  na "UTOAJI"Kwa MUNGU,Yatima, Wajane na kwa Wenyeshida na TABU.....

Na itakuwa,ukiisha kuingia katika nchi akupayo BWANA,MUNGU wako,iwe urithi, na  kuimiliki, na kukaa ndani yake;
Neno la Leo:Kumbukumbu La Torati:26:1-15;
[12]Utakapokwisha kutoa zaka,katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu,ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na  mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;.....................


"Swahili NA Waswahili"Amani na Upendo

Saturday, 2 March 2013

Chaguo La Mswahili Leo-Wenge Musica BCBG - Djodjo Ngonda na Nyingine Nyingii!!!!

Nani alikuambia Afrika si Wabunifu?




Waungwana maneno meengi sinaaa..Mmmhhhh...Kitambo kidogo..walikugusa/Kuwapenda?Jee Bado wapo Juu? Nini /Wapi unakumbuka ukisikiliza Nyimbo hizi?..

Mimi ninawakumbuka watu wengi saana wengine wapo Hai na wengine washatangulia[Kufa].Wengine ninamawasiliano nao Wengine hata sijui wako wapi...Yote ni Maisha.......
Twende Sote sasaaa.......


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.