Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 25 March 2013

Sivuno's Baby Shower na Waswahili wa Holland!!!!!



Sivuno na mamayake Mdogo. Rabia......Muke  ya Nyembo.Ndiye Aliyekuwa msimamizi mkuu[Mama Shughuli]

Shughuli hi ilifanyika Holland[Uholanzi].....
 kama unavyoona Waswahili wa huko na Ushirikiano/Umoja wao kwenye Kufanikisha Jambo/Mambo Yao.....
Basi nisiwe na maneno Meengi...Endelea kuangali Picha!!!!!!!








MC Wa siku hiyo Alikuwa da'Sekky.....kama unavyomuona ......Mwanamke kujiamini!!!!!!






























Watu wakijiachia.......

Rabia Mama wa Shughuli alitunzwa....

 Familia ya Nyembo inawashukuru sana woote  mliofanikisha kwa Hali,Mali, Muda na kuonyesha Upendo na Umoja.
MUNGU azidi kuwabariki...
Tunawapenda Wote na Asanteni Sana.



unaweza kutuma picha na mengineyo kwa Email hii;rasca@hotmail.co.uk

"Swahili NA Waswahili"
Pamoja Sana.



Friday, 22 March 2013

Jikoni Leo;Tupike Pamoja;Recipe of strawberry jam - Mapishi ya (Subtitled in English!!!!!!

This is a video showing how to prepare a Strawberry jam, but you can use any fruit you like: orange, apple, mango, pinneaple, peach..., for East-African users and all the swahili speakers all around the world. It's also subtituled in English. Please, subscribe to our channel if you like it. We are working to offer you more video-recipes in swahili, in our Youtube channel and in our web-sitehttp://www.tupikepamoja.com/


Haya waungwa mambo hayo..tengeneza JAM Mwenyewe!!!!!
Mmmhhhhh Tamu Saaanaaaaa!!!!

Swahili Na Waswahili na Tupike Pamoja

Sunday, 17 March 2013

Natumai Mmekuwa na J'Pili yenye Amani;Burudani- Alipo Roho,Nimemuona BWANA na Nyingine!!!

Nimatumaini yangu J'Pili inaendela vyema.
Tumalizie kwa  Wema,Busara,Hekima na Upole Kiasi...


[1]Mzee usimkemee,bali umwonye kama baba; na Vijana kama ndugu;
[2]Wanawake wazee kama mama;wanawake  vijana kama ndugu wa kike; katika usafi wote.

Neno la Leo:Timotheo:5:1-16


"Swahili NA Waswahili"
MUNGU Awabariki.

Wednesday, 13 March 2013

COVENTRY WOMEN GALA,ALL NATIONS WOMEN GET TOGETHER!!!!!!


COVENTRY WOMEN GALA!!!!
COVENTRY WOMEN GALA



BE PROUD TO BE A WOMAN


We welcome all women from different nations to get together
 and to meet other women
 and discuss,
 inspiring issues and to have fun.

Speakers will be Mariam Kilumanga
 (Chair person of Tanzania Women Association)
 from London.

 Aunty Fay from B'ham,
 Rachel from Coventry 
(Swahili na Waswahili Blog),, 
Zaneli Mary Kay Consult
from Coventry and other speakers.

There will be a Fashion show
 and many other Entertainment.


Different topics such as Women Empowerment,
 Motivation
 and promoting 
Women in business.
       
Don't Miss this wonderful event
 and tell your friends.
you are all welcome!!!!!!!
                                                   
COVENTRY WOMEN GALA
BE PROUD TO BE A WOMAN.

     WOMEN POWER.

Sunday, 10 March 2013

Tumalize J'Pili Vyema na Happy Mothers Day;Burudani-MIRIAM- anaitwa kila mtu na Mt.Cesilia!!!!!


Wapendwa/Waungwana..Leo Tumesheherekea/Tunasheherekea Siku Ya MAMA[MOTHERS DAY]..!!!!Niwatakie kila la kheri na Baraka kina MAMA Wote!!!!!!!

Na Wasiokuwa Mama lakini wanahitaji kuwa MAMA .MUNGU awajaalie   nanyi...Mtaitwa MAMA.

Pia Ahsanteni Sana Kina BABA Kwa  Yote,Kwani Pasipo Nyie Tusinge itwa MAMA!!!!.

Tumalize  J'Pili  hii Vyema na Kumshukuru MUNGU.... [1].BWANA akasema na Musa, akamwambia,[2]Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote,kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli,Wa binadamu na wa Wanyama; ni wangu huyo..

Neno La Leo;KUTOKA:13:1-16.Jambo hilo litakuwa ishara mkononi mwako,na utepe katikati ya macho yako; kwa kuwa BWANA alitutoa Misri, kwa  uwezo wa mkono wake.

"Swahili NA Waswahili"
Mbarikiwe Saaana.

Friday, 8 March 2013

Leo ni Siku Ya Wanawake Duniani;Wanawake Tusiogope!!Leo Tumuangalie da'Mwandale!!!!!!!





Waungwana; Leo ni Kilele cha Siku ya "WANAWAKE DUNIANI" Nami nichukue Nafasi hii kuwatakia Mafanikio,Ubunifu,Uwezo,Maarifa na Baraka katika Utendaji na Maisha  Mema...

WANAWAKE TUSIOGOPE,Kujaribu,Kutenda,Kuamua,Kuuliza/Kujiuliza,Kuchekwa na Kufanikisha Malengo/NdotoZetu.....

Hakuna aliyezaliwa anaweza..wote walijifunza na kulikuwa na Chanzo/Mwanzo mpaka Wale Waliofanikiwa kutimiza Ndoto zao zikawa kweli.....Na kwenye Safari ya Maendeleo kuna Mapito/Changamoto nyingi sana mpaka ufikie Malengo...
Kuna kukatishwa Tamaa,Kuchekwa na Kubezwa.....

Pia ni Vigumu kwa walio wengi kujitambua Yeye anakipaji,Mzuri kwa kufanya nini na Kujikubari au Kukubarika kwa Siku za Mwanzo..Lakini hakuna linaloshindikana mbele za MUNGU..Kama ni Safari uendayo ni yako au si yako Itajulikana Tuu...Hakuna cha Kazi hizi za KIUME au KIKE..
WANAWAKE wa LEO Wanajitahidi Sana Sana  Kujitoa/ Kujihusisha na Mambo mbalimbali ili kufanikisha NDOTO zao na Kuleta Mabadiliko,Katika Utendaji,Kujitafutia Kipato na Kusaidia Familia na Jamii Pia.Wengi wao Wamekuwa si WAOGA !!!!!!!!!!

Nisi watenge/Kuwasahau MAMA zetu, Hasa wa KIJIJINI, Pia nao kwa sasa Wanasonga Mbele..Japo bado wanapitia changamoto nyingi sana....Lakini Wengi wao WANAJITAMBUA.

Basi kwa Leo niishie hapa kwani Maneno yanakuwa Meeengi Sana..
Mimi huwa Navutiwa Sana na WANAWAKE Wanaojichanganya na Mambo Tofauti Kama DADA/MWANAMKE HUYU;MWANDALE MWANYEKWA!!!!!!!!!!!!!!

Vipi Mwenzangu dada Huyu anakuvutia? Karibuni kwa Maoni/Ushauri na Tuelimishane kwa Upendo!!!

AFRIKA BARA LETU,TANZANIA NCHI YETU,KISWAHILI LUGHA YETU!!!!!!

   "Swahili NA Waswahili "Wanawake Tusiogope!!!!!!