Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 17 May 2013

Kuelekea Siku Ya Mtoto wa Afrika;Tujivunie Kuwa Wa-AFRIKA Jee Umejiandaaje?










Waungwana,Wazazi/Walezi,Watoto..Mmejiandaaje na Siku ya Mtoto wa AFRIKA?
ni Siku yetu na kujifunza zaidi mambo Yetu na Watoto Wetu,Jamii Yetu na Wasio Wa Afrika kujua AFRIKA...Kukumbuka/Kuenzi Mema/Mazuri ya Kwetu,Kujivunia Kuwa Wa AFRIKA na Mengine meengi.....
Mimi ninakakitu kidogo cha Kufanya Mwaka Huu na Watoto kama nikipata Muda mzuri na Uwezo kidogo..Nia Yangu nilipenda kufanya  kwa Familia..Yaani  Wazazi/Walezi na Watoto.Tukacheza,Kula na Kukumbukia Enzi zetu na Michezo Yetu na Watoto  wa Leo kujifunza kupitia sisi na Sisi Kujifunza Kupitia ya Kwao/Sasa.

Kama Ungependa Kuniunga mkono/Kuungana nami katika Hili, Usisite Kuwasiliana Nami.
Email;rasca@hotmail.co.uk.Mob;[+44] 0750 44 100 40. kwa sms/WhatsApp.

Pia Karibuni kwa Maoni,Ushauri na Kuelimishana kwa Upendo.

Asanteni na Karibuni Tuungane Pamoja.

                      Pata Burudani;
                      Freedom is coming Tomorro na Video ya SARAFINA...mimi bado naipenda sana Wewe Jee?

Tuesday, 14 May 2013

Waswahili Wetu Leo;Tano Ladies-Wakati Umefika Asiye na Mwana....!!!!!




 Umeshapata Ticket yako? unangoja nini? hazitauzwa malangoni!!!

 Mhhh..Wacheshi,Watanashati..ndiyo hao Tano Ladies.....

   Mikakati zaidi ili wewe upate Raha nasi Karaha...bibi eehhh.

 Wanasema Shughuli Uwanja/Ukumbi..ndiyo huo wakujimwaga zaidi....

Wasikilize wenyewe wasemaje?


Pia unaweza  kuwapitia https://www.facebook.com/pages/TANO-Ladies

Kuona wanapendezaje zaidi nipitie;http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Sunday, 12 May 2013

Muwe Na J'Pili yenye Furaha na Amani;Burudani-Enock Jonas - Wema wa Mungu,Living Water na.....!!!!!




Wapendwa Muwe na J'Pili yenye Furaha,Amani,Upendo,Neema,Utu wema na Upole Kiasi.....

Mwanangu,kama ukiyakubali maneno yangu, Na kuyaweka akiba maagizo yangu [2]Hata ukatega sikio lako kusikia hekima, Ukauelekeza moyo wako upate kufahamu;....

Neno La Leo;Mithali 2:1-11;Busara itakulinda;Ufahamu utakuhifadhi.



"Swahili NA Waswahili"Rehema na kweli zisifarakane nawe.
                           Nawapenda Woote.

Saturday, 11 May 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Mchanganyiko-Waka Waka,[Shakira]Congo Mama[Joe Mafela][Brenda][Lucky Dube] Na...!!!!




Waungwana Chaguo La Mswahili Leo..mambo Mchanganyiko..wewe tuu upate Burudani na kukumbuka wapi na ilikuwa vipi wakati huo unasikiliza/kuangalia Burudani Ya Leo..

Mengi sina nawatakia J'Mosi Njema..Twende sote sasa...Hai Congo mameee,Congo,Congo MAMAAA...Aiiii  SHEBELEZA Njalo MAMA.ekuseni MAMA..............

  "Swahili NA Waswahili" Tunawatakia Kheri na Baraka wote Wanaofunga Ndoa Leo na Watu Wote.



Wednesday, 8 May 2013

Wa-Afrika Na Sherehe Zao Leo;Kenya wedding!!!

Waungwana; Leo tupo Kenya na Shrehe zao za Arusi..nini kimekuvutia/kupenda na kipi kimechukiza/kutokipenda...

Ni Kweli Kwa Afrika Mashariki na Kati Kenya wanaongoza kwa uwandaaji wa Sherehe, Kuanzia Mapambo,Uvaaji,Burudani,picha na Yotemuhimu yahitajiwayo?

  Jee wewe unapicha,Video, za Arusi,Pati za jikoni,Kuagwa,Kipa imara na nyinginezo..za Miaka mitano Nyuma na kuendelea na ungependa kushiriki nasi?
 Unaweza kututumia ili tukumbuke/kumbushane ilikuwaje wakati huo au wewe ulivaaje/ulitokelezeaje na siku yako ilikuwaje.
  
Tuma kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk


Nawe unayefunga Ndoa sasa usisite kututumia...Wewe unayetafuta Mwenza/Mchumba usikate  Tamaa..Mshirikishe MUNGU yupo nawe wala Hajakusahau/kukuacha.

     Swahili-Matukio/Events
          Pamoja Sana.

Sunday, 5 May 2013

Tumalizie J'Pili Kwa Kuombeana/Kutiana Moyo;Burudani-MWAMBA WENYE IMARAA na Nyingine!!!!!

Wapendwa;Tumalizie J'Pili hii kwa kuwaombea, Wagonjwa,Wafiwa, Wenzetu  wa Arusha, Wenye shida na Tabu, TANZANIA,AFRIKA,DUNIA.
MUNGU apate kuwalinda,Kuwaponya,kutatua shida zao, Amani iwe juu yao.
Nanyi mkiwa katika kusali,msi payuke-payuke,kama watu wa mataifa;maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.

Neno La leo;Mathayo Mtakatifu:6:1-21.

"Swahili Na Waswahili" MUNGU atubari Sana.


Saturday, 4 May 2013

Poleni Sana Familia Ya Costa Shirima!!!!!


Ulale kwa Amani Mpendwa wetu COSTA SHIRIMA.Pole  Sana Mke,Watoto,Wazazi,Ndugu,Jamaa na Mrafiki kwa Msiba huu wa Mpendwa wetu  COSTA SHIRIMA.Daima Tutakukumbuka na Kuenzi Mema yote uliyoyatenda.Familia ya ISAAC,Swahili NA Waswahili Blog Tupo Pamoja katika wakati huu Mgumu Kwenu.

Habari kamili,shukrani;http://mrokim.blogspot.co.uk/
MFANYA BIASHARA COSTA SHIRIMA ALIYEDONDOKA  GOROFANI KARIAKOO...



TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.

Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.

Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito mahali alipokuwa.


Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na kishindo hicho.

Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.

Marehemu ameacha Mjane na watoto 5.

Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika. Timu nzima ya Father Kidevu Blog inatoa pole kwa wote waliofikwa na Msiba huo.