Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 12 June 2013

Coventry Women Gala ya Tarehe-08/06/2013[Sehemu ya 2]Mgeni Alikuwa Mama Balozi JOYCE KALLAGE!!!


Waungwana;Tunaendelea na Matukio ya Coventry Women Gala...Mama Balozi Joyce Kallage na Da'Rose Kiondo..Wakifurahi Pamoja..ni Raha tuu..
Da'Agness akikaribisha Wageni na kujitambulisha.

Da'Halima akijitambulisha na kuwahakikishia watu Watashiba..

Hawa walisimamia Chakula na Kukaribisha Wageni.

Da'Stella akijitambulisha ..Yeye alikuwa msimamizi mkuu.

Da'Mija akijitambulisha..Yeye alisimamia Mitindo

Da'Rachel akijitambulisha..Yeye alisimamia Burudani, ndiye aliyepamba Ukumbi na Mc..
DJ Richie Dee..Yeye ndiyo aliyetuburudisha[Muziki]

Mama Balozi ;JOYCE KALLAGE;
Yeye alitupongeza na kutusisitiza kuendelea na masomo,Kusaidia watoto wengine wa kike Nyumbani wanaohitaji Kuendelea na Masomo lakini hawana uwezo.Kuungana  na kujitoa kwa Moyo na kufanya mambo mengi ya maendeleo.Pia alisisitiza sana tusijisahau Kufuata na kuendeleza mambo mema ya Kwetu..Hategemei mtoto wa mswahili asijue kiswahili ni aibu.Kama tumeshaliachia hili watoto wetu hawajui "KISWAHILI" Tufungue darasa la Kiswahili.
Aliongea Meengi.
Asante sana MAMA,Nasi tutafuata Ushauri wako.
[TEAM MAMA BALOZI]

Wanawake Oyeee!!!!Coventry Women Gala Oyeee!!!!!Waswahili Ughaibuni Juu!!!!!Wanawake na Maendeleo!!!!!
Amesema amefurahi kuona tumeweza kurudia tena!!

Hayo yote kwa furaha na unyenyekevu yalitoka kwa da'MARIAM KILUMANGA;Mwenyekiti wa;Tanzania Women's Association[TAWA UK.]
Alisisitiza Tusikate Tamaa na yupo pamoja nasi wakati wowote..Da'Mariam tulikuwa nae wakati uliopita.
Asante Saaaaana.
Dada/Mama;Hilda..Yeye ni Mfanyabiashara wa siku nyimgi,Amepitia changamoto nyingi sana.
Na sasa amesimama vilivyo..Ametufunza mambo mengi sana..alisema yeye si muongeaji sana..Mzuri sana kwenye Vitendo.

Asante Sana kwa Yote mama.


Dada;ROSE KIONDO,Kutoka Ubalozi wetu wa Tanzania hapa UK.

Da'ROSE KIONDO;Yeye alitusisitiza kujihusisha na Ubalozini kwani pale ni kwetu na tutambue hivyo..kwanini tunakuwa waoga na Nyumbani kwetu?Mtu hujivunia chake na kwako..kwa hapa tulipo Pale ndiyo Nyumbani,Wapo pale kwa sababu yetu pia.Aliongea Meengi yenye Faida kwetu.

Asante sana dada.

Alicheza kwanza..

Alitumia vilivyo uwanja...

Mc..mwenyewe hoii..usimchezee kabisa..Mada zake anazitunza vilivyo..

Ni-Aunty/Mama da'Fay..wewe utakavyo penda kumuita yeye hana shida..Yeye alitusisitiza zaidi,kutumia muda vizuri,kujiendeleza kielimu kwani haina mwisho..atakushangaa eti ukisema sina muda kwasababu nina watoto,mume,kazini,kazi za nyumbani..Ukiamua na kama wewe ni msomaji utasoma tuu..ni wewe utakavyojipanga..kila siku utasema muda huna mpaka lini?Tusipoteze muda kwenye mambo yasiyo na manufaa..hasa  tutumie hii MITANDAO vyema na si kutukanana na kuumizana..Tupendane..
Bila kusahau DIET..Na kutafuta mbinu ya kupunguza mwili..Aliongea meengi saana siwezi kumaliza yote hapa..


EPUKA UZEE USIOKUWA WAKO BIBI EEEEEHH.
.

Da'SUSAN

DA'SUSAN yeye aliongelea MADAWA YA KULEVYA..Utayajuaje,Watumiaji,kuepuka,uuzaji,Madhara yake na kuwalinda watoto wetu,Vijana,Jamii na nasisi wenyewe pia..Na mambo mengii yahusianayo na Madawa ya kulevya..

Asante sana.
Umeona hiyo beji niliyo jibandika hapo? Hawa wanatengeneza keki,beji na mengine meengi..ni wadada wanaojituma..ni AHLAM NA KOIYA..Wape Kazi watoto wa Nyumbani..
Hongereni Sana

Da'TINNA..Yeye ni mwimbaji  mzuri sana sauti MUNGU amemjaalia..usisite kumpa kazi. Dada/Mtoto wa Nyumbani.ni burudani tosha sauti yake.

Mama Balozi,Wageni walipata Nafasi  ya kuona/kununua bidhaa mbalimbali kutoka kwa wanawake Wenzao...


Wewe unangoja nini?
Jitoe,Jitambulishe/Tambulisha kazi zako.Ujuzi wako..
Nategemea Kuwaona Wanawake wengi Shughuli ijayo..








Kueleke Siku Ya Mtoto Wa Afrika; Wazo La Leo na Emu-Three!!!!!!



WAZO LA LEO:,Kumbuka ipo siku maalumu, inayotambulikana kama ya siku ya mtoto wa Afrika tarehe 16 June, sijui kama upo makini na siku hii, huenda kwako ni historia tu ya Mauaji ya Soweto…kwani unaishi kwenye kisiwa cha amani, huna shida…una kazi nzuri, gari..nk. Lakini kumbuka kuna hawa watoto wa mitaani, unawakumbuka?

 Je siku ya mtoto kwako inakugusaje?


Je wewe kama mzazi, unahisije ukiwaona watoto wa mitaani, au ndio huko kusema, `hawa watoto wanaomba omba tu, hawaendi shule…’ hawa kwa mateso wanayoyapata hawana tofauti na wale watoto waliouwawa kikatili,…..wewe hutumii, silaha, lakini unatumia njia nyingine, isiyoonekana, ya kutokutimiza wajibu wako kama mzazi.


Kumbuka mateso wanayopata hawa watoto, kwanza kisaikolojia pale wanapoona wenzao wakiwa kwenye sare za shule, au wakipita na magari wakiepelekwa mashuleni.  Lakini pia kuwa mateso ya afya zao, kwani wengine wanaishia majalalani kuokota yale mabaki ya vyakula mliyokula na kusaza. Huyu ni mtoto wako hata kama hukumzaa wewe, kumbukeni kila mtoto ana mzazi, na mzazi wake ni mimi na wewe.

Imeandikwa na emu-three wa Diary Yangu.



Zaidi ingia kwa ndugu wa mimi,Pia kwa Visa vya kusisimua na Mambo meengi;http://miram3.blogspot.co.uk/




Kwa Habari na mambo meengi ya watoto,wazazi/walezi nifuate huku;http://www.watotonajamii.blogspot.co.uk/



Monday, 10 June 2013

Coventry Women Gala ya Tar;08/06/2013-Mgeni;Mama Balozi Joyce Kallage;[Sehemu ya 1]!!!!

Waungwana;CoventryWomen Gala ya safarihii tulikuwa na Mama Balozi JOYCE KALLAGE.
Ameongelea nini Yeye pamoja na Wageni wengine?Usihofu nitakufahamisha..kwa leo Angalia Picha Kwanza. 
[TEAM MAMA BALOZI] 

Mama na Wanamitindo

Mama na Mbunifu wetu da'Mija na da'Halima[Maonyesho ya Mavazi yote ni kazi ya mikono ya Da'Mija!!]
  Mama Balozi Joyce Kallage hayuko nyuma kwenye MITINDO!!!!!




  Nasi tuliungana na wanamitindo kuonyesha Umoja....


  Wanamitindo wakipoziiii..




 

  Da'Rose Kiondo kutoka Ubalozini alikuwa na mengi ya kutuambia..nitakujulisha..


 Wamama wa Coventry na mama Balozi Joyce








  Asante sana mama yetu kwa Ukarimu na kuungana nasi....da'Stella alituwakilisha na kumkabidhi maua kama ishara ya Upendo wetu kwake..














   Mitindo ni kazi ya Mbinifu wetu hapa Coventry..Mwanamke wa Shoka...Da'Mija!!!

 Tulicheza saaaana..

   Itaendelea.....

    "Swahili Na Waswahili" Raha Tupu.

Sunday, 9 June 2013

Nawatakia J'Pili Njema yenye Matumaini;Burudani-Anne Gracious;Nitasimama,Rose Muhando-Woga wako na..!!!!!!!!!


Wapendwa;Muwena J'Pili njema yenye matumaini,baraka,Amani na Furaha.
Hatimaye,ndugu,tuombeeni Neno la BWANA Liendelee,na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;
Neno La Leo;2Wathesalonike:3;1-18;[16]Sasa,BWANA wa Amani mwenyewe na awape amani daima kwa njia zote.BWANA awe pamoja nanyi nyote.
  
"Swahili NA Waswahi"Mbarikiwe Sana.

Friday, 7 June 2013

Wakati Umewadia..Ni J'Mosi Hii;Coventry Women Gala!!!!!


 Umeshapata Ticket Yako? Umejiandaajee?Mwanamke na Wanawake Wenzio Njoo Uungane nao kwa mambo Mazuri..Ukijua Hili wengine wanajua Lile..Jitokeze,Ucheze,Ujifunze na Ufurahi na Wanawake Wengine  kutoka Miji Tofauti!!!!
       Ukumbi utakuwa wazi kuanzia saa 10:00 jioni[4:oopm]Tujitahidi kuwahi Waungwana.....

 Hakikisha umeshapata Tiketi Yako Mapema..

Mgeni Wetu atakuwa;MAMA; JOYCE KALLAGE,MKE WA BALOZI WA TANZANIA,UK.MH.PETER KALLAGE 





                                                                  
                                                              WICCO
                          [Women In Coventry Community Organisation]
                                                                 IS
                                               
                                                        PRESENTING 
                                         COVENTRY WOMEN GALA
                                                    ON: 08/06/2013          
                                                    TIME;18:00-12 MIDNIGHT
                                                                AT
                                         SPENCE COMMUNITY CLUB
                                                  ALBANY ROAD
                                                  EARLS DON 
                                                   CV5 6JR
                                                    COVENTRY 


                                    Women get together
To inspire,Motivate one another,to Advertise and Introduce your Business to Learn and Support each other in......

Accessing education and employment.
Improving marriage and family relationship,
Problems facing teenagers,Teenage sex and Pregnancy.
Awareness on signs of misuse of illegal substances on teenagers.

FASHION SHOW BY OUR COVENTRY DESIGNER MIJA
And many more.
ENTRANCE: £:10,  Including snacks,drinks will be sold at the bar.
For Advance tickets Call; [07500 87 53 94]/ [079 51 58 36 22]/ [079 50 19 87 03.]
DRESS CODE: AFRICAN ATTIRE[KITENGE OR ANY]

AND NOT FORGETTING THE BODY SHAKES!!!!!!!!MUSIC WILL BE THER!!!




KARIBUNI SANA COVENTRY!!!!