Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 27 July 2013

Siku kama yaLeo Tulifunga Ndoa-[Happy Anniversary]!!!!Tuliamua kufanya kazi za jamii.

Bibi Na Bwana tukielekea kuungana na Wapendwa katika kazi jamii/kujitolea



 

Mama Mchungaji na mimi Tukifurahia mambo yanavyokwenda sawa..

Tukisaidiana kuweka mambo vyema






Dada huyu yeye ni mbunifu wa vitu vya Asili,Mikufu,Bangili,Hareni na vinginevyo..
MUNGU amemjalia kazi za mikono yake..basi hutoa kwake/kurudishia yeye pia.




Kulikuwa na Michezo,Zawadi mbalimbali

Hii ndiyo Shughuli kubwa tuliyoiendea..Na pesa zote zilizopatikana..zilipelekwa huko.Wapo waliotoa Pesa,Muda,Vipaji na Mengine meengi ili tuu Jambo tulilokusudia lifanyike..na Lilifanyika kwa uwezo wake MUNGU. Kuna Mengi ya kujifunza/Tumejifunza,Kufundisha watoto wetu.


Mchungaji na Mama Mchungaji Waliwashukuru Watu wote kwa kufanikisha jambo hili


Hahahahahha maneno ya Mchungaji Rachel nimepoziii...


         Wapendwa/Waungwana Bibi na Bwana Isaac;Siku kama ya Leo tuliungana pamoja Kuwa Mwili Mmoja.
Tunamshukuru sana MUNGU kwa kutufikisha hapa.Pasipo yeye sisi si kitu.Azidi kuongoza katika safari yetu.

Shukrani Familia zetu,Ndugu,Jamaa na Marafiki katika Yote.
Shukrani Hebron Church

Kwapicha za watoto na Michezo,Tukutane;http://Watotonajamii.blogspot.com

"Swahili NA Waswahili" Tunawapenda wote.
  

Hadithi hii maana yake nini?



Mmmhh katika pitapita zangu kutafuta hadithi za Watoto wetu j'mosi, Nikakutana nahii.. kila hadithi ina mafunzo/maana ili watoto/watu wajifunze..jee nini maana ya Hadithi hii?

 Usikose kusikiliza/kuangalia Hadithi,Katuni na mengine meengi yahusiyo Watoto na Jamii.







Friday, 26 July 2013

Wimbo Toka Kwa Neema Decoras Milele Nitalisifu Jina Lako!!!!



 Ndugu,

 Salamu katika Jina la Yesu Kristo,

 Ninaitwa Neema
 Decoras. Ni muimbaji wa Nyimbo za Injili toka Dar es Salaam, Tanzania.
 Nimeambatanisha wimbo wa kwanza kutoka katika albam yangu, uitwao Milele Nitalisifu Jina Lako na kuutuma kwako ili uusikilize.


 Mashairi ya wimbo huu ni haya yafuatayo:

Kibwagizo (Chorus)
 Milele, Milele, Milele eeee,
 Milele, Milele, Milele
 eeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
 Aaah,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,

 Beti 1
 Hakika Upendo wako, ooooh
 Nashindwa
 kuupima mimi,
 Ulinipenda mimi, iiiih,
 Ukatoa uhai wako,
Yote hii Bwana, aaaah
Uniepushe na mateso,
Yote hii Bwana, aaaah
Uniepushe na kuzimu,
Ukaja duniani, iiiih,
Ukapata mateso mengi,
Ulijishusha sana, aaaah,
 Ili utukomboe sisi,
 Mimi sijaona, aaaah
 Upendo kama wako tena
 Mimi sijaona, aaaah
Upendo kama wako tena
 Nasema, Milele, Milele Nitalisifu Jina Lako

 Kibwagizo
 Milele, Milele, Milele eeeee,
 Milele, Milele, Milele eeeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
 Milele eeee, Milele, Milele eeeee,
  Aaah,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako Bwana,
 Aaaah, Nitalisifu Jina Lako oooh,

 Beti 2
 Niwapo mashakani, iiiih
 Rafiki hunikimbia,
 Niwapo ni mgonjwa, aaaah
 Watu husema pole sana,
 Lakini hawawezi, iiiih
 Kutatua shida zangu,
 Lakini hawawezi, iiiih
 Kutatua shida zangu,
 Peke yako nakuona,
 aaaah
 Waja kunifariji moyo,
 Peke yako nakuona, aaaah
 Waja kutibu afya yangu,
 Peke yako nakuona, aaaah
 Wanitendea miujiza,
 Ndio maana nasema, aaaah
 Una upendo mwingi sana,
 Ndio maana nasema, aaaah
 Una upendo mwingi sana,

 Kibwagizo
 Milele, Milele, Milele eeeee,
 Milele, Milele, Milele eeeee,

Swahili Na Waswahili;Inakutakia kila lililojema,Baraka katika Yote.Hongera Sana da'Neema Decoras.

Thursday, 25 July 2013

Mtu kwao;Leo Tuangalie Jiji La Dar-es-salaam!!!!!








Waungwana ;ni Kipengele cha "Mtu Kwao" Leo Tupo/Tuangalie/Tutembelee japo kwa Macho Jiji la Dar-es-Salaam[DAR]Bandari ya Salama.

Nini kinakufurahisha katika Jiji hili na Nini kinakukera/chukiza katika Jiji hili?
zaidi ingia;Prinxali

"Swahili NA Waswahili" MTU KWAO.

Sunday, 21 July 2013

Da'Sandra-Neema Atimiza Miaka 15..!!!!!!!
















 Haleluya Nampenda BWANA kwa kuwa anasikiliza Sauti yangu na dua zangu.
kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. Neno La Leo;Zaburi:116:1-2




Wapendwa/Waungwana; Mungu yu mwema Binti Yetu SANDRA-NEEMA. Ametimiza miaka 15.Tunamshukuru sana MUNGU katika yote,Tunamuweka binti huyu mikononi mwako BABA waMBINGUNI. Akawe baraka kwetu na Jamii pia. Asante sana MUNGU kwa zawadi hii maishani kwetu.
 Asante na Mbarikiwe sana Ndugu,Jamaa,Marafiki na watu wote mliokuwa/mnaondelea  kuwa nasi katika Maombi/Sala,Malezi kwa namna moja au Nyingine.
MUNGU akawabariki watoto woote.. pia awajaalie wanaohitaji watoto. Tuna yaweka haya yote mikononi mwa MUNGU.AMEEN!!

Familia ya Isaac inawatakia J'pili yenye Amani,Upendo,Baraka na Furaha.
  
"Swahili Na Waswahili"  Pamoja Daima.




Saturday, 20 July 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Marlaw, anakwambia -Bembeleza,Pii pii!!!!!






Waungwana; Natumaini wote wazima na Mnaendelea vyema na mambo yenu,vipi hali ya hewa huko mlipo?
 Hapa tulipo  leo jua linawaka vizuri...ni Raha na tuweza kunyoosha miguu/kutembea tembea na mambo mengine meengi ya nje yanawezekana.
Mnaofunga ndoa Leo tunawatakia Maisha mema  yenye Furaha,Amani,Upendo,Uvumilivu na mshikamano.Mnaotafuta Wachumba/wenza na mliokuwa kwenye maandalizi Mungu awasimamie.

Chaguo La Mswahili Leo Tumsikilize/angalie Marlaw.. mimi napenda  nyimbo zake hizi vipi wewe?
Maneno Mengi sina wewe pata Burudani na uwe na J'mosi njema.

"Swahili Na Waswahili" Pamoja sana.