Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 4 August 2013

Muwe na J'Pili Yenye Kumpendeza MUNGU;Burudani-Rose Muhando-Tembea baba na MUNGU Unashangaza!!






Wapendwa;Ni matumaini yangu J'pili Inaendelea Vyema..BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba,Watu hawa husema,Huu sio wakati utupasao kuja,huu sio wakati  wa kujenga nyumba ya BWANA.
Neno La Leo;Hagai:1:1-11;[5]Basi sasa,BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.

Muwe na J'Pili ya Kumpendeza MUNGU  na Kupendana wenyewe  Upendo wa Kweli.

"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Sana.



Saturday, 3 August 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Banana Zorro-Mama Yangu,Nzela na nyingine!!!!








Waungwana;"Chaguo La Mswahili Leo"  Banana Zorro.

Mama yangu wewe ni nguzo maishani mwangu Taa imulikayo mbele yangu.....Mmhhhhh...Nikisema nikulipeee itanigharimu Maisha yangu yote!!!!!!!Nikisema nikuzawadie sioni kile unachostahili... ninachoweza sema nakupenda sana mama Nakushuru kwa mema yote uliyotenda kwangu.........

Mengi sina mpenzi/mfuatiliaji.. jee hizi nyimbo zinakugusa/kuzipenda?
Zina Mafunzo/umejifunza kitu?

"Swahili NA Waswahili"

Thursday, 1 August 2013

Tarehe,Mwezi,Siku kama ya Leo Alhamisi;Mimi Rachel-siwa Nilizaliwa-Asante MUNGU!!!!!!













Wapendwa/Waungwana..Tarehe kama ya Leo,Mwezi kama huu,Siku kama hii Alhamisi ..Familia ya Bibi na Bwana Kiwinga,MUNGU aliwajaalia mtoto wa kike mwenye Afya Njema.
Leo ni kumbukumbu ya Siku yangu  ya kuzaliwa, na imejirudia kama ilivyo kwa siku hii ya Alhamisi..

Na Rudisha Shukrani na Utukufu kwa MUNGU BABA MUUMBA.Yeye ananijua zaidi ya wote,Yeye amenifanya hivi nilivyo,Yeye ameniokoa na kunilinda siku zote,Yeye ni Faraja yangu katika maisha yangu,Yeye ni Dereva wangu,Yeye ni Mwalimu wangu,Yeye ni Mwamba wangu,oohh MUNGU wewe ni kila kitu Maishani mwangu,Unatoshaa BABA..Wewe ukisema ndiyo nani atasema siyo?

Shukrani; kwa Wazazi/Walezi kwa yote.Nathamini na kukumbuka meengi sana sana hasa pale ninapo kutana na Mapito/Majaribu,Furaha na Kupiga hatua mpya.Sauti zenu haziishi masikioni Mwangu,Maneno yenu/Wosia,Upendo ,Ukarimu na Faraja zenu..Sina lakusema zaidi ya Asanteni na nawaombea kila iitwapo Leo na kuwapenda Saaaana.

Shukrani; kwa Mume wangu kipenzi kwa yote,wewe ni mwanaume unaye faa kuitwa MUME/BABA,Sijilaumu wala Kujutia kamwe kuungana nawe.MUNGU asante kwa Ubavu huu wangu.

Shukrani;Watoto wangu wote,Dada zangu na Wadogo zangu,Kaka zangu wote,Mawifi,Mashemeji.

Shukrani;Ndugu,Jamaa,Marafiki,  kwenye Safari ya Maisha yangu  nimekuta na Ndugu,Watoto,Dada,Kaka .Ambao si wakuzaliwa nao katika Tumbo Moja/kutokea Ukoo mmoja,Lakini kwangu nawathamini sana sana na Nawapenda mnooo.Ni vigumu kutaja kila mmoja lakini wenyewe manajijua.

Shukrani; Blogger wote,Wapenzi/wafuatiliaji wote wa Swahili na Waswahili,Mitindo Afrika na Nga'mbo,Watoto na Jamii.Pamoja Daima.

Nichukue Fursa hii kukuomba Msamaha/Radhi kutoka moyoni ,Wewe niliyekukosea,kwa makusudi au bila ya kukusudia,Nilikukwaza,kukuletea /kukuingiza majaribuni.
Nami  nichukue Nafasi hii kwa Kuwasamehe wale wote walionikosea/kunikwaza.MUNGU BABA Na atusamehe Sote!!!!!!!

Asanteni kwa mlionitumia ujumbe,Mlionipigia simu,Mlionitumia/letea zawadi,Mlioniombe/endelea kuniombea  Sala/Dua zenu nimezipokea.

Nikisema niendelee hapa sitomaliza mpaka kunakuchaa..kwani kwa umri huu nimepitia Meengi,Ngoja niishie hapa na Mengi usome:1.Wakorintho:12:1-31.[15]Kwa maana mwili si kiungo kimoja,bali ni vingi.

Asanteni sana kwa Kunisoma na MUNGU awabariki Nyote!!!!

Ni mimi;Rachel-siwa.


"Swahili na Waswhili"Pamoja Daima.

Wednesday, 31 July 2013

Wazo La Leo;Kutoka Kwa da'Rose-MWANADAMU MWANADAMU MWANADAMU!!!!!!



Mwanadamu yeyote anayeweza kuongea na wewe gizani, anayekupa ujumbe fulani kwakutumia jina la kivuli,mwanadamu aliyekosa ujasiri wakujidhihirisha kwenye mwanga, nazungumza na yule mwanadamu anayekufahamu,mwanadam ambaye kama ana neno na wewe anauwezo mkubwa wakukutafuta nakukwambia, mwanadamu ambaye anakuona kwenye mwanga yawezekana kila iitwapo leo lakini hakwambii, hana uhuru na mwanga, mwanadamu ambaye hawezi kutumia silaha zake  wakati akuonapo ila ukimpa nafasi ya giza kidogo anaitumia vizuri,mwanadamu asiyekuwa na ujasiri wakukutishia ila atakutishia gizani na ngurumo nyingi zenye vishindo.......mwanadam ambaye anakuthibitishia gizani kuwa yuko kazini na anaamini utaanguka na amekaa mkao wakusubiri uanguke duuuuu!!!!!(sina jina la kumpa ila mara jingine sidhani km anastahili kuitwa mwanadam) kwa maana nyingine niASKARI WA GIZANI....... 

walio wagizani hawaoni yaliyomwangani,na waliomwangani hawaoni yalio gizani....... wa gizani hata ukimwashia taa kwa jinsi yakibinadamu ataona, lakini kwa sababu yeye ni wagizani atatumia nguvu kujibadilisha ndani yake aendelee kuona giza, japo kuwa neema ya mwanga imemfikia (kwa mana nyingine hana neema yakutambua yaliyo  kwenye nuru)....na alie kwenye mwanga hata giza limpitie bado ataona mwanga tuu japokuwa kuna misukosuko,milima,mabondo, na mikasa ya kila namna bado ataona hicho ni kipindi tu.........JARIBU NI KAWAIDA YA MWANADAMU..............)


ninachoweza kusema ni hivi...... acha vita vya rohoni viwe vya rohoni, kuna wakati huyu mwanadamu (PEPO) anaweza kukupush ubinadamu ukuingie kwa namna fulani  USIJARIBU!!!!! Huo ni mlango mkubwa wa yeye kuingia kwa sababu utafanya uwanadamu usaidie kazi za rohoni  NI MWIKO MKUBWA KUSAIDIA KAZI ZA ROHONI............. ACHA KAZI ZA ROHONI ZIFANYIKE KIROHONI(VITA TULIVYONAVYO SI VYA DAMU NA NYAMA BALI..........................),( VAENI SILAHA ZOTE ZA VITA ILI.............) 

Monday, 29 July 2013

Waswahili Na Maisha Yao;Futari Ya Pamoja Marekani[DMV]!!!




Waungwana;"Waswahili na Maisha Yao",Waswahili wa Marekani DMV, wana utaratibu huu wa kukutana pamoja kila J'mosi na J'pili na Kuwa na Futari/Kufuturu pamoja.. Hii inaonyesha kuwa Waswahili hawa hawasahau baadhi ya mambo Mema/Mazuri ya kwao,Ukarimu,Umoja na Mengine meengi.

Hongereni Sana na Muwe na Funga Njema.

Shukrani;Vijimambo Blog.

"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Sunday, 28 July 2013

Natumai J'Pili inaendelea Vyema;Mbarikiwe Wote-Burudani-Shout To The Lord, na nyingine!!


                     Ni kwa Neema ya MUNGU tuu....

Wapendwa Nawatakia J'pili yenye,Rehema,Neema,Fadhili,Shukrani,Hekima,Upendo,Furaha,Baraka,Umoja,Uvumilivu,Tumaini na Upole Kiasi.
Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika,ni heri mwanaume asimguse mwanamke.
Neno La Leo;1.Wakorintho:7:117; [10]Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza;wala hapo si mimi,ila BWANA; mke asiachane na mumewe;[11]Lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena  mume asimwache mkewe..............

"Swahili NA Waswahili" Tunawapenda Wote.








Saturday, 27 July 2013

Siku kama yaLeo Tulifunga Ndoa-[Happy Anniversary]!!!!Tuliamua kufanya kazi za jamii.

Bibi Na Bwana tukielekea kuungana na Wapendwa katika kazi jamii/kujitolea



 

Mama Mchungaji na mimi Tukifurahia mambo yanavyokwenda sawa..

Tukisaidiana kuweka mambo vyema






Dada huyu yeye ni mbunifu wa vitu vya Asili,Mikufu,Bangili,Hareni na vinginevyo..
MUNGU amemjalia kazi za mikono yake..basi hutoa kwake/kurudishia yeye pia.




Kulikuwa na Michezo,Zawadi mbalimbali

Hii ndiyo Shughuli kubwa tuliyoiendea..Na pesa zote zilizopatikana..zilipelekwa huko.Wapo waliotoa Pesa,Muda,Vipaji na Mengine meengi ili tuu Jambo tulilokusudia lifanyike..na Lilifanyika kwa uwezo wake MUNGU. Kuna Mengi ya kujifunza/Tumejifunza,Kufundisha watoto wetu.


Mchungaji na Mama Mchungaji Waliwashukuru Watu wote kwa kufanikisha jambo hili


Hahahahahha maneno ya Mchungaji Rachel nimepoziii...


         Wapendwa/Waungwana Bibi na Bwana Isaac;Siku kama ya Leo tuliungana pamoja Kuwa Mwili Mmoja.
Tunamshukuru sana MUNGU kwa kutufikisha hapa.Pasipo yeye sisi si kitu.Azidi kuongoza katika safari yetu.

Shukrani Familia zetu,Ndugu,Jamaa na Marafiki katika Yote.
Shukrani Hebron Church

Kwapicha za watoto na Michezo,Tukutane;http://Watotonajamii.blogspot.com

"Swahili NA Waswahili" Tunawapenda wote.