Friday, 9 August 2013
Zawadi ya shilingi Milioni 10 kwa taarifa za washukiwa Zanzibar!!!!!
Polisi nchini Zanzibar wameahidi kutoa zawadi ya shilingi milioni 10 za Tanzania kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa watu waliowashambulia wasichana wawili waingereza kwa Tindikali.
Wasichana hao kutoka London, Kirstie Trup na Katie Gee, walirushiwa Tindikali kwenye nyuso zao walipokuwa wanatembea mjini Jumatano Jioni.
Taarifa zinazohusiana
afya
Serikali ya Zianzibar ndio itakayotoa zawadi hiyo.
Polisi wanasema kuwa hizo ni pesa nyingi sana kisiwani Zanzibar.
Kirstie Trup na Katie Gee, wote wenye umri wa miaka 18 kutoka London, walipelekwa hospitalini nchini Tanzania baada ya kushambuliwa Mashariki mwa kisiwa hicho.
Inaaminika kuwa walitoka Tanzania kuelekea Uingereza Alhamisi usiku.
Mama za wasichana hao, Rochelle Trup na Nicky Gee, walielezea kughadhabishwa mno na shambulizi hilo ambalo sababu yake haiwezi kujulikana na ambalo halikuchochewa kivyovyote. Walishambuliwa na wanaume wawili waliokuwa kwenye pikipiki.
Polisi walisema kuwa walirushiwa Acid kwenye nyuso zao, kifuani na kwenye mikono yao walipokuwa wanatembea mjini .
Mwandishi wa BBC anasema kuwa waliowashambulia walitoroka na polisi hawajui kwa nini wanawake hao walilengwa.
Mama za wasichana hao walisema kwenye taarifa yao kuwa walighadhabishwa mno na shambulizi hilo na hawaelewi kwa nini wasichana hao walishambuliwa ili hali walikwenda Zanzibar kwa nia njema.
''Tunashukuru kwa wale wanaotaka kujua kinachoendelea lakini tungeomba vyombo vya habari vituwache kwa sasa hadi tutakapokutana na watoto wetu,'' alisema msemaji wa familia za wasichana hao.
Wasichana hao walikuwa wamekaa Zanzibar kwa muda wa wiki mbili ingawa walitarajiwa kuwa huko kwa wiki tatu, kupitia kwa kampuni ya usafiri ya i-to-i Travel, ambayo ilisema inafanya kila iwezalo kuwarejesha nyumbani Uingereza.
Kari Korhonen, mkurugenzi mwenza wa kampuni ambayo wasichana hao walikuwa wanafanyia kazi, alisema kuwa hali yao si mbaya ikizingatiwa athari za Acid kwa mwili na visa ambavyo vimewahi kushuhudiwa vya kuchomwa kwa Tindikali
Msemaji mwingine aliongeza kuwa wasichana hao walikuwa njiani kuelekea kwa maankuli ya jioni wakati wa shambulizi hilo.
Habari zaidi;http://www.bbc.co.uk/swahili/
Thursday, 8 August 2013
Shusho, Kilahiro kuhudumu Washington DC wiki hii!!!!!
Watumishi wa Mungu Christina Shusho na Upendo Kilahiro, mwishoni mwa wiki hii watahudumu katika jiji la Washington DC na Vitongoji vyake (DMV).
Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries.
Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili
Maadhimisho haya yatafanyika
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.
Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo
Shusho na Kilahiro ambao ni miongoni mwa waimbaji mahiri wa muziki wa Injili Afrika Mashariki, wameshawasili Washington DC tayari kwa huduma hiyo ambayo ni sehemu siku tatu za Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries.
Maadhimisho haya yataanza siku ya Ijumaa na kumalizika Jumapili
Maadhimisho haya yatafanyika
The Way of the Cross Gospel Ministries
(at University United Methodist Church)
3621 Campus Drive
College Park, MD 20740
Hii inakuwa ni mara ya pili kwa watumishi hawa kuhudumu pamoja kanisani hapo katika kipindi cha miaka miwili, ambapo mwaka 2011waliungana na Upendo Nkone kuhudumu katika Mkutano mkubwa wa Injili ulilofanyika kanisani hapo.
Watazame na kuwasikiliza wanavyoelezea siku hizo
Mengi utayapata; http://www.changamotoyetu.blogspot.com
http://www.youtube.com/user/mutwiba
Wednesday, 7 August 2013
Jikoni Leo;da'Miriam Rose Kinunda wa Taste Of Tanzania-Q & A Book, Language and Chapati!!!
Mwenyewe da'Miriam Rose Kinunda [MIROKI] |
Miriam Kinunda is answering popular questions about the book, Why using English instead of Swahili, and Chapati......
Zaidi mfuate huku;http://www.TasteofTanzania.com na A Taste of Tanzania
"Swahili na Waswahili"Pamoja Daima.
Sunday, 4 August 2013
Muwe na J'Pili Yenye Kumpendeza MUNGU;Burudani-Rose Muhando-Tembea baba na MUNGU Unashangaza!!
Wapendwa;Ni matumaini yangu J'pili Inaendelea Vyema..BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba,Watu hawa husema,Huu sio wakati utupasao kuja,huu sio wakati wa kujenga nyumba ya BWANA.
Neno La Leo;Hagai:1:1-11;[5]Basi sasa,BWANA wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu.
Muwe na J'Pili ya Kumpendeza MUNGU na Kupendana wenyewe Upendo wa Kweli.
"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Sana.
Saturday, 3 August 2013
Chaguo La Mswahili Leo;Banana Zorro-Mama Yangu,Nzela na nyingine!!!!
Waungwana;"Chaguo La Mswahili Leo" Banana Zorro.
Mama yangu wewe ni nguzo maishani mwangu Taa imulikayo mbele yangu.....Mmhhhhh...Nikisema nikulipeee itanigharimu Maisha yangu yote!!!!!!!Nikisema nikuzawadie sioni kile unachostahili... ninachoweza sema nakupenda sana mama Nakushuru kwa mema yote uliyotenda kwangu.........
Mengi sina mpenzi/mfuatiliaji.. jee hizi nyimbo zinakugusa/kuzipenda?
Zina Mafunzo/umejifunza kitu?
"Swahili NA Waswahili"
Thursday, 1 August 2013
Tarehe,Mwezi,Siku kama ya Leo Alhamisi;Mimi Rachel-siwa Nilizaliwa-Asante MUNGU!!!!!!
Wapendwa/Waungwana..Tarehe kama ya Leo,Mwezi kama huu,Siku kama hii Alhamisi ..Familia ya Bibi na Bwana Kiwinga,MUNGU aliwajaalia mtoto wa kike mwenye Afya Njema.
Leo ni kumbukumbu ya Siku yangu ya kuzaliwa, na imejirudia kama ilivyo kwa siku hii ya Alhamisi..
Na Rudisha Shukrani na Utukufu kwa MUNGU BABA MUUMBA.Yeye ananijua zaidi ya wote,Yeye amenifanya hivi nilivyo,Yeye ameniokoa na kunilinda siku zote,Yeye ni Faraja yangu katika maisha yangu,Yeye ni Dereva wangu,Yeye ni Mwalimu wangu,Yeye ni Mwamba wangu,oohh MUNGU wewe ni kila kitu Maishani mwangu,Unatoshaa BABA..Wewe ukisema ndiyo nani atasema siyo?
Shukrani; kwa Wazazi/Walezi kwa yote.Nathamini na kukumbuka meengi sana sana hasa pale ninapo kutana na Mapito/Majaribu,Furaha na Kupiga hatua mpya.Sauti zenu haziishi masikioni Mwangu,Maneno yenu/Wosia,Upendo ,Ukarimu na Faraja zenu..Sina lakusema zaidi ya Asanteni na nawaombea kila iitwapo Leo na kuwapenda Saaaana.
Shukrani; kwa Mume wangu kipenzi kwa yote,wewe ni mwanaume unaye faa kuitwa MUME/BABA,Sijilaumu wala Kujutia kamwe kuungana nawe.MUNGU asante kwa Ubavu huu wangu.
Shukrani;Watoto wangu wote,Dada zangu na Wadogo zangu,Kaka zangu wote,Mawifi,Mashemeji.
Shukrani;Ndugu,Jamaa,Marafiki, kwenye Safari ya Maisha yangu nimekuta na Ndugu,Watoto,Dada,Kaka .Ambao si wakuzaliwa nao katika Tumbo Moja/kutokea Ukoo mmoja,Lakini kwangu nawathamini sana sana na Nawapenda mnooo.Ni vigumu kutaja kila mmoja lakini wenyewe manajijua.
Shukrani; Blogger wote,Wapenzi/wafuatiliaji wote wa Swahili na Waswahili,Mitindo Afrika na Nga'mbo,Watoto na Jamii.Pamoja Daima.
Nichukue Fursa hii kukuomba Msamaha/Radhi kutoka moyoni ,Wewe niliyekukosea,kwa makusudi au bila ya kukusudia,Nilikukwaza,kukuletea /kukuingiza majaribuni.
Nami nichukue Nafasi hii kwa Kuwasamehe wale wote walionikosea/kunikwaza.MUNGU BABA Na atusamehe Sote!!!!!!!
Asanteni kwa mlionitumia ujumbe,Mlionipigia simu,Mlionitumia/letea zawadi,Mlioniombe/endelea kuniombea Sala/Dua zenu nimezipokea.
Nikisema niendelee hapa sitomaliza mpaka kunakuchaa..kwani kwa umri huu nimepitia Meengi,Ngoja niishie hapa na Mengi usome:1.Wakorintho:12:1-31.[15]Kwa maana mwili si kiungo kimoja,bali ni vingi.
Asanteni sana kwa Kunisoma na MUNGU awabariki Nyote!!!!
Ni mimi;Rachel-siwa.
"Swahili na Waswhili"Pamoja Daima.
Subscribe to:
Posts (Atom)