Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 20 August 2013

Afya Na Jamii;TATIZO LA MIFUPA AU KUUMWA MIGUU/MAGOTI: OSTEOPOROSIS:


Tatizo hili hujulikana kwa jina la kitaalamu kama Osteoporosis. Ugonjwa huu unatokana na kupunguka kwa protini na madini kwenye mifupa (madini chokaa/calcium). Hali hii hupelekea mifupa kuwa milaini na myepesi ambapo inaweza kuvunjika kirahisi. Kipindi cha utoto hadi kufikia umri wa miaka 30, ni kipindi ambacho mifupa hujijenga zaidi. Baada ya hapo mifupa huwa ina kawaida ya kupoteza madini zaidi.
Tatizo hili linatokea sana kwa watu wazima, hasa zaidi kwaa wanawake ambao wamefikia kipindi cha kukoma hedhi (menopause), kuanzia miaka 50. Ni kipindi ambacho wanawake hupungukiwa na homoni yenye kazi ya kuilinda na kuikinga mifupa. Tatizo hili huwapata wanawake zaidi kwa kuwa wana mifupa midogo na myembamba kuliko wanaume. Miaka mitano (5) hadi aba (7) tangu mwanamke kukoma hedhi hupungukiwa na madini chokaa kwa asilimia ishirini (20%), zaidi ya wanaume. Kuanzia miaka 65 hadi 70 wanawake na wanaume hupoteza madini chokaa kwaasilimia sambamba.
NINI CHA KUFANYA
1. Mazoezi hasa kipindi ambacho umriu mepiga hatua
2. Kwa wale wenye uzito uliozidi, jitahidini kufanya utaratibu wa kupunguza
3. Jitahidi kupata madini chokaa (calcium) kwa wingi (maziwa freshi, maziwa mgando, mboga za majani)
4. Jitahidi kupata Vitamini D (mayai, maziwa, samaki, mboga za majani, pata jua)
VIRUTUBISHI
Kwa ambao tatizo limekuwa kubwa, inawapasa kujitahidi kupata virutubishi ili kuirejeshea mifupa nguvu na uimara, pia kuondokana na maumivu.
Virutubishi vifuatavyo vimewasaidia wengi wenye tatizo hili.
1. Calcium
2. Chitosan
3. Lycopen



KUKOSEKANA KWA UTE KATIKATI YA VIUNGO (JOINTS) - CARTILAGE

Kajiraba fulani ambako hujulikana kwa jina la kitaalamu kama “Cartilage” (katileji) ambako hupatikana katikati ya mifupa. Kuna kitu fulani huwa kinapatikana katikati ya mifupa miwili ya goti la mnyama (ng’ombe, mbuzi) huwa wengi wanapenda kukila kwenye baada ya kuchemshwa au kupikwa. Kama unaijua hii, basi ndio katileji yenyewe.
Katileji inasaidia kuikinga mifupa isiumie.Vilevile inafanya kazi ya kusaidia kuubeba uzito wakati wa kutembea, kuinama, kunyoosha viungo au kukimbia.
Zaidi ya asilimia 85 (85%) ya katileji ni maji, na jinsi umri unavyosonga mbele, maji hayo huwa yana kawaida ya kupungua. Na asilimia 15 niprotini.
Tatizo hili lipo zaidi kwenye sehemu ya magoti. Endapo katileji inakuwa ina tatizo, husababisha maumivu makali hasa unapotaka kusimama au kutembea, vile vile kwenye mabega, au nyonga. Pia inaweza sababisha uvimbe (goti au nyonga au bega kuvimba).
Mtu ambaye katileji yake ina tatizo aidha imelika au kutokuwepo kabisa, anatakiwa kupatiwa vitu au virutubishi ambayo vitasaidia kuirekebisha katileji au kuijaza kwa upya.
Virutubishi vifuatavyo vimesaidia wengi wenye tatizo hili:
1. Shark Cartilage
2. Calcium
3. Chitosan

OFISI ZETU ZIPO karibu na huduma zifuatazo:
1. Ofisiya TRA, au karibu na
2. Afya Dispensary, au karibu na
3. Mjasiriamali kwanza, au karibu na
4. Kanisa la Sabato au karibu na
5. Kanisa la Lutherani au karibu na
6. Uwanja wa mpira wa Mwenge.

Anaye hitaji ufafanuzi zaidi tuwasiliane: 0715 594 564 au 0756 594 564

Au tembelea website yetu www.1000ufahamu.com

Sunday, 18 August 2013

J'Pili ya Leo;Tuendelee Kuwaombea Wenye Shida Na Tabu,Burudani-Upendo Nkone na Abiudi Misholi.!!!!!

Wapendwa;J'Pili hii tuendelee kuwaweka mikononi mwa BWANA wenye Shida na Tabu.
Ikawa tulipokuwa tukienda mahali pale pa kusali,Kijakazi mmoja aliyekuwa na pepo wa uaguzi akatukuta, aliyewapatia bwana zake faida nyingi kwa kuagua.
Neno La Leo;Matendo ya Mitume:16:16-34;






Muendelee kuwa wakati mwema Kila iitwapo Leo.

"Swahili na Waswahili" MUNGU ni mwema.

Saturday, 17 August 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Mary Mary-Shackles na Nyingine!!!



Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo...Mary Mary..[Erica na Tina]Mimi Huwa nawakubari/Nawapenda/Wananibambaaa saaana..Pia huwa nafuatilia sana vipindi vyao kwa Tv.
Je vipi wewe? 
Mengi sina,Nisikuchoshee..Pata Burudani Kitu Roho napenda......









"Swahili na Waswahili" Pamoja Daima.

Sunday, 11 August 2013

Natumaini J'Pili inaendelea Vyema;Burudani-Hakuna Mungu kama Wewe na Nyingine!!!!!

Natumaini J'Pili Inaendele Vyema..
Ni neno jema kumshukuru BWANA, Na kuliimbia jina lako,Ee Uliye juu.

Neno La Leo:Zaburi:92:1-5;Ee BWANA jinsi yalivyo makuu matendo yako! Mawazo yako ni mafumbo makubwa.
Wapendwa/Waungwana; Nawatakia kila lililo Jema, Baraka,Amani na Furaha.






"Swahili NA Waswahili" Mbarikiwe Wote.

Saturday, 10 August 2013

Watoto Na Malezi; Watoto wa zamani,Mnakumbuka Kipindi cha MAMA na MWANA?



Watoto wa Zamani Mpo? Mnakumbuka  MAMA na MWANA/WATOTO WETU/CHEI CHEIIII..Mhh mimi ni mmoja wa waliokuwa wapenzi  wa Kipindi cha Watoto RTD...
Enzi ya Shangazi/Mama, Debora Mwenda,Sango Kipozi,Eda Sanga na Wengine....

Mhhh Chei Chei Shangaziii..Uje tena Shangazii...


Sehemu ya Kwanza ya Hadithi ya Binti Mfalme;



Sehemu ya Pili



Kujua Mengi Kuhusiana na Watoto Nifuate Huku;http://Watotonajamii.blogspot.com Huku Utakutana na Mambo ya Watoto,Wazazi/Walezi.Hapa tutaendeleza Watoto Na Malezi kwani Swahili Na Waswahili ni Mama Leo..Lakini nimetenganisha Mambo Kidoogo..huko ndiyo Penyewe kwa Mambo ya Watoto na Jamii.

Pia kwa Mambo ya Mitindo Nifuate Huku;http://www.mitindoafrica-abroad.blogspot... Kwa Undani Zaidi..
Panapo Majaaliwa/Kwa Mapenzi ya MUNGU ipo siku yote yatakuwa kwenye Nyumba moja.
Yote Haya yapo Ndani ya SWAHILI NA WASWAHILI NA WAPENDAO YA WASWAHILI NA YASIYO YA WASWAHILI YANAYO FAA KUJUZWA WASWAHILI. 

Pamoja Daima.

Friday, 9 August 2013

Tamasha kubwa la muziki wa Injili kufanyika Washington DC kesho!!!!


 Waimbaji wanaofanya vema kwenye muziki wa Injili Afrika Mashariki, Upendo Kilahiro na Christina Shusho, watatumbuiza katika Tamasha kubwa la Injili litakalofanyika Jumamosi hii jijini Washington DC

 Kama walivyoongea kwenye VIDEO HII, waimbaji hao wamekamilisha maandalizi ya tamasha hilo ambalo pia litashirikisha waimbaji wenyeji wa hapa Marekani.
 

 Tamasha hilo kubwa lililo sehemu ya Maadhimisho ya miaka mitano ya kanisa la The Way of The Cross Gospel Ministries litafanyika siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi kamili mpaka saa tatu usiku (6:00pm - 9:00pm) na kiingilio kwenye tamasha hilo kitakuwa ni dola kumi ($10) kwa watu wazima, bure kwa watoto.

 Anwani ambapo litapofanyika tamasha hilo ni

 The Way of the Cross Gospel Ministries 

 (at University United Methodist Church) 

 3621 Campus Drive 

 College Park, MD 20740 

 Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na

 Mch. Ferdnand Shideko +1 240 476 6718 ama

 Ms Flora Mnkande +1 240 217 6335

 Waimbaji hawa wote watatumbuiza nyimbo zao za zamani na mpya na wanawaalika watu wote kujumuika nao na waimbaji wenyeji kuweza kupata BARAKA kwa njia hii ya uimbaji

   

   
Zaidi utayapata; http://www.changamotoyetu.blogspot.com
 http://www.youtube.com/user/mutwiba