Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 1 October 2013

Ya Kale Ni Dhahabu-Zilipendwa;Arusi!!!!!!

Binti P.. akienda kufunga Ndoa..
Bibi Na Bwana...
Watoto na Show..

Waungwana ya Kale ni Dhahabu..

Unaweza kutambua hii ni miaka gani?
Nini kimekuvutia/Bado Unakipenda na Nini umekumbuka kupitia Picha hizi?
Una Maoni/Ushauri gani kwa Arusi/Wanaofunga Ndoa sasa?

Kama una picha zako za zamani na unapenda kushiriki nasi,Tuma kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk.

"Swahili NA Waswahili" Tunawatakia kila la kheri Wanandoa katika Maisha yenu Yoote.

Pamoja Daima.

Sunday, 29 September 2013

Natumaini J'Pili ni Njema kwenu;Burudani,Bahati Bukuku-Barthimayo,Waraka wa Amani...!!

Wapendwa Muendelee kuwa na  J'Pili njema, Yenye Kutafakari,Amani,Upendo na Kujitolea kwa wenye Kuhitaji.

Kwa maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.....

Neno La Leo;Mathayo Mtakatifu:20:1-16....Vivyo hivyo wa  mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.





"Swahili NA Waswahili" MUNGU awabariki Sana.

Saturday, 28 September 2013

Chaguo La Mswahili Leo;-Baka Gdine!!!!!

Waungwana;Chaguo La Mswahili Leo si Wengine..Wanaitwa/kujiita.

Orchéstre Baka Gbin

Mmmmmhhh...hapa ni mwendo wa kusakata mpaka chiniii.. si maneno..
Iyeeeeehh mama eehh Iyeehhhh mama eehhh.........!!!!

mimi nimewapenda sana.. vipi wewe?
Endelea na Burudani.....

.






"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana

Thursday, 26 September 2013

Wanawake Na Mitindo Ya Nywele;Box Braids!!!



Waungwana;Wanawake Na Mitindo, Hii mitindo sasa inaenda na Inarudi..Lakini haiishi hamu,Zaidi Style za Ubanaji zinaongezeka..haya ukibinua kushoto/kulia Juu/Chini inakwenda tuu na inapendeza sana.

Unakumbuka mitindo/misuko hii ya Rasta ilianza lini?
Jee wewe unaipenda? na jee inampendeza kila mtu au inaendena na sura ya mtu.. Nyembaba/Ndefu.Pana/Mviringo?
Vipi hii Mitindo inaendena na Umri?

Mwanamke Kupendeza na Kuiga sawa/kupo, Lakini tusivuke Mipaka.
Karibuni Wote Kwa Maoni/Mawazo, Ushauri,Tuelimishane kwa Upendo.

Kwa Mitindo Zaidi ingia;http://www.mitindoafrica-abroad.blogspot.com/

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana

Wednesday, 25 September 2013

Sunday, 22 September 2013

Muendelee na J'Pili hii vyema; Burudani-chidumule, mimi FurahaYangu!!!

Wapendwa muendelee kuwa na J'Pili njema, Amani na Upendo.

Pia tuwaweke wenzetu wa KENYA mikononi mwa MUNGU katika kipindi hiki kigumu kwao.


"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday, 21 September 2013

TAARIFA YA MSIBA WA MAREHEMU LILIAN NABURI - TANGA

R.I.P LILIAN NABURI Bwana Ametoa na bwana ametwaa jinalake libarikiwe     Tuungane jumatatu kumsindikiza mpendwa wetu


Marehemu Lilian Naburi
Familia ya Mzee Geofrey Naburi wa Nguvumali Tanga inatangaza kifo cha Binti yao Mpendwa Lilian Naburi kilichotokea Arusha Jumatano ya tarehe 18/09/2013. Mazishi yanategemewa kufanyika Jijini Tanga siku ya Jumatatu ya tarehe 23/09/2013 katika makaburi ya Bombo.
Kwa mawasiliano zaidi unaweza ukawasiliana na kaka wa marehemu
Ndugu Ben Naburi kwa namba ya simu +255 713 563003
Blog hii inaungana na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Bwana alitoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe