Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 15 October 2013

Mahojiano ya Jamii Production na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Dr Charles Kimei‏

Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) akizungumza na Jamii Production  ndani ya ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico uliopo Jijini Washington DC

Jumatano ya Oktoba 9, 2013, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRBD Dr Charles Kimei akiambatana na Mkurugenzi wa Masoko wa (CRDB) Tully Mwambapa, Bw. Mkurugenzi wa Hazina (CRDB) Alex Ngusaru na Msaidizi wa Dk.Kimei , Kenneth Kasigila walikuwa jijini Washington DC (pamoja na mambo mengine) kueleza mipango ambayo CRDB inayo katika kuboresha huduma za akaunti ya Tanzanite pamoja na kutambulisha huduma mpya ya JIJENGE.

Jamii Production ilipata fursa ya kuhojiana na Dr Kimei ambaye amefafanua mengi kuhusu huduma hizo.

KARIBU UUNGANE NASI





Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei na akipata picha na mpiga picha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry baada ya mahojiano.

--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA@ CAPITAL RADIO. Kutekwa kwa Waziri Mkuu wa Libya na kukamatwa kwa Al-Libi‏



Kutoka Tripoli nchini Libya....Watu wenye silaha mapema Alhamis walimteka na baadae kumuachia huru Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ali Zeidan juu ya kile ambacho waasi wamesema ni kuonyeshwa kukerwa na matatizo ya RUSHWA NA USALAMA katika nchi hiyo.

Hili linaonekana kutekelezwa kufuatia kukamatwa kwa mshukiwa wa kundi la kigaidi la AlQaeda Nazih Abdul-Hamed al-Ruqai, ambaye pia anafahamika kama Abu Anas al-Libi aliyekamatwa jumamosi iliyopita nchini Libya na makomandoo wa Marekani

Huu ni muendelezo wa taarifa tofauti na za kuchanganya tangu kukamatwa kwa Al-Libi

Ifuatayo ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es
Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Oktoba 12, 2013


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"

www.jamiiproduction.blogspot.com
http://www.youtube.com/user/mutwiba/videos
https://soundcloud.com/jamii-production

Sunday, 13 October 2013

Nawatakia J'Pili Njema;Bethany Children's choir from Tanzania sing 'Mambo sawa sawa' na Nyingine!!

Wapendwa Nawatakia J'Pili Njema yenye, Imani,Ulinzi,Tumaini,Furaha na Tusisahau kusaidia wenye Kuhitaji....
Hatimaye,ndugu,tuombeeni neno la BWANA liendelee,na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu;
Neno La Leo;2Wathesalonike:3:1-18;Neema ya BWANA wetu YESU Kristo na iwe pamoja nanyi nyote.

Burudani ya Leo Kutoka kwa Bethany Children's Choir Tanzania; Kujua Mengi au kwa Msaada zaidi ili uwafikie Watoto Hawa Ingia Hapa;http://www.bethanyfamily.net






"Swahili Na Waswahili" MUNGU awabariki Sana.

Saturday, 12 October 2013

Chaguo La Mswahili Leo;Sam Mangwana na Franco!!!!


Mmmmmhhh mambo ya kitambo kidogo...
Endelea kupata Burudani..
.



"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Thursday, 10 October 2013

Mtu Kwao; kaka Tonny Samaka-Ana Haya ya Kusema!!!!


   Maneno ya  kaka;Tonny Samaka

Boom fc,ashanti,sharif star,forever fc,god lion,pentagon,barcelona,mkunguni fc,fildaus fc,dizonga fc,santa maria nk,popote ulipowahi kusikia kati ya hizo timu zinacheza iwe tmk,kino nk,ujue watoto wa ilala WANAWAKILISHA NA USHINDI NJE NA NDANI,i love ILALA bana!team#ILALA.

Wewe unasemaje?

"Swahili Na Waswahili" Pamoja sana.


Wednesday, 9 October 2013

Sunday, 6 October 2013

Nimatumaini Yangu J'Pili inaendelea Vyema;Burudani-Ruach Team-Godwin Ombeni,Mwamba wenye Imara na...!!!!!

Wapendwa muendeele na J'Pili  hii Vjema,Muwe na Imani,Matumaini,Furaha na Ushindi.....

[31]Akawatolea mfano mwingine,akisema,Uflame wa Mbinguni umefanana na Punje  ya hadali, aliyoitwaa mtu akaipanda katika shamba lake;
[32]Nayo ni ndogo kuliko mbegu zote;lakini ikiisha kumea,huwa  kubwa kuliko mboga zote, ikawa mti,hata nyuni wa angani huja na kukaa katika matawi yake.
Neno La Leo;Mathayo Mtakatifu:13:24-35.






"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.