Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi kusini mwa jangwa la sahara.
Kama
tunavyojua, ni lugha ya taifa kwa nchi za Tanzania naKenya, na pia
yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi,
Rwanda, Uganda na visiwa vya Comoro.
Ikizungumzwa na watu
wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee
ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na
inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani
Na matumizi
yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi
kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na
biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.
Kiswahili sasa
kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia
inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.
Kiswahili
ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na
hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya
waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha
darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.
Na leo,
wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV
(Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha
Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami
katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.
KARIBU UUNGANE NASI