Mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA, Georgina Lema
Moja ya sababu zilizotusukuma kujadili masuala kuhusu FAMILIA ZA KAMBO ni takwimu zilizopo hivi sasa kuhusu familia hizi.Kwa mujibu wa mtandao wa www.blendedandbonded.com, hapa Marekani
• 41% ya ndoa za kwanza huishia kwenye talaka
• 60% ya ndoa za pili huishia kwenye talaka
• 73% ya ndoa za tatu huishia kwenye talaka
• 45% ya wanawake na 50% ya wanaume wataoa tena ndani ya miaka mitano ijayo
• 50% ya ndoa za marudio huhusisha watoto wa mahusiano yaliyopita walio chini ya miaka 18
•Ndoa 2100 huanzishwa kila siku nchini Marekani
• 42% ya watu wazima wana uhusiano wa kambo. Hii inajumuisha mzazi wa kambo / mtoto wa kambo ama ndugu wa kambo
Kwa idadi ya Marekani, takwimu hizi zinamaanisha kuwa familia za kufikia zinahusisha watu wazima wapatao milioni 95.5
•Kuna baba wa kambo milioni 16.5
•Kuna Mama wa kambo milioni 14.
•Wataalamu
wa mahusiano wanasema kuwa ndoa za kufikia ndio zitakuwa ndoa zenye
umaarufu na nyingi zaidi nchini Marekani na kuwa, kutokana na kukosekana
kwa taarifa sahihi kuhusu familia za kufikia, familia hizi mara nyingi
zimejikuta kwenye migogoro na mafarakano.
Nasi tuko hapa kujaribu kuepusha hilo kwa kushirikiana nanyi katika kile tunachoweza kuelimisha kudumisha ndoa hizo.
Ungana nasi katika sehemu hii ya mwisho ya MADA hii.
--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"