Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 22 February 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?‏


Photo: Mobile88.com

Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya
WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu
bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi
kifupi tu.

Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano
ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni
19 kununua WhatsApp.

Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Monday, 17 February 2014

Tano Ladies Na Maadhimisho ya Siku Ya Wanawake Duniani;Tarehe 8.03.2014!!!!!!

Wakiwa na Mhe.Balozi ;Liberata Mulamula
Wakiwa na Mhe.January Makamba
Wenyewe Wanawake wa Shoka Tano Ladies!!!!

"Swahili Na Swahili"Tukiwa na Nia Moja,Pamoja Tunaweza.

Thursday, 13 February 2014

Jikoni Leo; Tupo Sokoni-Zanzibar Market!!!!!









Waungwana; "Jikoni Leo" tupo sokoni.
Nini kimekufurahisha na nini kimekuchukiza katika masoko haya?
Kwa walio mbali na Nyumbani nini kimekukumbusha na unakikosa hapo ulipo?

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday, 12 February 2014

Wanawake Na Urembo-Nywele,Makeup!!!!



Waungwana;Wanawake na Urembo, jee wewe kwako UREMBO ni nini?
Kila Mwanamke  anacho anachokipenda kukifanya,kuboresha UREMBO wake,Wapo wanaopenda kunyoa Nyusi,Kupaka Wanja,Rangi za mdomo,Kusuka,Kuweka Nywele Bandia,Kucha na Mengine meengi.Jee wewe Wapenda nini?

kwapicha zaidi ingia;http://www.mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/


"Swahili NA Waswahili" Pamoja Daima.

Monday, 10 February 2014

[AUDIO]: Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...BAJETI KATIKA FAMILIA‏


Bwn Solomon, Sunday Shomari na Herriet Shangirai wakijadili jambo ndani ya studio za Jamii Production. Washington DC
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi hiki, tumejadili suala la BAJETI KATIKA FAMILIA.
umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.

Wachangiaji studio walikuwa ni Herriet Shangirai, Sunday Shomari, Solomon na Mubelwa Bandio
KARIBU UUNGANE NASI

Sunday, 9 February 2014

Natumaini mnaendelea/Mmekuwa na J'Pili Njema;Burudani-Here I am to worship,Open the Eyes of my Heart!!!!!

Muendelee na J'Pili yenye Amani,Furaha na Neema.
Kwa kila jambo kuna majira yake, 
Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Neno La Leo;MHUBIRI:3:1-22.

[15]Yale yaliyoko yamekuwako;na hayo yatakayokuwako yameshakuwako;naye MUNGU huyatafuta tena mambo yale yaliyopita...........




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday, 8 February 2014

Rekodi katika michuano ya Olimpiki Sochi‏

Michuano ya 22 ya Olimpiki ya majira ya baridi imeanza jana huko Sochi nchini Russia.
Mabadiliko mengi yametokea katika miaka sita na nusu ya maandalizi yake
Na wakati mamilioni ya watu duniani wakiwa wameelekeza macho na masikio yako huko, kujua nani atashinda nini na nani atavunja rekodi gani, tayari rekodi kubwa zaidi katika michuano hiyo imevunjwa hata kabla ya kuanza kwake.
Na tuipitie safari safari ya maandalizi ya michuano hii mpaka ilipofikia na baadhi ya vikwazo ilivyopambana navyo

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).


Hii ilikuwa ripoti ya Februari 8, 2014


--
*JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"