Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 15 March 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Mfungwa aliyekuwa akisubiria KIFO aachiwa huru‏


Picha iliyopigwa na mwanasheria wake, ikimuonyesha Bwn Ford, siku ya kwanza kama mtu huru baada ya miaka 30 jela kwa kosa ambalo hakufanya. Photo Credits: theatlantic.com
Wiki hii, mmoja wa wafungwa nchini Marekani, ambaye alikuwa kwenye orodha ya wanaosubiri kunyongwa kutokana na kuhukumiwa kifo kwa mauaji  aliyotuhumiwa kufanya mwaka 1984 aliachiwa huru baada ya Jaji kukubali kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa ni yeye aliyeshiriki mauaji hayo.

Sasa, mfungwa huyu atalipwa dola 25,000 kwa kila mwaka aliotumikia kifungo hicho, lakini, kwa mujibu wa sheria ya Louisiana, kiwango cha juu anachoweza kulipwa ni dola 250,000

Ina maana, atalipwa kwa miaka 10 tu kati ya 30 aliyokaa gerezani

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Tuesday, 11 March 2014

[AUDIO]: Kipindi cha FAMILIA. Siku ya wanawake duniani‏

Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Kipindi hiki kilirushwa moja kwa moja (live) Jumamosi Machi 8, 2014

Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulijikita zaidi katika SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ambapo wageni Mary Ndaro akiwa Wichita Kansas na Mch. Tumaini Mwanyonga  walijadili kwa mapana suala hili.

Wamegusa mengi mema ambayo ni muhimu kuyasikiliza.





Photo Credits: happyholidays2014.com

Monday, 10 March 2014

Jikoni Leo; Njoo Tupike Na Chef Kile-Kuchoma Ndizi Mzuzu kwa Oven na Mengine!!!!!

Waungwana;"Jikoni Leo" Tupo na Njoo Tupike Na Chef Kile.

Vijiwe/Vibaraza vya Mapishi kwa sasa Vinakuwa Kwa Kaaasi.
Sasa kama wewe ni Mpishi/Unapenda Kujifunza ,Mpenzi wa mapishi mbalimbali Wakati ndiyo huu.
Nisiwachoshe na Maneno Meengi...
Twende Sote sasa;"Jikoni Leo" Na....





Jee kuna faida/umejifunza kitu hapa?

Mimi hii ya Ndizi  Mzuzu kwa Oveni nimeondoka nayo/Nimejifunza!!!!

Zaidi ingia;youtube.Njoo Tupike /http://www.njootupike.com/

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Sunday, 9 March 2014

JumaPili hii Tusifu Na Kuabudu;Burudani-Mr&Mrs Goodluck Sandy-Alipo BWANA,Viumbe Vyote,Hakuna mwingine Tena,MUNGU U Mwema,Hakuna wa Kufanana na YESU!!!!!

Hatuja chelewa saana,Wapendwa Waungwana..WANAWAKE JUU!!



Wapendwa; Nawatakia JumaPili Njema, Yenye Kusifu na Kuabudu,Imani,Furaha,Amani,Tumaini,Subira,Uvumilivu,Hekima,Busara na UPENDO!!!!


Wanafunzi waliposikia,walishangaa mno,wakisema,Ninani basi awezaye kuokoka?



Neno La Leo;Mathayo Mtakatifu:19:23-30


YESU akawakazia macho,akawaambia,kwa wanadamu hilo haliwezekani; bali kwa MUNGU yote yanawezekana.


Lakini wengi walio wa  kwanza watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.
"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Friday, 7 March 2014

International Women's Day 2014 - UDSM female staff.

Wanawake tunaweza.. Mamaaa GerryHans nawatakia wanawake woote kila la kheri ktk kusherehekea siku ya wanawake duniani. Kina Mama oyeeeee...

Picha na Mpiga picha Wetu;Phoibe Penza- Mshana[Mwanapenza]


Kama unapicha,Ujumbe wowote,Usisite kututumia kwa Email;rasca@hotmail.co.uk

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.




Sunday, 2 March 2014

Nimatumaini Yangu JumaPili hii Inaendelea Vyema na Yenye Furaha;Burudani Kutoka kwa-Muyiwa!!!!!

Na muendelee na J'Pili yenye Amani,Furaha,Imani na Upendo.

Mitume wakamwambia BWANA tuongezee Imani.

Neno La Leo;Luka Mtakatifu:17:1-10.

Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya  yote mliyoagizwa,semeni,Sisi tu watumwa wasio na faida;Tumefanya  tu yaliyotupasa kufanya.




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Wote.