Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Saturday, 22 March 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90: Kupotea kwa Air Malaysia na takwimu za usalama wa anga duniani‏

Ndege aina ya Boeing 777 ya Malaysia Airlines ikiruka kutoka Roissy-Charles de Gaulle Airport nchini Ufaransa mwaka 2011.
Photo Credits: PressTv
Wakati harakati za
kutafuta ndege ya Shirika la ndege la Malaysia iliyopotea zikizidi kushika kasi
na kuvunja rekodi ya kushirikisha mataifa mengi duniani, baadhi ya takwimu
kuhusu hali ya usalama wa safari za anga duniani zimezidi kuibuka na kufungua
macho ya wengi waliokuwa wakiamini kuwa tukio hili ni la kwanza na / ama
miongoni mwa machache kupata kutokea duniani.


Mtandao wa Usalama wa safari za Anga ama Aviation Safety Network
ilitoa orodha ya ndege zilizopotea tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya
dunia.



Kwa mujibu wa takwimu hizo, ndege 88 zimepotea
tangu mwaka 1948, hivyo kufanya wastani wa ndege zinazopotea na kutopatikana
wala miili ya abiria kuwa 1.33 kwa mwaka.


Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90
ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es
Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30
AM).

Tuesday, 18 March 2014

IskaJojo Studios; Ilimuhoji Miriam Kinunda Author of Taste of Tanzania Cookbook‏


IskaJojo Studios; Ilimuhoji "Miriam Kinunda" Mwandishi wa kitabu cha mapishi a Taste of Tanzania: Modern Swahili Recipes for the West.
Akieleza historia yake fupi ya kazi na mapishi na mengineo yanayoweza mnufaisha yoyote anayetaka kuandika kitabu na kufanikisha.



Miriam Kinunda - Taste of Tanzania  Na  IskaJoJo Studios 


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Sana.

Monday, 17 March 2014

Boniface Makulilo azungumzia maisha katika jeshi la Marekani kwenye kipindi cha NJE-NDANI‏

Boniface Makulilo alipokuwa katika Jeshi la Maji la Marekani (Navy)
Mtanzania Boniface Makulilo ametumikia Jeshi la Maji (NAVY) hapa
Marekani kwa miaka miwili na sasa ni mwanajeshi mstaafu (Veteran)

Amezungumza
na Mubelwa Bandio wa Jamii Production kuhusu maisha yake ya jeshini na
namna ambavyo watu toka nje ya nchi wanaweza kunufaika na mafao yaliyopo
jeshini.

Ameeleza mengi ya manufaa ambayo wengi hatuyajui kuhusu maisha katika jeshi hilo.

Karibu uungane nasi

NJE-NDANI ni kipindi kutoka Jamii Production Washington DC kinachokujia moja kwa moja (LIVE) kila Jumamosi kuanzia saa 6 mpaka 8 mchana (saa za Marekani mashariki) ambacho kinaleta Habari na Taarifa kuhusu yale yanayotokea na kuwagusa waAfrika walio NJE na NDANI ya Afrika.

Sunday, 16 March 2014

Nawatakia JumaPili Njema na Furaha;Burudani kutoka kwa Beatrice Kitauli-YESU Unipendaye[TENZI],Imbombo Inunu mwa JESU na Nyingine!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu Jumapili inaendelea vyema..

Heri kila mtu amchaye BWANA,Aendaye katika njia yake.


Neno La Leo;Zaburi:128:1-6

Tazama,atabarikiwa hivyo,yule amchaye BWANA......





"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Saturday, 15 March 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Mfungwa aliyekuwa akisubiria KIFO aachiwa huru‏


Picha iliyopigwa na mwanasheria wake, ikimuonyesha Bwn Ford, siku ya kwanza kama mtu huru baada ya miaka 30 jela kwa kosa ambalo hakufanya. Photo Credits: theatlantic.com
Wiki hii, mmoja wa wafungwa nchini Marekani, ambaye alikuwa kwenye orodha ya wanaosubiri kunyongwa kutokana na kuhukumiwa kifo kwa mauaji  aliyotuhumiwa kufanya mwaka 1984 aliachiwa huru baada ya Jaji kukubali kuwa hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuonyesha kuwa ni yeye aliyeshiriki mauaji hayo.

Sasa, mfungwa huyu atalipwa dola 25,000 kwa kila mwaka aliotumikia kifungo hicho, lakini, kwa mujibu wa sheria ya Louisiana, kiwango cha juu anachoweza kulipwa ni dola 250,000

Ina maana, atalipwa kwa miaka 10 tu kati ya 30 aliyokaa gerezani

Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Tuesday, 11 March 2014

[AUDIO]: Kipindi cha FAMILIA. Siku ya wanawake duniani‏

Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Kipindi hiki kilirushwa moja kwa moja (live) Jumamosi Machi 8, 2014

Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulijikita zaidi katika SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ambapo wageni Mary Ndaro akiwa Wichita Kansas na Mch. Tumaini Mwanyonga  walijadili kwa mapana suala hili.

Wamegusa mengi mema ambayo ni muhimu kuyasikiliza.





Photo Credits: happyholidays2014.com

Monday, 10 March 2014

Jikoni Leo; Njoo Tupike Na Chef Kile-Kuchoma Ndizi Mzuzu kwa Oven na Mengine!!!!!

Waungwana;"Jikoni Leo" Tupo na Njoo Tupike Na Chef Kile.

Vijiwe/Vibaraza vya Mapishi kwa sasa Vinakuwa Kwa Kaaasi.
Sasa kama wewe ni Mpishi/Unapenda Kujifunza ,Mpenzi wa mapishi mbalimbali Wakati ndiyo huu.
Nisiwachoshe na Maneno Meengi...
Twende Sote sasa;"Jikoni Leo" Na....





Jee kuna faida/umejifunza kitu hapa?

Mimi hii ya Ndizi  Mzuzu kwa Oveni nimeondoka nayo/Nimejifunza!!!!

Zaidi ingia;youtube.Njoo Tupike /http://www.njootupike.com/

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.