Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 11 April 2014

Jikoni Leo;Kitchen Boss- Date Night Dessert,Buddy and wife Lisa..!!!!!

Waungwana;"Jikoni Leo" mimi huwanafuatilia/Mpenzi Sana wa  vipindi vya huyu Bwana..Basi leo nikaona vyema nikusogezee hapa, kama wewe hujapata kuviona Au ulipitwa na hiki au kingine basi upate uhondo kidooogo....

Mwanaume Jiko au?

Mwanaume akipenda jiko/kupika  wengi wao wanakuwa wapishi wakubwa na kuwa kazi na yenye kumuingizia Pesa.Lakini Wanawake wengi ,wapishi wanaishia kupikia familia, mitaani/mama Ntilie.... ni wachache sana inakuwa kazi ya Maana/kumuingizia pesa. Hivi ni kwanini?


"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Tuesday, 8 April 2014

Maangalizi ya afya Washington DMV...bure‏



Wataalam wa afya DMV (HCP Metro DC) wanatuleta huduma ya afya kwa wale wasiokuwa na bima ya afya. Huduma hii itatolewa kwa usawa bila kujali dini,rangi,umri,uraia au uchumi.



Kama una rafiki, ndugu au  mzazi asiyekuwa na bima ya afya tunaomba mshiriki ili tuwe na jamii inayoshamiri na yenye afya njema. Zoezi hili litachukuwa hatua ya kuwaona wale watakaokuwa na hali pungufu ya afya njema mara moja kwa mwezi.




Tarehe: 04/12/2014   (Jumamosi)
Saa 3:00 asubuhi hadi mchana 7:00 (waweza kuja hata kwa saa moja)  
MAHALA
3621 Campus Drive, 
College Park, MD 20740

Leo hii wadau wetu tunaomba tujitolee kufanikisha huduma hii ya maangalizi ya afya ya bure kwa wadau wa DMV. 

Unaweza kujitolea kwa namna mbalimbali


  • Iwe ni kumsadia mtu usafiri,
  • kuandikisha majina ya wanaokuja
  • kubeba na kupanga meza kabla na baada ya maangalizi
  • au kushiriki katika timu ya kitaalam
Tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe nesiwangublog@gmail.com ili tuweze kupata idadi na uhakika wa msaada wako.

Monday, 7 April 2014

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA. Mauaji kwenye kambi ya jeshi Fort Hood‏

Jenerali Mark Milley, Kamanda wa Fort Hood akizungumza na waandishi wa habari  
Wiki iliyopita, nchi ya Marekani ilikumbwa na mauaji mengine yaliyotokea kwenye kambi ya jeshi huko Fort Hood, Texas.

Jumatano Aprili 2, askari mmoja wa Jeshi la nchi hiyo, Ivan Lopez ambaye
inasemekana alikuwa na matatizo ya msongo wa mawazo, aliwafyatulia
risasi na kuwaua wanajeshi wenzake 3, kujeruhi 16 kabla hajajigeuzia
bastola na kujiua

Mauaji haya, yanarejesha kumbukumbu ya mauaji
makubwa kabisa kutokea kwenye kambi za jeshi nchini humo, yaliyotokea
kwenye kambi hiyohiyo takriban miaka 5 iliyopita.



Hii ni sehemu ya
ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA
kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam
Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Sunday, 6 April 2014

Tumalizie JumaPili hii kwa Amani;Burudani-PASTOR ANTHONY MUSEMBI - Unastahili na ni Wewe,Mataifa Yote,Unaweza,natamani Wamebarikiwa,Nakuabudu Na Angalia.!!!!!

Wapendwa;Nimatumaini yangu JumaPili hii Imeenda/inaendelea Vyema...Muwe na Amani,Baraka,Rehema, na Upendo

Mwanangu,usiisahau sheria yangu,Bali moyo wako uzishike amri zangu.


Neno La Leo;Mithali:3:1-10
Rehema na kweli zisifarakane nawe;Zifunge shingoni mwako;Ziandike juu ya kibao cha moyo wako
.




Mmmmhhhhh..MUNGU ni MWEMA SAANA.


"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Wote Mliopita Hapa.

Wednesday, 2 April 2014

Wa Afrika Na Sherehe zao Leo Tupo ;RWANDA: TWIN BROTHERS MARRY TWIN SISTERS!!!!!!




Mwenzangu umeonaje hii Arusi?
Mimi nimeona kama hawana Furaha..sijui wamelazimishwa au Utiifu/Heshima...
Tunawatakia kila la kheri na Baraka.

Mengi sina karibu kwa Maoni Yako.

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Monday, 31 March 2014

Jikoni Leo; Nyama Choma - How to Eat Your Meat the East African Way,Tanzanian Mishkaki - Beef and Chicken Kebabs

Waungwana;"Jikoni Leo" Mmmmmmhhh mambo ya mitaani Bongo Tanzania....
Lakini wa Ughaibuni/Ng'ambo..hasa U.K. Hali ya hewa kwa sasa si mbaya saaana..unaweza kufanya mambo haya.





Shukrani;Mark Wiens

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Sunday, 30 March 2014

Nawatakia JumaPili Njema na Happy Mother's Day;Burudani kutoka -African Gospel.....[Mchanganyiko]!!!!!!!!


Happy Mother's Day to all mothers, may GOD bless you.
Natumaini Jumapili hii inaendelea vyema..

Lakini  yanenaje?Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo.

Neno La Leo;Warumi:10:5-15

Tena wahubirije, wasipopelekwa?kama ilivyoandikwa,Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema. 




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana