Wapendwa;Nawatakia JumaPili yenye Unyenyekevu,Upole,Uvumilivu,Upendo na Umoja....
Kwahiyo nawasihi,mimi niliye mfungwa katika BWANA,Mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa;
Kwa unyenyekevu wote na upole,kwa uvumilivu,mkichukuliana katika upendo.
Neno La Leo;Waefeso:4:1-16
3.Na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.4.Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5.BWANA mmoja,imani moja,ubatizo mmoja.
6.MUNGU mmoja,naye ni BABA wa wote,aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote.
7.Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo.
"Swahili Na Waswahili"MUNGU Atubariki Sote.