Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 19 May 2014

Mahojiano ya Maggid Mjengwa na Kwanza Production‏


Maggid Mjengwa


Karibu katika mahojiano mwanahabari makini na wa muda mrefu ambaye pia ni mmiliki wa Kwanza Jamii, Maggid Mjengwa na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production.
Amegusia mambo mbalimbali kama masuala ya uandishi, siasa (kama mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba) na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.

Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu masuala tofauti yaliyo muhimu kwa mustakabali wa nchi za Afrika Mashariki
Karibu

Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

Friday, 16 May 2014

Matembezi ya Mswahili Vijijini;Burudani-Nuta Jazz Band (Tanzania) - Pongezi Wakulima (60's Tanzanian Rumba!)

Waungwana;Nipatapo muda huwa napenda kuzunguka/Kutembea na kujifunza/kujione mambo yakoje...
Basi Leo niwapeleke Shamba /Vijijini kidogo.

Swali.....
Wakulima wa Ng'ambo wapi wanapatia na Wakulima wa Afrika wapi wanakosea?
Jee Mkulima ni Mtu Masikini/Fukara,Mnyonge,Kaishiwa na........?

Jee unapenda kuwa Mkulima?








Nuta....Pongezi kwa Wakulima...


"Swahili Na Waswahili" Muwe na Wakati Mwema.

Monday, 12 May 2014

Boko Haram: Waonyesha wasichana waliotekwa


Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara


Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Kanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.

Habari zaidi;http://www.bbc.co.uk/swahili/habari

Shukrani.

Sunday, 11 May 2014

Nawatakia JumaPili Njema;Burudani-Umoja One SDA Church choir Volume 3 DVD



Wapendwa;Nawatakia JumaPili Njema,Amani,Baraka,Upendo,Utuwema,Kweli,Shukrani,Tumaini,Imani,Upole kiasi na Utukufu Turudishe kwa BWANA......


Sisi twatokana na MUNGU.Yeye amjuaye MUNGU atusikia;yeye asiyetokana na MUNGU hatusikii.Katika hili twamjua Roho wa kweli,na roho ya upotevu.........

Neno La Leo;Waraka wa Kwanza wa Yohana:4;1-21
Kuzipima Roho;1-6
MUNGU ni Pendo;7-21


Na amri hii tumepewa na yeye,ya kwamba yeye ampendaye MUNGU,Ampende na ndugu yake.


Mhhhhhh.......
 Asante/Shukrani;Umoja SDA

"Swahili Na Waswahili"MUNGU Atubariki Sote.

Sunday, 4 May 2014

Nawatakia JumaPili Njema;Burudani,Kijitonyama-Twaokolewa kwa Neema Na Nyingine!!!!!!!!

Wapendwa nawatakia JumaPili Njema na Yenye Baraka,Amani,Upendo na Utukufu Turudishe kwake BWANA....

Mimi nitasimama katika zamu yangu,nitajiweka juu ya mnara,nitaangalia ili nione atakalo niambia, na jinsi nitakavyojibu katika habari ya kulalamika kwanngu.
Neno La Leo;Hababkuki;2:1-5.


BWANA akanijibu akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji.





"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.