Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 28 May 2014

Amina's Baby Shower,Coventry,UK.!!!!!!

Mapokezi/Twasubiri Mgeni...

Michezo......
Mawilimatatu,Kutakiana kheri,kucheka/Furaha.....


Kucheza tulicheza....

Baadhi ya wanakamati ikiongozwa na Zayana[Mwasu]



Ilkuwa  Shughuli ndogo ya[Suprise] Baby Shower ya Amina[Emmy].
Iliandaliwa na Dada yake Zayana[Mwasu] mwenye nguo Nyekundu,Akishirikiana na Baadhi ya Ndugu,Jamaa na Marafiki.
Ilifanyika Coventry,UK.
Pia wageni mbalimbali kutoka Birmingham na Vitongoji vingine walijumuika pamoja.

Da'Zayana[Mwasu] Anawashukuru sana Wote kwa,Zawadi,kutoa Muda,Upendo na Mengineyo.
MUNGU awabariki na Kuwaongezea pale mlipopunguza na zaidii.
Anawapenda Wote.

Burudani/Muziki na kaka Paul....
Muongozaji wa Shughuli/MC;Da'Rachel siwa[Kachiki]
Picha na Mpiga Picha wetu wa Swahili Na Waswahili;Da'Neema[Nyanyile]



"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Tuesday, 27 May 2014

Mjadala na Hussein Kauzela, Shamis Khatry, Liberatus Mwang'ombe na Solomon Christopher‏




Karibu katika mjadala na Hussein Kauzela, Shamis Khatry, Liberatus Mwang'ombe na Solomon Christopher uliojikita zaidi katika mwenendo wa kusaka katiba mpya nchini Tanzania.

Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu suala hili muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Tanzania.
Karibu

Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

Monday, 26 May 2014

Mahojiano ya Idd Ligongo (Bicco) na Kwanza Production‏



Idd
Photo Credits: Idd's Facebook Page 
Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Idd Ligongo
Msanii na mwanahabari makini ambaye amezungumza mengi mema kuhusu Sanaa na Habari ya Tanzania.
Amezungumzia historia yake katika fani hizi, ilipo na anapoiona ikielekea

Ni kati ya mazungumzo ninayoamini utapata mengi ya kujifunza.
KARIBU UNGANE NASI


Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

Sunday, 25 May 2014

Natumaini JumaPili hii Inaendelea Vyema;Burudani-Emmy Kosgei-Asiyalasun,Jerusalem!!!!!!!



Wapendwa;Natumaini JumaPili inaendelea Vyema,Iwe Yenye Amani,Baraka,Upendo,Rehema na Furaha..
Ndugu zangu,wengi wenu msiwe waalimu.Kama mjuavyo,sisi waalimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine.
Neno La Leo;Yakobo:3:1-18

Je,ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu?Basi,aoneshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na Hekima.

Ulimi;1-12
Hekima itakayo juu mbinguni;13-18






"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Thursday, 22 May 2014

Siku Kama Ya Leo Da'Tracey-Sarah Alizaliwa[13]!!!!!!!





Wapendwa/Waungwana;Siku kama ya Leo Binti Yetu Mpendwa,Da'Tracey-Sarah,Alizaliwa.
 Leo ametimiza miaka 13.Tunamshukuru sana MUNGU kwa Zawadi hii,Tunamtakia Masomo/Maisha Mema yenye Baraka,Amani,Upendo,Hekima.
Awe Baraka kwetu na Jamii pia.
Awe Kichwa na si Mkia.
MUNGU akumpe miaka mingi ,Akupe Maono/Njozi na Ukapate Kufanikisha Ndoto zako.
MUNGU azidi kumsimamia kila iitwapo Leo.


Mungu Ukawajaalie na wale wanaotafuta Watoto.

Shukrani kwa Wote Mnaoungana/Mlioungana/Mnaoendelea kuungana nasi Katika Malezi,MUNGU azidi kuwatendea kila lililo Jema.


Pia tunawatakia kheri na Baraka Watoto/Watu  wote waliozaliwa siku kama ya leo.


Familia ya Isaac tunawapenda Wote na Asanteni kwa yoooote!!



"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Monday, 19 May 2014

Mahojiano ya Maggid Mjengwa na Kwanza Production‏


Maggid Mjengwa


Karibu katika mahojiano mwanahabari makini na wa muda mrefu ambaye pia ni mmiliki wa Kwanza Jamii, Maggid Mjengwa na Mubelwa Bandio wa Kwanza Production.
Amegusia mambo mbalimbali kama masuala ya uandishi, siasa (kama mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba) na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.

Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu masuala tofauti yaliyo muhimu kwa mustakabali wa nchi za Afrika Mashariki
Karibu

Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

Friday, 16 May 2014

Matembezi ya Mswahili Vijijini;Burudani-Nuta Jazz Band (Tanzania) - Pongezi Wakulima (60's Tanzanian Rumba!)

Waungwana;Nipatapo muda huwa napenda kuzunguka/Kutembea na kujifunza/kujione mambo yakoje...
Basi Leo niwapeleke Shamba /Vijijini kidogo.

Swali.....
Wakulima wa Ng'ambo wapi wanapatia na Wakulima wa Afrika wapi wanakosea?
Jee Mkulima ni Mtu Masikini/Fukara,Mnyonge,Kaishiwa na........?

Jee unapenda kuwa Mkulima?








Nuta....Pongezi kwa Wakulima...


"Swahili Na Waswahili" Muwe na Wakati Mwema.