Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 15 June 2014

Tumalizie JumaPili hii Kwa Baraka;Hongera Kina Baba Wote[Happy Father's Day];Burudani,John Lisu - Yu Hai Jehovah,Fungua Macho!!!!



"Happy Father's Day" BABA wa Watoto Wangu ,BABA Yangu  Japo Hayupo Duniani/Ametangulia ,
Kina BABA woote mnaojua majukumu yenu kama BABA..Na Mnaotarajia kuwa BABA,Mnaopenda kuwa BABA Lakini bado labda kwa sababu moja au Nyingine....MUNGU Awabariki sana sana ,Awape kheri,Hekima,Busara,Amani Katika Malezi Yenu!!!!



Wapendwa;Natumaini JumaPili hii InaendeleaVyema/Imekuwa Njema...Mbarikiwe Sana Wote..

Utabarikiwa mjini,Utabarikiwa na mashambani.Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, Na uzao wa nchi yako,Na uzao wa wanyama wako wa mifugo,maongeo ya  ng'ombe wako,Na wadogo wa kondoo zako.......


Neno La Leo:Kumbukumbu la Torati;28:1-15.
[Baraka kwa Wanaotii]


Litabarikiwa kapu lako,Na chombo chako cha kukandia unga..........






"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.

Saturday, 14 June 2014

Friday, 13 June 2014

Watoto Na Mitindo,Michezo;Summer Collection;[Maandalizi Ya Familly Fun Day]!!!!!!






Hamjambo Wazazi/Walezi na Watoto wangu Wapendwa?  Summer Time....Wakati wa Jua umewadia,Hiki ni kipindi kizuri sana hapa Ng'ambo kwa Michezo ya Nje,Unaweza kuvaa vizuri na si nguo nyiingi yaani makoti,Masweta na.......Pia kunakuwa na Likizo[Summer Holiday].

Maandalizi Ya  "Family Fun Day" zaidi itakuwa Michezo;Kuchora,Kuimba,Kucheza,Mitindo,Kuangalia Vipaji vya Watoto wetu,Nyama Choma na VyaKula vingine,  Kufurahi Pamoja... na Watoto.

Wengi huwa wanakwenda Likizo Afrika na sehemu nyingine kwa wale watakao kuwepo kwa mwaka huu tutafanya tukutane na kucheza pamoja.
Itakuwa baada ya mfungo wa Ramadhani ili  wote tufurahi pamoja.
  Tarehe 02/08 panapo Majaaliwa.


Kama kuna Ushauri,Msaada katika kuandaa na Mengine yote,Usisite kuwasiliana nami.
Email;rasca@hotmail.co.uk.
Simu;0750 44 100 40.


Wote Mnakaribishwa katika Yote.

kuhusu mambo ya Watoto zaidi;http://watotonajamii.blogspot.co.uk/

Swali;Kwanini watoto wetu ni waoga?

Kwanini Hawajiamini?
Kwanini wana Aibu?

Monday, 9 June 2014

Kuelekea Kombe la Dunia...Mahojiano na Halifa Ramadhan kutoka Brazil‏



Photo Credits: EyesOnNews.com 
Siku chache kabla ya kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la Soka huko Brazil, mambo mengi yamekuwa yakizungumzwa kuhusu maandalizi ya michuano hiyo.
Kuna malalamiko na maandamano nchini humo ambavyo kwa hakika vinaleta taswira isiyo njema kuhusu maandalizi ya michuano hiyo
Kutaka kujua mengi, Kwanza Production imefanya mahojiano na Halifa Ramadhan.

Mtanzania mwenye maskani yake nchini Brazil ambaye amezungumzia mengi kuhusu maandalizi ya fainali za kombe la dunia na pia maisha ya nchini humo kwa ujumla.
KARIBU UUNGANE NASI
Kwa maoni ama ushauri tuandikie kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Sunday, 8 June 2014

Natumaini JumaPili hii inaendelea Vyema;Burudani-Kinondoni Revival Choir,Ninakushukuru,Mtu wa Nne!!!!!!


Wapendwa Natumaini JumaPili inaendelea vyema....
Iwe yenye Imani,Tumaini,Kusifu/Kuabudu na Kushukuru....

Basi,mfalme Nebukadneza akashangaa,akainuka kwa haraka na kuwauliza washauri wake,"Je,hatukuwafunga watu watatu na kuwatupa motoni?Nao wakamjibu mfalme,"Naam,mfalme!Ndiyo!"


Neno La Leo;Kitabu Cha Danieli;3:1-30

Nebukadneza anasimamisha sanamu;1-7
Marafiki wa Danieli;8-18
Wenzake Danieli wanahukumiwa;19-25

Vijana wanaachwa huru;26-30

Kisha akauliza,"Lakini  sasa mbona ninaona watu wanne wakitembeatembea humo motoni bila kufungwa na wala hawadhuriki, na mtu wa  nne anaonekana kama  mwana wa MUNGU?"



"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Wote.

Saturday, 7 June 2014

Mahojiano ya Dekula Kahanga "Vumbi" na Kwanza Production‏


Karibu katika mahojiano ya Kwanza Production na Dekula Kahanga "Vumbi"
Vumbi ambaye anamiliki Dekula Band nchini Sweden

Amezungumzia mambo mengi ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa albamu yake mpya ya Shujaa Mamadou Ndala iliyozinduliwa Aprili 23 na 24 huko Sweden.

Pia, ametoa ushauri kwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaotaka kufanya muziki nchi za Scandinavia

KARIBU UUNGANE NASI

Kwa maoni na ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Sunday, 1 June 2014

Tumalizie JumaPili Hii Hivi;Burudani-Mbele "sala sikoyo " na Nyingine..!!!!!


Wapendwa tumalizie JumaPili hii kwa Hekima,Busara,Amani,Upendo na Furaha....

Mwenyezi-MUNGU akujibu uwapo taabuni;Jina la MUNGU wa Yakobo likulinde.

Neno La Leo;Zaburi;20:1-9
Wengine hujigamba kwa magari ya vita;
Wengine hujigamba kwa farasi wao.
Lakini sisi twajivunia Mwenyezi-MUNGU,MUNGU wetu.
 





"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima