Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 1 October 2014

Mahojiano na Dr Patrick Nhigula. Mgombea u-Rais wa DICOTA

Karibu katika mahojiano kati ya Mubelwa Bandio wa Kwanza Production na Dr Patrick Nhighula, mgombea wa nafasi ya uRais wa DICOTA 2014. Mbali na kuielezea DICOTA yenyewe, pia ameeleza nia yake kugombea nafasi hiyo
Karibu umsikilize


Thursday, 25 September 2014

Hotuba ya Rais Kikwete kwenye mkutano wa tabianchi, Umoja wa Mataifa


Photo Credits: UN Photo/Ryan Brown
Septemba 23, 2014, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk Jakaya Kikwete, ambaye pia ni kiongozi wa kamati ya viongozi wa nchi na serikali za Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi alihutubia kikao kilichoandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Kin Moon kujadili changamoto za mabadiliko ya tabianchi duniani. 
Hii ni hotuba yake, kwa hisani ya Umoja wa Mataifa


Sunday, 21 September 2014

Tumalizie Jumapili hii Vyema;Burudani-Judy Jacobs - Days of Elijah (No God Like Jehovah) holy Ghost filled song,I will worship you(I exalt thee)......

Wapendwa;Tumalizie Vyema,Mungu azidi kuwatendea,Tusikate tama,Tuwe na tumaini,Tupendane na Tusaidie wenye kuhitaji......Mungu awe Mlinzi Wetu...

Aketie mahali pa siri pake Aliye juu, Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi....

Neno La Leo;Zaburi;91:1-16

2;Nitasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,Mungu wangu nitakayemtumaini.
3;Maana yeye atakuokoa na mtego wa mwindaji,Na katika tauni iharibuyo.

4;Kwa manyoya yake atakufunika,Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;Uaminifu wake ni ngao na kigao.


 


"Swahili Na Waswahili"Muwe Na Wakati Mwema.

USIKU WA DENIS B. MSAKI (NASIBU) NA SIAEL NDANI YA UKUMBI WA GREEN LEAF KIMARA KOROGWE


Kati kati ni Bwana na Bibi Denis (Nasibu) Msaki wakiwa na wasimamizi wao katika harusi yao takatifu iliyofungwa katika kanisa la Roman Katoliki parokia ya Mavurunza Kimara jijini Dar es salaam.
Maharusi Denis na Siael wakimtanguliza Mungu kabla ya kuanza kwa sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Green leaf Kimara Korogwe.
 
Bwana na Bibi Denis (Nasibu) Msaki siku ya jana ya tarehe 20/09/2014 ndio siku yao ambayo walikuwa wanaisubiri kwa muda mrefu baada ya kutimiza ndoto yao katika uchumba wao na kufunga ndoa takatifu katika kanisa la Roma parokia ya Mavurunza Kimara jijini Dar na baadae ikafuatiwa na sherehe ya nguvu iliyofanyika katika ukumbi wa Green leaf uliopo Kimara korogwe jijini Dar es salaam.
Sherehe hiyo iliongozwa na MC msanii maarufu wa maigizo Bwana Novatus Michael anayejulikana kwa jina la kisanii kama Nova

Sunday, 14 September 2014

Worshiping YouGod is fighting for us, pushing back the darkness, - Deluge!!!!!!!


Wapendwa;Natumaini Jumapili hii inaendelea vyema,Iwe yenye Baraka,Amani,Upendo,Imani,Haki na Hekima.....

Kama vile Ibrahim alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki....

Neno La Leo;Wagalatia;3:1-29
Fahamu basi,Ya kuwa  wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu....








"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Thursday, 11 September 2014

Jikoni Leo;How to cookUgali[Tanzania/Kenya]Sadza[Zimbabwe]Nshima[Zambia/Malawi]Pap[SouthAfrica]Fufu [West Africa].......

Waungwana;"Jikoni Leo" ni Ugali kwa sisi Waswahili tunaita hivyo..kila watu wanajina lao...kikubwa mlo!!!!!!
Nafikiri ni chakula kinacholiwa na Wa-Afrika/sehemu kubwa Afrika.. kama siyo wote...wapo wale wasioupenda tuu lakini wanaujua..hata kwetu wapo.
Kuna wanaosema Ugali wa Ng'ambo hauivi vizuri,haunogi.....,pia kuna wanaosema Ugali wa majiko haya ya Umeme,gesi na....haunogi/hauivi vyema....Ugali mtamu na kuiva vyema ule wakupikia Kuni,Mkaa...



to cook sadza

Mbira JunctionMbira Junction
Thanks

Pia watoto wengi wanaoishi Ng'ambo hawapendi Ugali..Sababu ni nini?

Je watoto wako wanapenda Ugali?


Pia watu wengine wanaoshi Ng'ambo wanapika Ugali mwingi na kuweka kwenye Fridge/ Freezer..ili akihitaji anapasha tuu..vipi hii wewe unaweza?

Ugali unamboga zake....
Ugali unaupishi wake...usiwe na mabuja,vidongevidonge...

Lakini kila kitu kisizidi,kikizidi hakinogi..basi si kila siku Ugali.

Asante;Tanzania na da'

 


Zimbabwe;Thanks


Tahanks;
AfricaCookingChannel

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Mitindo Afrika;Asili Ya Kanga

 



Shukrani;qtvkenya
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.