Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 3 November 2014

Jikoni Leo na Mitindo-Ubah Hassan

Waungwana; Jikoni Leo,Wa Afrika/Wasomali na Mitindo...
Leo tuungane da'Ubah Hassan..ni Msomali anayeishi Ng'ambo.

Si mwanamitindo tuu na jikoni pia anahusika....
basi nisikuchoshe..


Tuungane na da'Ubah...
 


Shukrani/Thanks;Andrew Day

Na kwa mambo ya mitindo zaidi nifuate;http://mitindoafrica-abroad.blogspot.co.uk/
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Sana.

Saturday, 1 November 2014

Natumaini Juma Pili ilikuwa/Inaendelea Vyema;Burudani-Kinondoni Revival Choir- Twalilia Tanzania,Imekwisha na Nyingine.....!!!!!

Wapendwa;Nawatakia Jumapili njema,Yenye Baraka,Tumaini,Imani,Upendo,Furaha,Shukrani na Utukufu tumrudishie Mungu......

18  Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.
19  Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
Neno La Leo;Zaburi 145
1  Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.
2  Kila siku nitakuhimidi, Nitalisifu jina lako milele na milele.
3  Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana, Wala ukuu wake hautambulikani.
4  Kizazi kwa kizazi kitayasifu matendo yako, Kitayatangaza matendo yako makuu.
5  Nitaifikiri fahari ya utukufu wa adhama yako, Na matendo yako yote ya ajabu.
6  Watu watayataja matendo yako ya kutisha, Nami nitausimulia ukuu wako.
7  Watalihubiri kumbukumbu la wema wako mkuu. Wataiimba haki yako.
8  Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma, Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
9  Bwana ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote.
10  Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru, Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
11  Wataunena utukufu wa ufalme wako, Na kuuhadithia uweza wako.
12  Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13  Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote, Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.
14  Bwana huwategemeza wote waangukao, Huwainua wote walioinama chini.
15  Macho ya watu wote yakuelekea Wewe, Nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16  Waufumbua mkono wako, Wakishibisha kila kilicho hai matakwa yake.
17  Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
18  Bwana yu karibu na wote wamwitao, Wote wamwitao kwa uaminifu.
19  Atawafanyia wamchao matakwa yao, Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.
20  Bwana huwahifadhi wote wampendao, Na wote wasio haki atawaangamiza.
21  Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana; Wote wenye mwili na walihimidi jina lake takatifu milele na milele.










Shukrani;

Kinondoni Revival Choir.

    Africha Entertainment


"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Friday, 31 October 2014

Wazo La Leo; Na Mswahili-Emu-three Wa Diary Yangu.....


WAZO LA LEO: Sio kila jambo la heri laweza kirahisi tu, kuna mambo mengine huja na mitihani yake, lakini mwisho wake huwa ni neema, na furaha kama utakuwa mvumilivu na kusimamia kwenye haki.Halikadhalika mambo ya ubaya, yana mvuto wake, usipokuwa makini unaweza kuzama kwenye giza nene, na mwisho wa ubaya ni kudhalilika, na kuumbuka, na kawaida majuto huja baadaye, kama utafanikiwa kujinasua. Tujitahidi sana kuwa makini katika matendo yetu, tusivutike tu kwa tamaa, tuangalie uzuri na ubaya wake kwanza.

kwa Hadithi/Visa/Mikasa ya Maisha,Usikose pitia hapa;http://miram3.blogspot.co.uk/

Dunia Yangu ndiyo hadithi/kisa kinachoendelea sasa....[Sehemu Ya 56]

Twende Pamoja..!!!!

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Wednesday, 29 October 2014

Jikoni Leo;Sheikha Agili-How to Make Swahili Biriyani..!!!!!!

Waungwana;"Jikoni Leo" na Sheikha Agili,Jinsi ya Kupika Swahili Biriyani..
Mimi nimpenzi wa mapishi ya bi Sheikha..


Nawe kama mpenzi wa Mapishi/Mpishi unaweza kutushirikisha mapishi yako...nasi tukajifunza kupitia wewe....Mlango upo wazi karibu sana.Haya tujifunze kupika biriyani....
Twende pamoja na bi'Sheikha...
.

Shukrani;Sheikha Agil

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Monday, 27 October 2014

Mswahili Wetu Leo;Da'Zahabu Luciannne -Tabia Ya Bibi mbele ya Bwana[Haya Wamama wa Ng'ambo kazi kwenu]..

Waungwana; Mswahili wetu Leo...da'Zahabu Lucianne...
Haya Wamama wa Ng'ambo kwanini Hamuwaheshi ma Bwana?
 Mnasugulishaga ma Bwana masaani,Kutwa mpo kwa Facebook na Musimu......
Muache kuita ma Bwana majinaa eeh Bwana yako eehh.........


Twende pamoja na da'Zahabu...





Shukrani;Augmanify

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Sunday, 26 October 2014

Wapendwa muendelee na Jumapili Vyema;Burudani-Pole wana Congo Uamusho,Wasiwasi mjini, Choir CBCA Bugabo/ Bukavu, RD-CONGO,



Wapendwa;Nawatakia Jumapili Njema yenye ,Amani,Busara,Hekima na Kupendana Kindugu..
Neno La Leo;Warumi:13:1-14

Kupendana kindugu
8Msiwe na deni kwa mtu yeyote, isipokuwa tu deni la kupendana. Ampendaye jirani yake ameitekeleza sheria.9Maana, amri hizi: “Usizini; Usiue; Usitamani;” na nyingine zote, zimo katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.” 10Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, upendo ni utimilifu wa sheria.
11Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: Sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini.12Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga.13Na tuishi kwa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana, na wala sio kwa ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu. 14Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha.



"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima.

Wednesday, 22 October 2014

Jikoni Leo;MAman Nicole loboko cuisine congolise tilapia na mayebo..!!!


Waungwana;"Jikoni Leo" Tupo Congo kwa Mamaa Nicole.
Mengi sina tujifunze Mapishi tuu..kama Lugha gongana/inasumbua, samahani kwa hilo twende pamoja kwa kufuatilia vitendo..Tutapata kitu tuu.










Shukrani;matsombe Samba

"Swahili Na Waswahili" Pamoja Daima