Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 8 December 2014

Tunaweza Badilika - Mzee Yusuf & Khadija Kopa


Collabo ya kihistoria kati ya Mfalme Mzee Yusuf na Malkia Khadija Kopa katika wimbo na video ya pamoja yenye malengo ya kuhamasisha jamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake.

Video hii iliyorekodiwa mkoani Morogoro inamuonyesha Mzee Yusuf na Khadija Kopa kama mume na mke ambao wamebahatika kupata watoto wawili 'Kulwa' na 'Doto' ambao ni mapacha. Mzee Yusuf ni dereva wa daladala wakati Khadija ni mama wa nyumbani lakini pia mjasiriamali.

Pamoja na kwamba watoto wao ni mapacha ambao wanafanana na kulingana kwa karibu kila kitu ikiwemo umri lakini tofauti ya jinsi yao inaonekana kumpa haki zaidi mtoto wa kiume ambaye anaonekana kuelekea shuleni wakati pacha mwenzie anaonekana kuhangaika na shughuli za nyumbani ikiwemo kutafuta maji, kufanya usafi n.k.

Kwa upande mwingine, Mzee anaonekana kutokuijali familia yake haachi pesa ya matumizi nyumbani na hata anapoulizwa anakuwa mkali sana wakati huo huo anaonekana kuchezea mabinti wengine akiwa kazini.

Stori inabadilika kabisa pale mzee anapokutana na Mwanamabadiliko ambaye anafanikiwa kumshawishi kubadili tabia hizo kwa ajili ya manufaa ya familia yake. Kuanzia hapo Mzee anaonekana akinunua nguo za shule za mwanae wa kike na kubandika ujumbe wa mabadiliko katika gari na nyumba yake.

Baada ya hapo maisha yanaonekana kuwa ya raha mustarehe.

"Tukae na tu-starehe tule raha na maisha." Kinasema kibwagizo katika wimbo huo.



Shukrani,zaidi ingia;Tunaweza

Sunday, 7 December 2014

Muendelee na Jumapili Hii Vyema;Burudani- Mchanganyiko Tusifu na Kuabudu...!!!

Wapendwa nawatakia/Muendelee na Jumapili hii Njema...
Leo sina mengi..Tusifu na Kuabu..MUNGU wetu ni mwema sana sana...
Tuwaweke kwenye maombi/sala watu wote wenye Shida/Tabu,Wanaopitia Majaribu,kukata tamaa,Wenye kuhitaji.....2Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, 


Neno la Leo;Yakobo1:1-27
Salamu;1
Imani na hekima;2-8

Umaskini na utajiri;9-11
Majaribio;12-18
Kusikia na kutenda;19-27

Bible Society of Tanzania









"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Monday, 1 December 2014

Mswahili Wetu Leo;da'Louise UWACU-U&I TALK [ NUBI-KMT ] Episode 3 in Ki SWAHILI

Mswahili wetu Leo ni "da'Louise"..yeye ni mzaliwa wa Rwanda[Mnyarwanda].
da'Louise yeye anapenda kujifunza zaidi kiswahili...

Basi nisikuchoshe ungana na dada huyu wa Kinyarwanda...Hongera da'Louise.



Thanks/Shukrani;uwacuvideo

"Swahili Na Waswahili"Pamoja sana.

Sunday, 30 November 2014

Nawatakia Jumapili Njema;Burudani-Angela Chibalonza- Uliniumba nikuabudu na Nyingine....

Wapendwa;Natumaini jumapili ilikuwa/ inaendelea Vyema,
1Njoni tumwimbie Mwenyezi-Mungu,
tumshangilie mwamba wa wokovu wetu!

Neno La Leo;Zaburi:95;1-11
Utenzi wa kumsifu Mungu
1Njoni tumwimbie Mwenyezi-Mungu,
tumshangilie mwamba wa wokovu wetu!
2Twende mbele zake na shukrani;
tumshangilie kwa nyimbo za sifa.
3Maana Mwenyezi-Mungu, ni Mungu mkuu;
yeye ni Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4Vilindi vyote vya dunia vimo mikononi mwake,
vilele vya milima ni vyake.
5Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya;
kwa mikono yake aliiumba nchi kavu.
6Njoni tusujudu na kumwabudu;
tumpigie magoti Mwenyezi-Mungu, Muumba wetu!
7 Maana yeye ni Mungu wetu,
nasi ni watu wa kundi lake,
ni kondoo wake anaowachunga.
Laiti leo mngesikiliza sauti yake:
8“Msiwe wakaidi kama kule Meriba,
kama walivyokuwa kule Masa jangwani,
9wazee wenu waliponijaribu na kunipima,
ingawa walikuwa wameona mambo niliyowatendea.
10Kwa miaka arubaini nilichukizwa nao,
nikasema: ‘Kweli, hawa ni watu waliopotoka!
Hawajali kabisa njia zangu!’
11 Basi, nilikasirika, nikaapa:
‘Hawataingia mahali pangu pa pumziko!’”
Bible Society of Tanzania



"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.

Friday, 28 November 2014

Jikoni Leo; Na Mswahili-Chef Issa[Issa Kapande]..

Waungwana;"Jikoni Leo"Tuangalie/Tujifunze na Mpishi wa Leo ni Mswahili, kaka yetu huyu Isaa Kapande...
Mapishi ya Viazi...Mmmhh kila mtu anaupishi wake si vibaya tukijufunza Mapishi mbalimbali.
Hata nawe kama ni mpishi/unapenda mapishi usisite kutushirikisha nasi tukajifunza kupitia mapishi yako.Tutumie kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk
Pia usisite kuuliza pale ulipokwama/shindwa...kama wewe unajua hiki na kuna wengine wanajua kile,   Tunaweza kujifunza kupitia wengine.

Mimi natatizwa/siwezi kupika hafu keki[Half cake]..kama maandazi lakini yale yanakuwa Magumu na yamekatika katika..
Tanzania/Dar... mara nyingi yanashushiwa/kinywaji cha Tangawizi...
Msaada waungwana mwenye kuyajulia......










Shukran;Zaidi-activechef/http://activechef.blogspot.co.uk/

"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Sunday, 23 November 2014

Muendelee Na Jumapili hii Vyema;Burudani-Freedom (Live from Faith Christian Center) - Kenneth Reese

Wapendwa nawatakia jumapili njema,yenye Baraka,Furaha,Upendo,Amani,Shukrani,Upole kiasi......
34Nawapeni amri mpya: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. 35Mkipendana, watu wote watajua kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu.”

Neno La LeoYohana:13:1-36.
Amri mpya
31Baada ya Yuda kuondoka, Yesu akasema, “Sasa Mwana wa Mtu ametukuzwa, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. 32Na kama utukufu wa Mungu umefunuliwa ndani ya Mwana, basi, naye Mungu ataudhihirisha utukufu wa Mwana ndani yake mwenyewe, na atafanya hivyo mara. 33“Watoto wangu, bado niko nanyi kwa muda mfupi tu. Mtanitafuta, lakini sasa nawaambieni yale niliyowaambia viongozi wa Wayahudi: ‘Niendako nyinyi hamwezi kwenda!’ 34Nawapeni amri mpya: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. 35Mkipendana, watu wote watajua kwamba nyinyi ni wanafunzi wangu.”
Bible Society of Tanzania

I wanna clap a little louder than before,I wanna sing a little louder than before,
I wanna Jump higher than before,I wanna shout louder than before.........Hallelujah..!!!!




"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.