Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 30 December 2014

Mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma???


 Amani, Heshima na Upendo kwa wana-blog wote.

Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo mpaka sasa.

Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo. Ni harakati kubwa sana hasa katika kusonga na maisha yetu ya kila siku na pia kuendeleza gurudumu hili la blogs

Nimekuwa nikituma makala, vipindi na kazi zangu kwenu nanyi mmekuwa wakarimu sana kuzipokea. Ushirikiano ambao umenifanya nizidi kujivunia kuwa mmoja wa bloga

Lakini pia, najivunia sana
kuwasiliana na kila mmoja wetu hivi sasa ili kuanzisha mjadala wa changamoto zilizo mbele
yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii.

Ningependa tuanze kwa kujiuliza, Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu.

Nashukuru
kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya
kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (Bofya hapa) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blogu zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (Ipitie hapa)

Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.

Lakini
kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa
safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.

Bloga awekaye picha
anataka kuionesha jamii alichokiona.

Bloga ahabarishaye anataka kuihabarisha
jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka
kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye
biashara anataka jamii ijue palipo na huduma ama biashara husika. Afunzaye mapishi, mitandao,
mavazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.

Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.

Na hili ni lengo jema.

Lakini swali linarejea kuwa......

Mwaka huu ambao unaomalizika wiki hii unaonekana
kuwa hatua gani kwetu?

Logo hapo juu inaonyesha hatua iliyopihgwa katika siku za mwisho za mwaka. Kuanzishwa kwa mtandao wa bloga ambao (ukitumiwa vema) utakuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi.

Ninalowaza ni hili.....

Vipi tunaweza kuweka nguvu na jitihada zetu pamoja kuweza kuitumikia vema na kwa ufasaha jamii yetu???

Mafanikio
ya bloga mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA, lakini tunalostahili kufanya sasa, ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema
tutendalo.



Tunapoumaliza mwaka 2014, tuangalie nyuma na kujiuliza, mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma??





Na jibu la swali hili, liwe CHANGAMOTO YETU sote



Baraka kwenu nyote



Heri ya Mwaka Mpya 2015

Monday, 29 December 2014

NesiWangu Show...........Malaria Kit

NesiWangu Show ni kipindi kinachokusudia kuongeza mwako katika uwanja wa Afya, upatikanaji wa huduma zake na elimu-afya kwa jamii.

Katika kipindi hiki, tunazungumza na Mkurugenzi wa Jenga Tanzania Foundation, Nassor Basalama anayezungumzia kuhusu kipimo cha Malaria ambacho Jenga Tanzania Foundation inapanga kukisambaza bure kwa watu wa kipato cha chini nchini Tanzania.


Karibu uungane nasi.....

Thursday, 25 December 2014

Heri ya Sikukuu ya Christmas Wapendwa/Waungwana..!!!

Wapendwa/Waungwana;Nawatakia Heri,Baraka,Furaha,Amani na Upendo katika siku kuu hii ya Christmas.
Shukrani sana kwa Familia yangu,Ndugu,Jamaa,Marafiki na Wote tunaofanya/shirikiana kwa namna moja au nyingine.
kwa ujumbe/zawadi na kwa yote...

Shukrani za pekee kwa da'Rose Miriam Kinunda,[http://tasteoftanzania.com/blog/]
MiriamKinunda.commimi na familia yangu tunasema asante sana na Mungu azidi kukubariki pamoja na familia yako kila iitwapo Leo.(you surprised our famliy)
Muwe na Wakati mwema leo na siku zote.


Mathayo 2:1-23
1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema,

2 Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.

3 Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye.

4 Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi?

5 Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,

6 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

7 Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota.

8 Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie.

9 Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto.

10 Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno.

11 Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.

12 Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.




"Swahili Na Waswahili"Pamoja daima.

Monday, 15 December 2014

Jikoni Leo;[Mkate wa Mchele]Makate or Rice Cake na Raihana Mulla...

Waungwana "Jikoni Leo" na bi'Rahiana Mulla..Mapishi ni Mkate wa Mchele[Mkate wa kumimina].
Waswahili wanasema Mchele mmoja Mapishi mbalimbali..

Haya tuendelee kujifunza......

Thanks/Shukrani;Zaidi-Raihana Mulla
"Swahili Na Waswahili"Pamoja daima.

Friday, 12 December 2014

Swahili/Kiswahili Na Waswahili;ULIMI, MATAMSHI, NA KUKAA UGENINI

Watangazaji wa DW wakijadili na kujadiliana masuala kadhaa ya kilugha likiwemo lugha asilia ya mtu huathirika vipi akikaa ugenini kwa muda mrefu, yaani kwenye mazingira ambako lugha yake ya kuzawa nayo haitumiki? Jee, matamshi yake yatapotoshwa mpaka aonekane msemaji mgeni kila azungumzapo kwa lugha yake asilia? Na vipi msamiati wake, utapigwa na wakati au la?







Shukrani;John Mtembezi Inniss

Monday, 8 December 2014

Tunaweza Badilika - Mzee Yusuf & Khadija Kopa


Collabo ya kihistoria kati ya Mfalme Mzee Yusuf na Malkia Khadija Kopa katika wimbo na video ya pamoja yenye malengo ya kuhamasisha jamii kupinga ukatili dhidi ya wanawake.

Video hii iliyorekodiwa mkoani Morogoro inamuonyesha Mzee Yusuf na Khadija Kopa kama mume na mke ambao wamebahatika kupata watoto wawili 'Kulwa' na 'Doto' ambao ni mapacha. Mzee Yusuf ni dereva wa daladala wakati Khadija ni mama wa nyumbani lakini pia mjasiriamali.

Pamoja na kwamba watoto wao ni mapacha ambao wanafanana na kulingana kwa karibu kila kitu ikiwemo umri lakini tofauti ya jinsi yao inaonekana kumpa haki zaidi mtoto wa kiume ambaye anaonekana kuelekea shuleni wakati pacha mwenzie anaonekana kuhangaika na shughuli za nyumbani ikiwemo kutafuta maji, kufanya usafi n.k.

Kwa upande mwingine, Mzee anaonekana kutokuijali familia yake haachi pesa ya matumizi nyumbani na hata anapoulizwa anakuwa mkali sana wakati huo huo anaonekana kuchezea mabinti wengine akiwa kazini.

Stori inabadilika kabisa pale mzee anapokutana na Mwanamabadiliko ambaye anafanikiwa kumshawishi kubadili tabia hizo kwa ajili ya manufaa ya familia yake. Kuanzia hapo Mzee anaonekana akinunua nguo za shule za mwanae wa kike na kubandika ujumbe wa mabadiliko katika gari na nyumba yake.

Baada ya hapo maisha yanaonekana kuwa ya raha mustarehe.

"Tukae na tu-starehe tule raha na maisha." Kinasema kibwagizo katika wimbo huo.



Shukrani,zaidi ingia;Tunaweza

Sunday, 7 December 2014

Muendelee na Jumapili Hii Vyema;Burudani- Mchanganyiko Tusifu na Kuabudu...!!!

Wapendwa nawatakia/Muendelee na Jumapili hii Njema...
Leo sina mengi..Tusifu na Kuabu..MUNGU wetu ni mwema sana sana...
Tuwaweke kwenye maombi/sala watu wote wenye Shida/Tabu,Wanaopitia Majaribu,kukata tamaa,Wenye kuhitaji.....2Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, 


Neno la Leo;Yakobo1:1-27
Salamu;1
Imani na hekima;2-8

Umaskini na utajiri;9-11
Majaribio;12-18
Kusikia na kutenda;19-27

Bible Society of Tanzania









"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Wote.