Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 12 January 2015

HUYU NA YULE........Mahojiano na Dr Talib Ali


Karibu katika kipindi cha HUYU NA YULE ambapo wiki hii tumeongea na Dk Talib Ali

Yeye ni mwanzilishi wa Avatar Dental Care iliyopo Leesburg Virginia.

Ameeleza mengi kuhusu kazi zake na mikakati aliyonayo baadae
Pia, ametoa punguzo la 50% kwa waTanzania watakaoenda kutiiwa kwake, pamoja na mpango wa malipo ya awamu kuwzesha watu kumudu gharama hizo

Karibu
Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production

Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com
.

Friday 9 January 2015

Monday 5 January 2015

HUYU NA YULE.......Mahojiano na Dr Crispin Semakula

Karibu katika kipindi cha HUYU NA YULE ambapo wiki hii tumeongea na Dr Crispin Semakla.

Daktari wa mahgonjwa ya kisukari, shinikizo la damu na pia Mwalimu wa Afya katika Chuo Kikuu nchini Marekani

Pia ni mwanzilishi wa Access Medical and Dialysis Center iliyopo Dar Es Salaam

Ameeleza mengi kuhusu maradhi anayoshughulika nayo na pia kituo chake.


Huyu na Yule ni kipindi kinachotayarishwa na Vijimambo Blog na kuzalishwa na Kwanza Production

Kwa mawasiliano, maoni ama ushauri, tafadhali wasiliana nasi kupitia kwanzaproduction at gmail.com

Sunday 4 January 2015

Heri Ya Mwaka Mpya Na Muwe na Jumapili Njema;Burudani-10,000 Reasons (Bless the Lord) - Matt Redman,COVERED | Official Planetshakers Video

Wapendwa/Waungwana;Nimatumaini yangu mmevuka salama mwaka 2014 na mmeanza vyema mwaka huu mpya wa 2015.
Nawatakia kila lililo Jema,Furaha,Amani,Upendo,Mafanikio,Ushindi.
Wanaotafuta wenza Mungu akawaonyeshe walio wao,Wanaohitaji Watoto Mungu akawabariki,Uwe mwaka wa Shuhuda na Mkono wa Mungu ukawaguse wenye Shida/Tabu.
Mungu akaonekane kwa kila muhitaji.
Tuwe na Upendo wa kweli,Tusameheane,Tuchukuliane,Tusibebe mizigo isiyo ya lazima.
Tusahau yaliyopita na Tuanze upya.
Mungu ni Mwema sana.
Nawapenda wote.



1Hapo mwanzo, Mungu aliumba mbingu na dunia. 2Dunia ilikuwa bila umbo na tupu. Giza lilikuwa limefunika vilindi vya maji na roho ya Mungu ilikuwa ikitanda juu ya maji.
3Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa.4Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, 5mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.
Neno La Leo;Mwanzo1:1-31
26Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” 27 Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. 28Mungu akawabariki na kuwaambia, “Zaeni muongezeke, mkaijaze nchi na kuimiliki; muwatawale samaki wa baharini, ndege wa angani, na kila kiumbe hai kitembeacho duniani.”
Bible Society of Tanzania

You have removed my shame,
You take as I am
You call me justified,
Now I am covered by Your grace







"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Friday 2 January 2015

Maelezo ya Mwanasheria wa Uhamiaji kuhusu sheria mpya za uhamiaji nchini Marekani


Mwanasheria wa uhamiaji Fatmata Barrie akizungumza na wanaDMV kwenye mkesha wa mwaka mpya
Katika mkesha wa mwaka mpya (2014-2015), Jumuiya ya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia , kulikuwa na matukio mbalimbali.

Moja wapo lilikuwa ni maelezo ya mwanasheria wa uhamiaji Fatmata Barrie kuhusu maamuzi mapya ya serikali ya Marekani kwenye sheria za uhamiaji.

Karibu umsikilize

Wednesday 31 December 2014

Chaguo La Mswahili Leo-Pharrell Williams- Happy From Tanzania,DRC-Congo-Kinshasa,Goma,Burundi,Rwanda

Waungwana;Natumaini wote Mnafuraha,Amani,Upendo.....
kama wewe huna hivyo pole sana na Mungu   yu pamoja nawe!!!!!

Because I'm Happy...........!!!!!!!!
Be Happy.......!!!!!!!















"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Tuesday 30 December 2014

Mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma???


 Amani, Heshima na Upendo kwa wana-blog wote.

Kwanza namshukuru MUNGU kwa baraka ya uhai ambayo mimi nawe tunayo mpaka sasa.

Pili nikupe pole kwa harakati za maisha ambazo sote twazipitia kufanikisha yale mema tupendayo. Ni harakati kubwa sana hasa katika kusonga na maisha yetu ya kila siku na pia kuendeleza gurudumu hili la blogs

Nimekuwa nikituma makala, vipindi na kazi zangu kwenu nanyi mmekuwa wakarimu sana kuzipokea. Ushirikiano ambao umenifanya nizidi kujivunia kuwa mmoja wa bloga

Lakini pia, najivunia sana
kuwasiliana na kila mmoja wetu hivi sasa ili kuanzisha mjadala wa changamoto zilizo mbele
yetu kama JAMII YA WANA-BLOG wenye lengo la kuigusa jamii.

Ningependa tuanze kwa kujiuliza, Je! Tunasonga mbele ama nyuma katika harakati zetu.

Nashukuru
kwa blogs na tovuti mpya ambazo zinachipuka na kuendeleza nia njema ya
kuigusa jamii. Kaka Luta Kamala aliwahi kuandika akijuliza KWANINI TUNA-BLOG? (Bofya hapa) na hata Kaka Chambi Chachage aliuliza kama uwepo wa blogu zetu unakuza ama kufifisha tasnia nzima ya uandishi (Ipitie hapa)

Jibu halisi tunalo mioyoni mwetu kulingana na dhamira tulizonazo.

Lakini
kwa ujumla, haijalishi ni sababu gani ilikufanya u-blog, mwisho wa
safari sote tunajikuta na zao moja ama "mlaji" mmoja ambaye ni JAMII.

Bloga awekaye picha
anataka kuionesha jamii alichokiona.

Bloga ahabarishaye anataka kuihabarisha
jamii. Yule aandikaye Utambuzi anataka jamii ijitambue. Anayeweka
kumbukumbu ni sababu anataka jamii ije isome baadaye. Atangazaye
biashara anataka jamii ijue palipo na huduma ama biashara husika. Afunzaye mapishi, mitandao,
mavazi, mitindo nk, woote wanalenga katika kuielimisha jamii.

Kwa maana nyingine sote twaiandikia JAMII.

Na hili ni lengo jema.

Lakini swali linarejea kuwa......

Mwaka huu ambao unaomalizika wiki hii unaonekana
kuwa hatua gani kwetu?

Logo hapo juu inaonyesha hatua iliyopihgwa katika siku za mwisho za mwaka. Kuanzishwa kwa mtandao wa bloga ambao (ukitumiwa vema) utakuwa chachu ya mabadiliko ya nchi hasa kwa mwaka huu wa uchaguzi.

Ninalowaza ni hili.....

Vipi tunaweza kuweka nguvu na jitihada zetu pamoja kuweza kuitumikia vema na kwa ufasaha jamii yetu???

Mafanikio
ya bloga mmoja mmoja yanaweza kudhihirisha kuwa TUNAWEZA, lakini tunalostahili kufanya sasa, ni kushirikiana na kuwa makini katika kila jema
tutendalo.



Tunapoumaliza mwaka 2014, tuangalie nyuma na kujiuliza, mwaka unakatika....Tumesonga mbele ama nyuma??





Na jibu la swali hili, liwe CHANGAMOTO YETU sote



Baraka kwenu nyote



Heri ya Mwaka Mpya 2015