1Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi? 2Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja.
Neno La Leo;Wafilipi 2:1-30
Unyenyekevu na ukuu wa Kristo
1Je, maisha yenu katika Kristo yanawapeni nguvu? Je, upendo wake unawafarijini? Je, mnao umoja na Roho Mtakatifu na kuoneana huruma na kusikitikiana nyinyi kwa nyinyi? 2Basi, ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na fikira moja, upendo mmoja, moyo mmoja na nia moja. 3Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.4Pasiwe na mtu anayetafuta faida yake mwenyewe tu bali faida ya mwenzake. 5Muwe na msimamo uleule aliokuwa nao Kristo Yesu: 6Yeye, kwa asili alikuwa daima Mungu;lakini hakufikiri kwamba kule kuwa sawa na Munguni kitu cha kungangania kwa nguvu.7Bali, kwa hiari yake mwenyewe,aliachilia hayo yote, akajitwalia hali ya mtumishi,akawa sawa na wanadamu,akaonekana kama wanadamu.8Alijinyenyekesha na kutii mpaka kufa,hata kufa msalabani.9Kwa sababu hiyo Mungu alimkweza juu kabisa,akampa jina lililo kuu kuliko majina yote.10Ili kwa heshima ya jina la Yesu,viumbe vyote mbinguni, duniani na kuzimu,vipige magoti mbele yake,11na kila mtu akiri kwamba Yesu Kristo ni Bwana,kwa utukufu wa Mungu Baba.
"Swahili Na Waswahili" Mbarikiwe Sana.