Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 19 April 2015

Katika kipindi cha "HUYU NA YULE" kesho (Jumatatu), usikose kujua UNDANI wa maisha ya Linda‏


NI MENGI AMEZUNGUMUZA AMBAYO MIMI NA WEWE HATUKUYAJUA
Kesho Jumatatu katika kipindi cha huyu na yule cha mahojiano na mwanamitindo mbunifu wa LB kutoka Atlanta, Georgia atakapoelezea historia yake yenye milima na mabonde historia ya maisha yake yenye huzuni na furaha wakati mwingine Linda akitokwa na machozi kwa kukumbuka maisha aliyopitia. Je Mume wake Mali walijuana nae wapi? na mengine mengi kuhusu maisha yake ikiwemo kampuni yake ya LB na malengo yake ya kupeperusha bendera ya Tanzania anga za kimataifa. USIKOSE mahojiano yaliyofanywa na mwakilishi wa Vijimambo na kwanza production Michigan Alpha Igogo ambae alitaka kujua undani wa maisha ya mwanadada Linda


Alpha Igogo akifanya mahojiano na Linda jijini Atlanta
Maswali yalikua moto Linda akipumua na kumkumbatia Alpha Igogo baada ya mahojiano kufikia mwisho

MKUTANO MKUBWA WA NENO LA MUNGU WA WASABATO WATANZANIA WAISHIO NCHINI MAREKANI WATOTO WATENGEWA SEHEMU YAO.‏


 Watoto wakiwa sehemu yao chini ya uangalizi maalumu huku wazazi wao wakihudhuria mkutano mkubwa wa neno la Mungu unaondelea DMV kwa siku nne ikiwa leo Jumampili April 19, 2015 ndio hitimisho la mkutano huo.
 Watoto wakiangalia vipindi vya watoto kwenye luninga.
 Msimamizi wa watoto Tanya Muganda akielekeza jambo.
 Tanya Muganda akiwapatia zawadi watoto

Wednesday, 15 April 2015

Tuesday, 14 April 2015

WANAFUNZI WA CARMAN AINSWORTH HIGH SCHOOL WATEMBELEA UBALOZI WATANZANIA WASHINGTON DC.


 Wanafunzi wa Carman Ainsworth High School iliyopo Michigan watembelea ubalozi wa Tanzania Washington DC, na kupata fursa ya kuonana na Mhe balozi Liberata Mulamula.

                      Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza kwa makini Mhe, balozi Leberata Mulamula.

                             Mhe, balozi Liberata Mulamula akitoa historia fupi ya Tanzania.


                      Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwashukuru wageni wake kwa kuchagua ubalozi wa Tanzania kama sehemu mojawapo ya ziara yao hapa mjini Washington DC.

Sunday, 12 April 2015

Tumalizie Jumapili hii Vyema;Burudani-Chidumule- furaha yangu,Mwansasu&Chidumule-Yesu Ni Bwana na Mwasongwe....


Wapendwa;Nawatakia kila lililo jema..Nawapenda wote

58Basi, ndugu zangu wapenzi, simameni imara na thabiti. Endeleeni daima kuwa na bidii katika kazi ya Bwana, mkijua kwamba kazi mnayofanya katika utumishi wa Bwana haitapotea bure.

Neno La Leo;Wakorintho:15:1-58

Ufufuo wa Kristo
Ufufuo wetu

Mwili wa ufufuo
Bible Society of Tanzania









"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.