Friday, 24 April 2015
SHEREHE YA CHAUKIDU YA MCHANA CHUO CHA HOWARD YAFANA
Rais wa CHAUKIDU Prof Lioba Moshi watatu toka kushoto akimkaribisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi mara tu alipowasili kama mgeni rasmi chuo kikuu cha Howard Washington, DC katika sherehe ya chama cha ukuzaji wa Kiswahili Duniani siku ya Alhamisi April 23, 2015 kulia ni Prof Venessa White Jackson
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtambulisha mkewe mama Sitti Mwinyi kwa mwenyeji wao Prof Lioba Moshi pia na yeye akimtambulisha mama Sitti Mwinyi kwa Prof Venessa White Jackson kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula .
Prof Lioba Moshi Rais CHAUKIDU akielezea historia fupi ya CHAUKIDU na baadae kumkaribisha Rais mstaafu kuongea na wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya chama hicho iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015 katika chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
Ms Mamburi Lyambaya (kushoto) akimtambulisha Prof Venessa White Jackon na yeye kuwasalimia wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya CHAUKIDU iliyofanyika katika chuo kikuu cha Howard Washington, DC.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa meza kuu kulia ni prof Venessa White Jackson '
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba kwa kuwashukuru CHAUKIDU kwa kummpa mwaliko na kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa lugha ya Kiswahili hakusita kukubali kuja kujumuika nao pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliwapongeza kwa kuitangaza lugha ya Kiswahili nchini Marekani.
Kutoka kushoto ni Balozi wa Umoja wa Afrika Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na mama Sitti Mwinyi wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Howard wakiimba nyimbo za Kiswahili kwa ustadi mkubwa kuliko wastajabisha Watanzania na wadau wengine wa Kiswahili.
Wadau wa Kiswahili wakifuatilia sherehe ya CHAUKIDU
WADAU WA KISWAHILI SIKU YA CHAUKIDU CHUO KIKUU CHA HOWARD
Asha Nyang.anyi akiwa kwenye meza akikagua majina ya wadau wa Kiswahili kwenye sherehe ya Chama Cha Ukuzaji Wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) inayoendelea sasa hizi chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC na Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi atakua mgeni rasmi.
Wadau wa Kiswahili wakiendelea kuingia ukumbini.
Wadau kutoka Zanzibar wakipata picha
Walimu wa kiswahili wa vyuo mbalimbali wakipata picha ya pamoja.
wadau wa Kiswahili wakihudhuria sherehe ya CHAUKIDU
Walimu na maporofesa wa vyuo wakiwa ndani ukumbi wa Blackburn Center siku ya Alhamisi April 23, 2015 chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
Wadau wa Kiswahili wakibadilishana mawili matatu.
Wadau wa Kiswahili wakilonga Picha zaidi Baadae
Wednesday, 22 April 2015
BALOZI MPYA WA ANGOLA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.
Mhe, balozi wa Angola Agostinho Tavares akipokelewa na afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi .
Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwa na furaha baada ya mgeni wake kufika ofisini .
Mhe balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Angola Agostinho Tavares.
Mhe Balozi wa Angola nchini Marekani Agostinho Tavares akiweka sahihi kitabu cha wageni.
Mhe balozi wa Angola chini Marekani Agostinho Tavares akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha .
Mhe balozi Libarata Mulamula na balozi wa Angola nchini marekani Agostinho Tavares pamoja na afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme walipokua wakibadilishana mawazo.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI
RAIS MSTAAFU MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI AWASILI JIJINI WASHINGTON DC.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiambata na mama Sitti Mwinyi wawasili jijini Washington DC tayari kwa tamasha maalum la Chama cha Ukuzaji wa RaisiKiswahili Duniani.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa utawala Lilly Munanka wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, mara alipowasili hotelini.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi Edward Taji.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Emmanuel Swere.
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi John Anbiah
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiwa ameongozana na mama Sitti Mwinyi na baadhi ya msafara wake katika hoteli waliyofikia.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI
BALOZI WA RWANDA NCHINI MAREKANI MHE. MATHILDA MUKANTABANA ATEMBELEAAFISI ZA UMOJA WA AFRIKA WASHINGTON, DC.
Mhe Balozi wa Rwanda Profesa Mathilda Mukantabana akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa AU Mhe. Amina Salum Ali alipotembelea ofisi za Umoja wa Afrika uliopo Washington, DC nchini Marekani .Balozi Profesa Mathilda anachukua uongozi wa mikutano wa mabalozi wa Afrika katika kipindi cha mwezi April hadi July 2015 akiwakilisha kanda ya Afrika Mashariki.
Monday, 20 April 2015
Mahojiano na Linda Bezuidenhout (LB) Pt I
Karibu katika sehemu ya kwanza ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout
Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo
Nani alimfanya ashawishike na fani hii?
Maisha yake kimahusiano je?
Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake?
KARIBU
Ameeleza mengi ikiwa ni pamoja na historia yake kwa ufupi, safari yake kwenda nje ya nchi, alivyorejea na kuanza harakati zake za mitindo
Nani alimfanya ashawishike na fani hii?
Maisha yake kimahusiano je?
Familia yake sasa na inavyokabiliana na kazi zake?
KARIBU
Subscribe to:
Posts (Atom)