Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday 24 April 2015

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI APENDEZESHA SHEREHE YA CHAUKIDU SILVER SPRING, MARYLAND NCHINI MAREKANI


Meza kuu toka kushoto ni Rais wa CHAUKIDU Prof.Lioba Moshi, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi wakuhudhuria sherehe ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani. Mhe. Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa mgeni rasmi sherehe iliyofanyika Silver Spring, Maryland nchini Marekani siku ya Alhamisi April 23, 2015 na kuhudhuriwa na wadau wa Kiswahili kutoka mataifa mbalimbali wakiwemo Wamarekani wanaozungumuza lugha ya Kiswahili.
Dr. Hamza Mwamoyo mkuu wa idhaa ya Kiswahili Voice of Amerika (VOA) akimsabahi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi huku wakipata picha ya kumbukumbu wenginine kwenye picha ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi.
Farida(kulia) wa Farida Catering akiwaelekeza Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi, Mama Sitti Mwinyi na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula aina ya vyakula alivyopika katika kuhitimisha sherehe ya CHAUKIDU siku ya Alhamisi April 23, 2015 Silver Spring, Maryland nchini Marekani. Hii ni mara ya pili kwa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuonja mapishi ya Farida Catering mara ya kwanza ilikua katika shere ya miaka 3 ya Vijimambo iliyofanyika mwaka 2013 Capitol Heights.
Farida akiwaonyesha ustadi wa ukutaji matunda Rais mstaafu Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na Mama Sitti Mwinyi.
Prof. Lioba Moshi akiongea machache ya kumshukuru Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuhudhuria sherehe ya CHAUKIDU tangia mchana na usiku bila kuchoka pia alimshukuru Balozi wa Tanzania nchini Marekani kwa kuwezesha kuja nchini kwa Rais Msataafu aliyependezesha na kunogesha sherehe ya chama chao na baadae alimkaribisha Balozi Liberata Mulamula kuongea machache.
Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa CHAUKIDU kwa kufanikisha sherehe yao na baadae aliwatambulisha maafisa na wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani akiwemo Balozi wa heshima Ahmed Issa na wadau mbalimbali wakiwembo waandishi wa vitabu Kapuya kutoka California na Mzee Safari kutoka Maryland na baadae kumkaribisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuongea na wadau wa Kiswahili nchini Marekani.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongea na wadau wa Kiswahili katika kuhitimisha sherehe ya CHAUKIDU iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015 Silver Spring, Maryland. Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi mbali na kuwashukuru CHAUKIDU pia alitumia fulsa hiyo kuweka sawa baadhi ya maneno la lugha ya Kiswahili ambayo hukosewa kutamkwa ipasavyo kwa kutoa mfano alisema katika kiswahili kahuta tarehe 1 au tarehe 2 usahihi ni tarehe mosi na tarehe pili huku akitolea mfano kwa lugha ya kiingereza kwamba hata nao hutamka 1st na 2nd mfano mwingine alisema unaposema nawaahidini ni ahadi unayotoa kwa watu wasiokuwepo mbele yako lakini unaposema ninakuahidini ndio sahihi kwa ahadi unayotoa kwa watu waliopo mbele yako na mengine mengi.
Kamati nzima ya CHAUKIDU ikipata picha ya kumbukumbu 

Mzee Mwinyi ahutubia wadau wa Kiswahili Washington DC


Ifuatayo ni hotuba ya Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Ali Hassan Mwinyi alipohutubia mkutano wa nne wa Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) uliofanyika tarehe 23 Aprili 2015 katika Chuo Kikuu Cha Howard jijini Washington DC

KARIBU




SHEREHE YA CHAUKIDU YA MCHANA CHUO CHA HOWARD YAFANA


Rais wa CHAUKIDU Prof Lioba Moshi watatu toka kushoto akimkaribisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi mara tu alipowasili kama mgeni rasmi chuo kikuu cha Howard Washington, DC katika sherehe ya chama cha ukuzaji wa Kiswahili Duniani siku ya Alhamisi April 23, 2015 kulia ni Prof Venessa White Jackson 
 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akimtambulisha mkewe mama Sitti Mwinyi kwa mwenyeji wao Prof Lioba Moshi pia na yeye akimtambulisha mama Sitti Mwinyi kwa Prof Venessa White Jackson kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula .  
Prof Lioba Moshi Rais CHAUKIDU akielezea historia fupi ya CHAUKIDU na baadae kumkaribisha Rais mstaafu kuongea na wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya chama hicho iliyofanyika siku ya Alhamisi April 23, 2015 katika chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.


Ms Mamburi Lyambaya (kushoto) akimtambulisha Prof Venessa White Jackon na yeye kuwasalimia wadau wa Kiswahili waliohudhuria sherehe ya CHAUKIDU iliyofanyika katika chuo kikuu cha Howard Washington, DC.




Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiwa meza kuu kulia ni prof Venessa White Jackson '


Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba kwa kuwashukuru CHAUKIDU kwa kummpa mwaliko na kwa kuwa yeye ni mdau mkubwa wa lugha ya Kiswahili hakusita kukubali kuja kujumuika nao pia Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliwapongeza kwa kuitangaza lugha ya Kiswahili nchini Marekani.


Kutoka kushoto ni Balozi wa Umoja wa Afrika Mhe. Amina Salum Ali, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula na mama Sitti Mwinyi wakifuatilia hotuba ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.


Wanafunzi wa chuo kikuu cha Howard wakiimba nyimbo za Kiswahili kwa ustadi mkubwa kuliko wastajabisha Watanzania na wadau wengine wa Kiswahili.


Wadau wa Kiswahili wakifuatilia sherehe ya CHAUKIDU

WADAU WA KISWAHILI SIKU YA CHAUKIDU CHUO KIKUU CHA HOWARD




 Asha Nyang.anyi akiwa kwenye meza akikagua majina ya wadau wa Kiswahili kwenye sherehe ya  Chama Cha Ukuzaji Wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) inayoendelea sasa hizi chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC na Rais msataafu Ali Hassan Mwinyi atakua mgeni rasmi.
Wadau wa Kiswahili wakiendelea kuingia ukumbini.
 Wadau kutoka Zanzibar wakipata picha
 Walimu wa kiswahili wa vyuo mbalimbali wakipata picha ya pamoja.
 wadau wa Kiswahili wakihudhuria sherehe ya CHAUKIDU
 Walimu na maporofesa wa vyuo wakiwa ndani ukumbi wa Blackburn Center siku ya Alhamisi April 23, 2015 chuo kikuu cha Howard kilichopo Washington, DC.
 Wadau wa Kiswahili wakibadilishana mawili matatu.
Wadau wa Kiswahili wakilonga Picha zaidi Baadae

Wednesday 22 April 2015

BALOZI MPYA WA ANGOLA ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC.



 Mhe, balozi wa Angola Agostinho Tavares akipokelewa na afisa wa ubalozi  Swahiba Mndeme alipotembelea ubalozi .
 Mhe, balozi Liberata Mulamula akiwa na furaha baada ya mgeni wake kufika ofisini .
 Mhe balozi Liberata Mulamula kwenye picha ya pamoja na mgeni wake balozi wa Angola Agostinho Tavares.
 Mhe Balozi wa Angola nchini Marekani Agostinho Tavares akiweka sahihi  kitabu cha wageni.
 Mhe balozi wa Angola chini Marekani Agostinho Tavares akimsikiliza kwa makini mwenyeji wake balozi Liberata Mulamula alipokua akijitambulisha .
Mhe balozi Libarata Mulamula na balozi wa Angola nchini marekani Agostinho Tavares pamoja na afisa wa ubalozi Swahiba Mndeme walipokua wakibadilishana mawazo.
               PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI

RAIS MSTAAFU MHESHIMIWA ALI HASSAN MWINYI AWASILI JIJINI WASHINGTON DC.


 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiambata na mama Sitti Mwinyi wawasili jijini Washington DC tayari kwa tamasha maalum la Chama cha Ukuzaji wa RaisiKiswahili Duniani.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa utawala Lilly Munanka wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC, mara alipowasili hotelini.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi Edward Taji.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme.
  Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa wa Ubalozi Emmanuel Swere.
 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa ubalozi John Anbiah
     Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Ali Hassan Mwinyi akiwa ameongozana na mama Sitti   Mwinyi na baadhi ya msafara wake katika hoteli waliyofikia.
                                  PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI

BALOZI WA RWANDA NCHINI MAREKANI MHE. MATHILDA MUKANTABANA ATEMBELEAAFISI ZA UMOJA WA AFRIKA WASHINGTON, DC.




Mhe Balozi wa Rwanda Profesa Mathilda Mukantabana akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa AU Mhe. Amina Salum Ali alipotembelea ofisi za Umoja wa Afrika uliopo Washington, DC nchini Marekani .Balozi Profesa Mathilda anachukua uongozi wa mikutano wa mabalozi wa Afrika katika kipindi cha mwezi April hadi July 2015 akiwakilisha kanda ya Afrika Mashariki.