Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 29 April 2015

Makala ya JK katika ibada ya kusimikwa Askofu jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu




Shukrani;ikulu mawasiliano


"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

BALOZI WA UMOJA WA AFRIKA AMINA SALUM ALI ATOA RAMBI RAMBI KWA KIFO CHA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA


Balozi Amina Salum Ali

Na mwandishi wako, Washington, DC

Balozi wa kudumu wa Umoja wa Afrika, Mhe. Amina Salum Ali leo ametoa salamu za rambi rambi kwa Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita aliyefariki siku ya siku ya Jumapili April 26, 2015 asubuhi na kuzikwa siku ya Jumanne April 28, 2015 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.



Balozi Amina Salum Ali alisema amepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha mmoja wa watumishi wa miaka mingi wa Serikali, Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF), aliendelea kwa kusema Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita atakumbukwa Tanzania, bara nzima la Afrika na dunia kwa jumla kama mmoja wa makamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni barani Afrika, hususan utawala wa kidhalimu wa makaburu Zimbabwe na Afrika ya Kusini na hatimaye kuachiwa huru kwa aliyekuwa Rais mzawa wa kwanza nchini Afrika Kusini, hayati Nelson Mandela.



Mzee Mbita alijitoa mhanga kuongoza mapambano ya ukombozi wa Afrika, Atakumbukwa milele kwa kurudisha heshima ya Muafrika.


Brigedia Jenerali msataafu Hashim Mbita ni mfano uliotukuka kwa watanzania na Afrika.Aliiongoza vizuri sana kamati ya ukombozi ya Umoja wa Afrika Mungu amlaze pema peponi, Amin.


Balozi Amina Salum Ali yupo safarini kuelekea Tanzania.

Monday, 27 April 2015

Mahojiano na mbunifu mavazi Linda Bezuidenhout (LB) Pt II


Karibu katika sehemu ya pili na ya mwisho ya mahojiano na mbunifu wa kimataifa wa mitindo mwenye asili ya Tanzania, Linda Bezuidenhout

 Ameeleza mengi kuhusu kazi yake na familia kwa ujumla.

Anavyokabiliana na kazi zake, changamoto za afanyalo, tuzo alizopata nk

Na pia, kaeleza kuhusu mtazamo wake juu ya waTanzania (hasa wa Diaspora) na ushauri kwa kinamama wote

KARIBU

Sunday, 26 April 2015

Tumalizie Jumapili hii kwa Furaha na Baraka..Burudani;Rebecca Magamba Na Sarah K.....



Wapendwa; Natumai Jumapili Imeisha/Inaendelea vyema...
Mungu Baba azidi kuwalinda na kuwatendea,,Furaha,Amani,Tumaini,Vitawale Nyumbani mwenu..
1Nyinyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa na dhambi zenu. 2Wakati ule mliishi kufuatana na mtindo mbaya wa ulimwengu huu, mkawa mnamtii mtawala wa pepo wenye nguvu wa anga, pepo ambao huwatawala sasa watu wasiomtii Mungu. 3Na hata sisi sote tulikuwa kama wao; tuliishi kufuatana na tamaa zetu za kidunia na kufanya tu mambo yale yaliyoipendeza miili na akili zetu. Kidunia, sisi kama vile pia wao, tulistahili ghadhabu ya Mungu. 4Lakini Mungu ni mwenye huruma nyingi. Alitupenda kwa mapendo yasiyopimika, 5hata, ingawa tulikuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, alitufanya hai pamoja na Kristo. Kwa neema ya Mungu nyinyi mmeokolewa.

 6Kwa kuungana na Kristo Yesu, Mungu alitufufua pamoja naye, tukatawale pamoja naye mbinguni. 7Ndivyo alivyopenda kuonesha kwa watu wa nyakati za baadaye ukuu wa neema yake aliyotujalia kwa ukarimu katika kuungana kwetu na Kristo Yesu. 8Maana, kwa neema ya Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu, bali ni zawadi ya Mungu. 9Wala halitokani na matendo yenu wenyewe, asije mtu akajivunia kitu. 10Sisi ni viumbe vyake Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.

11Nyinyi mlio kwa asili watu wa mataifa mengine – mnaoitwa, “Wasiotahiriwa” na Wayahudi ambao hujiita, “Waliotahiriwa,” (kwa sababu ya kile wanachoifanyia miili yao) – kumbukeni mlivyokuwa zamani. 12Wakati ule nyinyi mlikuwa bila Kristo; mlikuwa nje ya jamii ya Israeli; mlikuwa wageni na hamkuwa na sehemu katika yale maagano aliyoahidi Mungu. Mlikuwa bila matumaini na kama watu wasiomjua Mungu hapa duniani. 13Lakini sasa, kwa kuungana na Kristo Yesu, nyinyi ambao hapo awali mlikuwa mbali, mmekaribishwa kwa njia ya damu yake Kristo. 14Maana Kristo mwenyewe ametuletea amani kwa kuwafanya Wayahudi na watu wa mataifa mengine kuwa jamii moja. Kwa mwili wake yeye mwenyewe aliubomoa ule ukuta uliowatenganisha na kuwafanya maadui. 15Aliiondoa ile sheria pamoja na amri zake na kanuni zake, ili kutokana na jamii hizo mbili aumbe jamii moja mpya katika umoja naye na hivyo kuleta amani. 16Kwa mwili wake, Kristo aliuangamiza uadui wao; kwa msalaba wake aliziunganisha jamii hizo kuwa moja na kuzipatanisha na Mungu.
Neno La Leo;Waefeso 2: 1-22
Kutoka kifo na kuingia katika uhai
Umoja katika Kristo


17Basi, Kristo alikuja akahubiri Habari Njema ya amani kwenu nyinyi watu wa mataifa mengine mliokuwa mbali na Mungu, na pia kwa Wayahudi ambao walikuwa karibu na Mungu. 18Hivyo, kwa njia yake, sisi sote, Wayahudi na watu wa mataifa mengine, tunaweza kumwendea Baba kwa Roho mmoja. 19Basi, nyinyi si wageni tena, wala si watu wa nje. Nyinyi ni raia pamoja na watu wa Mungu, na ni watu wa jamaa ya Mungu. 20Mmejengwa juu ya msingi uliowekwa na mitume na manabii, naye Kristo mwenyewe ndiye jiwe kuu la msingi. 21Yeye ndiye mwenye kuliunganisha jengo lote na kulikuza hata liwe hekalu takatifu kwa ajili ya Bwana. 22Katika kuungana naye, nyinyi pia mnajengwa pamoja na wote wengine, muwe makao ya Mungu kwa njia ya Roho wake.
Bible Society of Tanzania









"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Mno.

MWANDISHI WA VITABU YASIN KAPUYA AKUTANA NA RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI WASHINGTON, DC


Mwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akimwelezea Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi ya jinsi gani vitabu vyake vinavyoweza kumkwamua mwananchi wa hali ya chini na kumfikisha juu katika kumboreshea maisha mapya. Akijitolea mfano wake mwenyewe alipoanzia shimoni Kariakoo mpaka kufika nchni Marekani na sasa kualikwa katika mikutano mikubwa ya kutoa semina ya jinsi gani unavyoweza au kampuni inavyoweza kuwa namba moja katika sekta ya biashara.
Mwandishi wa vitabu Yasin Kapuya akichangia jambo na Katibu Mkuu wa Rais mstaafu Bwn. Abdallah Makame (kulia) aliokua akiongea na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi siku ya Ijumaa April 24, 2015 jijini Washington, DC nchini Marekani.
Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi wakishikilia bango la kitabu chake kipya kitakachotoka hivi karibuni.


Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akimkabidhi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi moja ya vitabu vyake.

Mwandishi wa Vitabu Yasin Kapuya akiagana na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi. Picha na Vijimambo, Kwanza Production


BALOZI LIBERATA MULAMULA AONGOZA MKUTANO WA MABALOZI WA HESHIMA WASHINGTON, DC


Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani akifungua mkutano wa Mabalozi wa Heshima uliofanyika siku ya Ijumaa April 24, 2015 Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani. Mkutano huo ulizungumzia  uwekezaji na Utalii zikiwemo Changamoto zake na jinsi ya kukabiliana nazo. Pia katika mkutano huo uliokua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano uliudhuria pia na Viongozi wa Taasisi za Diaspora wa Tanzania ambao wanaguswa na kuiona nchi yao ikipiga hatua ya maendeleo katia sekta ya uwekezaji na Utalii.


Abdul Majid mwanaDiaspora Mtanzania anayeishi California nchini Marekani akielezea huduma kwa wateja bado ipo kiwango cha chini nchini Tanzania na jinsi gani ikiboreshwa inavyoweza kunua uchumi wa Tanzania.


Balozi wa Heshima Mhe. Kjell Berch akichangia na kuelezea majukumu ya Balozi wa heshima.


Rais wa East Africa Diaspora Business Counsil Benedict Kazora ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas akichanganua na kutoa maelezo yanayoweza na kurahisiha maswala ya uwekezaji na kukosoa baadhi ya makampuni yanavyowekeza Afrika kwa kujinufaisha yenyewe.


Karen Hoffman Rais wa The Bradford Group kutoka New York akielezea sekta ya Utalii na utangazaji wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani.


Balozi wa Heshima Mhe.Cemil Teber kutoka New Mexico akichangia jambo.


Balozi wa Heshima kutoka Ohio Mhe. Patrick Griswold akielezea sekta ya uwekezaji na changamoto inazokutana nazo huku akitoa mfano wake mwenyewe alipokua meneja mkuu wa General Tire miaka ya nyuma na tangia alipoondoka kiwanda kikafa na sasa anatarajiwa kwenda tena Tanzania kujaribu kukifufua upya kiwanda hicho.


Mkutano wa Balozi Liberata Mulamula na Mabalozi wa Heshima ukiendelea


Wakati wa chakula. Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI AFUNGA KIKAO CHA MABALOZI WA HESHIMA WASHINGTON, DC


Rais mstaafu awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiingia chumba cha mkutano cha Nyerere ndani ya mjengo wa Ubalozi Washington, DC siku ya Ijumaa April 24, 2015 kulikokua na kikao cha Mabalozi wa heshima kilichoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani chini ya Balozi Liberata Mulamula kwa ajili kuongelea maswala mbalimbali zikiwemo changamoto za utalii na uwekezaji nchini Tanzania na jinsi gani ya kukabiliana nazo, mbali na Mabalozi hao wa heshima na marafiki zao wengine waliohudhuruia kikao hicho ambacho kilikua sehemu ya maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano ni wawakilishi wa Taasisi za Diaspora za Kitanzania zinazopigana kusaidia maswala ya uwekezaji na Utalii kwa nchi yao Tanzania. Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi pia aliongozana na mkewe Mama Sitti Mwinyi.
Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mwenyeji wake Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwemo Mabalozi wa heshima wakisimama kwa ajili ya nyimbo za Taifa za Tanzania na Marekani.


Mhe. Liberata Mulamula Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimtambulisha Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Mabalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa  taasisi mbalimbali za Kimarekani zinazotangaza utalii wa Tanzania nchini Marekani na baadae kumkaribisha kuongea nao.


Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi akimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani anyoamtambulisha mbele ya mabalozi wa heshima na kwamba yeye Rais mstaafu ndiye aliyefanya mageuzi ya mfumo wa uchumi Tanzania tunaoendelea nao hivi sasa.


Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi akiongea na Mabalozi wa Heshima kuwashukuru kwa kuipenda na kuitangazaTanzania nchini Marekani na kuwaasa wasichoke kwa wao wamekua chachu ya maendeleo ya nchi aipendayo Tanzania.


Mbalozi wa heshima wakiwemo viongozi wa taasisi zinazotangaza Utalii na uwekezaji Tanzania wakimsuikiliza Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
 Picha ya pamoja.
Mayor De  Andre Windom wa mji wa Highland Park jimbo la Michigan akipata picha na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi
Balozi wa Tanzania nchini Marekani akimuaga Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na mkewe mama Sitti Mwinyi wakati walipokua waiondoka baada ya Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kumaliza kufunga kikao cha Mabalozi wa Heshima Ubalozini hapo.
Picha zote na Vijimambo, Kwanza Production