Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 14 June 2015

Wapendwa; Jumapili iendelee kuwa Njema Kwenu,Burudani-Fanuel Sedekia...


Wapendwa/Waungwana Natumaini wote hamjambo na Mungu yu pamoja nanyi.
Na Mnaendelea vyema na Jumapili hii...
Tupo pamoja sana japo wakati mwingine muda unakuwa hautoshi wa kugawa mambo,Lakini Mungu wetu ni mwema sana.
Anazidi kututendea,Kutupigania,Kutulinda,Kutubariki na Kutupa Ushindi.!!
Kwani yeye atosha..Majaribu/Mitihani ni Mapito tuu..Lakini yeye Hashindwi na Jambo.
Basi mpendwa usife moyo kwa unayoyapitia yupo muweza wa yote,Usibebe hiyo mizigo si yako bwana...
Nyanyuka,Simama na uwe na nguvu/Imani Bwana wa Bwana yupo..!!!!


1Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu.2Euodia na Suntike, nawaombeni na kuwasihi mpatane kama ndugu katika Bwana. 3Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai.

Neno La Leo;Wafilipi 4;1-23
Maagizo mbalimbaliShukrani kwa zawadi za Wafilipi

4Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! 5Upole wenu ujulikane kwa watu wote. Bwana yu karibu. 6Msiwe na wasiwasi juu ya kitu chochote, ila kwa kila hali, mwombeni Mungu katika sala juu ya mahitaji yenu, kwa shukrani. 7Nayo amani ya Mungu ipitayo akili zote za watu italinda salama mioyo na akili zenu katika kuungana na Kristo Yesu.
8Hatimaye, ndugu zangu, zingatieni mambo mema na yanayostahili kusifiwa; mambo ya kweli na bora; mambo ya haki, safi, ya kupendeza na ya heshima. 9Tekelezeni yale mliyojifunza na kupokea kutoka kwangu; mambo mliyosikia nimesema na kuona nimeyatenda. Naye Mungu anayetujalia amani atakuwa pamoja nanyi.

10Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo.11Sisemi hivyo sasa kwa sababu nahitaji kitu; maana nimejifunza kuridhika na vitu nilivyo navyo. 12Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa. 13Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu. 14Hata hivyo, nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana nami katika taabu zangu.
15Nyinyi Wafilipi mwafahamu wenyewe kwamba mwanzoni mwa kuhubiri Habari Njema, nilipokuwa naondoka Makedonia, nyinyi peke yenu ndio kanisa lililonisaidia; nyinyi peke yenu ndio mlioshirikiana nami katika kupokea na kuwapa wengine mahitaji. 16Nilipokuwa nahitaji msaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidi ya mara moja. 17Sio kwamba napenda tu kupokea zawadi; ninachotaka ni faida iongezwe katika hazina yenu. 18Basi, nimekwisha pokea vitu vyote mlivyonipa, tena ni zaidi kuliko nilivyohitaji. Nina kila kitu kwa vile sasa Epafrodito amekwisha niletea zawadi zenu. Zawadi hizi ni kama tambiko yenye harufu nzuri, sadaka inayokubaliwa na kumpendeza Mungu. 19Basi, Mungu wangu, kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo, atawapeni mahitaji yenu yote. 20Utukufu uwe kwa Mungu wetu na Baba yetu, milele na milele. Amina.



Salamu za mwisho
21Nawasalimu watu wote wa Mungu walio wake Kristo Yesu. Ndugu walio pamoja nami hapa wanawasalimuni.22Watu wote wa Mungu hapa, na hasa wale walio katika ikulu ya mfalme, wanawasalimuni.
23Nawatakieni nyote neema ya Bwana wetu Yesu Kristo.

Bible Society of Tanzania

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Wednesday, 10 June 2015

Niambie Live Show EP 4‏


Omby Nyongole, Henry Kente na Salma Moshi
Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE
Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia kuboresha maisha yako.
Ni Niambie Live....
KARIBU

Sunday, 7 June 2015

Natumai JumaPili Inaendelea/Ilikuwa Njema;Burudani-Yahweh - New Life Worship,Here I am to Worship,Days of Elijah ,My God is Awesome ...

Wapendwa Nimatumaini yangu Jumapili hii ilikuwa/Inaendelea Vyema
Nawataki kila lililojema,Amani,Furaha,Baraka na Fanaka.
Utukufu tumarudishie MUNGU.
.
5 Mwenyezi-Mungu ni mwema;
fadhili zake zadumu milele,
na uaminifu wake katika vizazi vyote.

Neno La Leo;Zaburi 100

Wimbo wa sifa
(Zaburi ya shukrani)
1Mshangilieni Mwenyezi-Mungu, enyi nchi zote!
2Mwabuduni Mwenyezi-Mungu kwa furaha,
nendeni kwake mkiimba kwa shangwe!
3Jueni kwamba Mwenyezi-Mungu ni Mungu.
Yeye ndiye aliyetuumba, nasi ni mali yake;
sisi ni watu wake, ni kondoo wa malisho yake.
4Pitieni milango ya hekalu lake kwa shukrani,
ingieni katika nyua zake kwa sifa.
Mshukuruni na kulisifu jina lake.
5 Mwenyezi-Mungu ni mwema;
fadhili zake zadumu milele,
na uaminifu wake katika vizazi vyote.
Bible Society of Tanzania














"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe Sana.

Thursday, 4 June 2015

Maisha;Hadithi Ya Kufundisha...


👌Hadithi ya kufundisha 👌
Siku moja jioni katika mji wa Washindao, kulikuwa na basi 🚍likisafiri kutoka mji huo kuelekea mji wa Wamtumainio.
Lilikuwa ni basi kubwa na limejaa abiria👫👪👬👭👫👪.
Wakati wakiendelea na safari, ghafla, mvua kubwa ☔iliyoambatana na radi⚡⚡⚡ ikaanza kunyesha.
Dereva hauogopa, wala abiria, wakaendelea na safari. Mara wakati wanaenda, radi ⚡ikaanza kufuatilia gari🚎. Kila wakienda, radi inapiga karibu na ⚡🚎⚡basi kana kwamba inalifuata basi. Likisimama, radi⚡ inapiga pembezoni mwa basi🚍⚡.
Dereva kuona hivyo, akasimamisha gari mita 5 kutoka kwenye mti 🚎............🌴. Akawaambia abiria👫👪👬👭👫👪, "Humu ndani ya basi, kuna mtu ambaye leo ni siku yake ya kufa🚷, tena kufa kwa radi⚡.
Ili tusife wote, nataka kila abiria🚶🚍💃 ashuke akaguse mti 🌴🚶💃🌴ili anayepigwa na radi, apigwe wengine wasife kwa ajili yake. "
Abiria wakitetemeka🙌🙇🙌, wakaanza kushuka🚶🚍💃 mmoja mmoja. Unaenda🌴🏃 unagusa mti , kisha unarudi 💃🚍kwenye basi. Abiria wote pamoja na dereva mmoja mmoja, wakaenda, wakagusa mti 🌴🏃na kurudi 💃🚍bila dhara lolote!
Akawa kabaki abiria mmoja tu🙇, ambaye alikuwa hajagusa mti.
Abiria wote kwa macho👀👀👀 ya hasira 😡😡😡wakamwambia akaguse mti. Akawa anaogopa 🙇🙌kufa. Akagoma. Wakamlazimisha kwa nguvu 💪sana na kumtoa nje
.🌴...... .......🚶👈🚍. Yule abiria akiwa amefumba macho😎, akaenda akagusa mti🌴🏃.
🙆Hamadi bin Vuu!
Radi kali sana⚡⚡⚡⚡⚡ ikalipiga basi🚍, abiria na wote waliokuwamo, wakafa palepale😪😔😪.
Kumbe uwepo wake ndio ulikuwa unazuia abiria wengine wasidhurike na radi.
📝MAFUNZO 📝
1. Unapofanikiwa, huwezi jua uwepo wa nani umefanikisha mafanikio hayo, usichukue sifa zote peke yako. Wapatie na wengine bila kumsahau MUNGU.
2. Unaweza kujiona huna thamani sehemu ulipo, iwe kwenye kundi la WhatsApp, darasani, kazini, kwenye basi, barabarani bila kujua kama uwepo wako ni wa muhimu sana kwa ustawi wa wengine.
3. Usimtenge wala kumnyanyasa mtu au jirani yako, huwezi jua uwepo wake unakusaidia kiasi gani.
4. Jali sana watu wako wa karibu, mchumba, mzazi, ndugu, mke, rafiki, jirani nk kwani uwepo wao ndio tunakuona unang'aa siku hadi siku.


Nimetumiwa Na Mpendwa


"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.

Wednesday, 3 June 2015

Niambie Live Show


Omby Nyongole, Dotto Maongo na Salma Moshi
Karibu kwenye kipindi hiki cha NIAMBIE LIVE

Kipindi kinachozungumzia mambo mbalimbali yaliyochukua nafasi za juu
kwenye mitandao ya kijamii. Pia kupata Tip ya siku / wiki kusaidia
kuboresha maisha yako.

Ni Niambie Live....

KARIBU

Monday, 1 June 2015

MISA YA KUMUAGA MZEE SAMUEL LUANGISA NEW YORK


Naibu balozi bi Maura Mwingira akitoa pole kwa watoto wa Mzee Luangisa, Bi Maura Mwingira kwa niaba ya balozi alipata nafasi ya kuongea machache mbele ya Watanzania waliojitokeza kwenye misa hiyo ya kumuombea marehemu mzee Luangisa pamoja na kuaga mwili wake tayari kwa safari ya kwenda nyumbani Bukoba Tanzania kwa mazishi.
Mtoto wa marehem Kwame akitoa wasifu wa mzee Luangisa wasifu huo uliwatoa machozi watu kutokana jinsi mzee Luagisa alivyokuwa mtu mwenye moyo wa kutoa kwakile alichonacho bila kuchagua wala kuhoji.
Mchungaji akiongoza misa mbele ya Watanzania wa New York na miji ya karibu na New York.
Watoto wa marehem wakiwa na sura za udhuni ya kuondokiwa na baba yao mpendwa ambae alikuwa nguzo ya familia hii pendwa.
Watu wakiaaga mwili wa mzee Luangisa pamoja na misa iliyofanyika jumamosi ya tarehe 30 mwezi wa 5. Kwa picha zaidi nenda soma Hapa.