Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 7 September 2015

Wimbo mpya wa UCHAGUZI toka kwa INNOCENT GALINOMA


Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, watu kupitia fani na kazi mbalimbali wamekuwa wakijaribu kuhamasisha wananchi kushiriki kufanya maamuzi yatakayolipeleka taifa letu mbele.

Innocent Galinoma, ni msanii mkongwe wa Reggae anayefanya kazi zake nchini Tanzania.

Naye ametunga wimbo maalum kwa ajili ya uchaguzi huu mkuu. Akisisitiza kuhusu kusikiliza na kuwahoji wagombea ili kujua fika wanalotaka kutufanyia katika kutatua kero zetu

Karibu usikilize kibao....UCHAGUZI

Sunday, 6 September 2015

Nimatumaini yangu Jumapili inaendelea vyema;Amani na itawale Tanzania,Burudani - Sisi sote,Gusa,Mungu yu mwema,Moyo wangu......




Wapendwa/Waungwana jumapili iendelee kuwa njema na yenye Baraka,Upendo na Amani ikatawale

 1Mwenyezi-Mungu alimwambia Mose, 2 “Iambie jumuiya yote ya watu wa Israeli hivi: Ni lazima muwe watakatifu kwani mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ni mtakatifu.3Kila mmoja wenu ni lazima amheshimu mama yake na baba yake, na kuzishika Sabato zangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. 4Msizigeukie sanamu za miungu, wala msijitengenezee sanamu za kusubu za miungu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
5“Mnaponitolea mimi Mwenyezi-Mungu sadaka za amani, mtanitolea kama itakiwavyo ili mpate kukubaliwa.6Sadaka hiyo ni lazima iliwe siku hiyohiyo inapotolewa au kesho yake. Chochote kinachobaki hadi siku ya tatu ni lazima kiteketezwe kwa moto. 7Kama sehemu ya nyama yake italiwa siku ya tatu, tendo hilo ni chukizo; na sadaka hiyo haitakubaliwa, 8naye atakayekula nyama hiyo ni lazima awajibike kwa uovu wake kwa sababu amekitia unajisi kitu kitakatifu cha Mwenyezi-Mungu. Mtu huyo atatengwa na watu wake.
Neno La Leo;Walawi19;1-37
Kutenda mema

9 “Utakapovuna mavuno ya nchi yako, usivune kabisa hadi mpakani mwa shamba wala usirudi nyuma kukusanya mabaki. 10Msirudie kukusanya kila kitu katika shamba la mizabibu, wala usiokote zabibu zilizoanguka chini; utawaachia maskini na wageni. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
11 “Msiibe, msidanganye wala kuambiana uongo.12Msiape uongo kwa jina langu hata kulikufuru jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
13 “Usimdhulumu jirani yako wala kumwibia. Mshahara wa mtu aliyeajiriwa usikae kwako usiku kucha hadi asubuhi.14 Usimlaani kiziwi wala kuweka kizuizi mbele ya kipofu, bali umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
15 “Unapotoa hukumu uamue kwa haki; usimpendelee maskini wala kumwogopa mwenye cheo. Bali ni lazima kumwamua jirani kwa haki. 16Kamwe usipitepite ukiwachongea watu wa jamaa yako. Usiyatie maisha ya jirani yako katika hatari ya kifo kwa maneno yako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
17 “Usimwekee kisasi ndugu yako moyoni mwako, bali upatane daima na jirani yako ili usije ukatenda dhambi. 18Usijilipize kisasi au kuwa na kinyongo dhidi ya wazawa wa watu wako bali umpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.


19 “Yakupasa kuyashika masharti yangu. Usiiache mifugo yako ipandwe na wanyama wa aina nyingine. Shambani mwako usipande mbegu za aina mbili. Usivae vazi lililofumwa kwa aina mbili za nguo.
20“Mwanamume akilala na mwanamke mtumwa ambaye ameposwa na mwanamume mwingine, lakini bado hajakombolewa wala kupewa uhuru, uchunguzi ufanywe. Lakini wasiuawe kwa sababu mwanamke huyo hakuwa bado huru. 21Mwanamume huyo ataleta mbele ya hema la mkutano sadaka yake ya kondoo dume ya kuondoa hatia na kunitolea mimi Mwenyezi-Mungu. 22Kuhani atamfanyia ibada ya upatanisho kwa kutumia kondoo huyo mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya dhambi aliyotenda; naye atasamehewa dhambi hiyo aliyotenda.
23“Mtakapofika katika nchi ya Kanaani na kupanda aina zote za miti ya matunda, matunda hayo hamtayala; hamtaruhusiwa kuyala kwa muda wa miaka mitatu.24Mnamo mwaka wa nne matunda yake yote yatakuwa matakatifu, yatatolewa kuwa sadaka ya sifa, kwa Mwenyezi-Mungu. 25Lakini matunda ya kuanzia mwaka wa tano hayo mnaweza kula, na mavuno yenu yataongezeka. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
26 “Msile nyama yoyote yenye damu. Msipige bao wala kufanya uchawi. 27 Nywele zenu msizikate pembeni wala kunyoa ndevu zenu. 28Msijitie alama zozote mwilini mwenu kwa ajili ya kuomboleza au kujikatakata mwilini au kujichanja chale. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.


29 “Usimchafue binti yako kwa kumfanya kahaba, nchi nzima isije ikaangukia katika ukahaba na hivyo kujaa uovu.30 Mtazishika Sabato zangu na kupaheshimu mahali pangu patakatifu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.
31 “Msiwaendee waaguzi wa mizimu wala wachawi ili kuwaomba wawaagulie na hivyo mkajitia najisi. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
32“Uwapo mbele ya mzee ni lazima usimame ili kumpa heshima yake; nawe umche Mungu wako. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.



33“Kama kuna mgeni katika nchi yako usimtendee vibaya. 34Huyo mgeni anayekaa nawe atakuwa kwako kama mwenyeji nawe utampenda kama unavyojipenda mwenyewe, kwa kuwa nawe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.




35 “Usikose kamwe kuamua kwa haki kuhusu vipimo vya urefu, uzito na ujazo. 36Ni lazima mtumie mizani halali, na vipimo vilivyo halali. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri. 37Ni lazima kuyashika na kuyatekeleza masharti yangu na maagizo yangu. Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu.”

Bible Society of Tanzania




"Swahili na Waswahili" Mbarikiwe wote.

Saturday, 5 September 2015

Reggae Time ya Pride FM......Justin Kalikawe




Ni zaidi ya miaka 12 sasa tangu kuondokewa na mwanamuziki mahiri wa Reggae kutoka nchini Tanzania, Justine Kalikawe.

Kwangu
ni kumbukumbu “mbichi” ya kuondoka kwake, kwa kuwa alifariki tukiwa
kwenye mkakati wa kufufua hamasa na umuhimu wa muziki wa reggae nchini.

Nakumbuka
ilikuwa ni mwaka 2003. Mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi saana kwangu.
Ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times
Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha Reggae jijini
Dar (ambako radio hiyo ilikuwa ikisikika).

Na nakumbuka tulipanga
kukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa Reggae nchini kuhusu
namna tunavyoweza kushirikiana kuunyanyua muziki huo uliolenga katika
KUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA AKILI YA JAMII ya wanyonywaji. Ni
katika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii
kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine
Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi.
Hivyo nikawa "namvizia" ili kujua muda ambao hashiriki kurekodi nimpate
naye aweze kuizungumzia tasnia ya Reggae nchini Tanzania.

Bahati
mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na
aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti. Huo ndio ukawa mwisho
wa ushiriki wake katika mkakati huo.

Lakini wakati anafariki,
nilikuwa likizo Bukoba, hivyo siku hiyohiyo nilipata taarifa
zilizonishtua sana, lakini nikazikubali na kuanza mikakati ya kushiriki
mazishi yake, jambo ambalo nililifanikisha.

Lakini….

Justin Kalikawe ni nani?

Thursday, 3 September 2015

DIASPORA YA MONTGOMERY COUNTY YAMUAGA BALOZI AMINA SALUM ALI




 Bwn. Daniel Korona akisherehesha hafla futi ya kumuaga Balozi wa Umoja wa Afrika aliyemaliza muda wake Mhe. Amina Salum Ali iliyoandaliwa na Jumuiya ya Diaspora kutoka Afrika wanaoishi Montgomery county iliyofanyika siku ya Jumatano Sept 2, 2015 Silver Spring, Maryland.
Kulia ni mwongozaji maswali Bi. Soffie Ceesay ambaye ni mwanachama mwanzilishi wa Montgomery County's African Affairs Advisory Group na African Immigrant Caucus akimuuliza Mhe. Amina Salum Ali maswali mbalimbali likiwemo nini anajivunia kwenye uongozi wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani. Balozi Amina Salum Ali alieleza ni ushirikiano wa nyanja mbalimbali mabazo nchi za Afrika zimenufaika na kupata mafanikio na uhusiano wa AU na Marekani kwa kuwezesha kupata Balozi wao nchini Marekani na kikubwa kabisa katika historia ya AU na yeye  kama Balozi kuwezesha Rais Barack Obama kwa mara ya kwanza katika historia kama Rais wa Marekani kuhutubia Umoja huo.


Isiah Leggett ambaye ni Montgomery County Executive akimtunukia cheti Mhe. Balozi Amina Salum Ali


Balozi Amina Salum Ali akitoa shukurani zake ambapo leo anaondoka kurudi Tanzania baada ya kumaliza muda wake kama Balozi wa kwanza wa Umoja wa Afrika nchini Marekani kazi aliyoifanya tangia 2006.
 Wahudhuriaji 
 Wageni waalikwa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

Tuesday, 1 September 2015

Mahojiano na Tausi Sued juu ya CSI FUNDRAISING




Dear All,



Come join the Embassy of Tanzania and Childbirth
Survival International (CSI) for CSI’s first annual fundraising on
September 12th at 4:30pm to 7pm, at the Embassy of Tanzania, Washington
DC.



In Tanzania, many of the lives lost during pregnancy,
childbirth, and immediately after birth, are often 100% preventable. We
are calling upon You to join us and help save lives. This fundraising is
to kickoff CSI’s saving lives at birth project in Biharamulo District
in northwest Tanzania. Biharamulo is one of Tanzania’s poorly performing
Districts that deserves immediate support and attention – We thank you
for answering the call. Visit www.childbirthsurvivalinternational.org for more information.



There’s
a registration fee of $100 and it includes a raffle ticket. All
donations are tax deductible and will be used to implement project
activities in Biharamulo. Registration link here.



Light Refreshments | Entertainment | Raffle Prizes | Networking



For information about the event, please contact

Sandra Kiyonga at sandra.kiyonga@childbirthsurvivalinternational.org or call 202-763-2100.



Tuko Pamoja!

Tuesday, 25 August 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU.


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015



Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015

Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Agosti 24, 2015


Monday, 24 August 2015

BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI MAREKANI MHE, WILSON MASILINGI AWASILI WASHINGTON DC.


    Balozi mpya atakayeiwakilisha Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi akiwa amefuatana  na Mkewe  Marystella Masilingi pamoja na mwanae Nelson Masilingi wawasili kituoni kwake Washington DC, awali ya hapo Mhe Wilson Masilingi alikua Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi.
Mhe Wilson Masilingi mara baada ya kutua Washington DC akisalimiana na atakayekua dereva wake Virgilio Paz maarufu kama Bong.
Safari ya Mheshimiwa Balozi pamoja na mama ikianza kuelekea Hotelini kwake ambapo atapumzika kwa muda kabla ya kuingia nyumbani kwake Bethesda ,Maryland.
Mhe Wilson Masilingi mara baada ya kufika Hotelini kwake akisaidiwa mlango na Afisa wa Ubalozi Swahiba Habib Mndeme.
Mhe Balozi Wilson Masilingi akisalimiana na baadhi ya Maafisa na Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani waliofika kumlaki pichani ni mmoja wa Maafisa Andrew Mugendi Zoka.
Mama Marystella Masilingi naye hakua nyuma kusalimiana na baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania.
Mhe Wilson Masilingi akiwa na bashasha tele kuona kwa jinsi gani Tanzania House walivyo na upendo na kuonyesha ushirikiano wao wa dhati kwenye tukio hilo muhimu.
Mhe Wilson Masilingi alifuatana na Mtoto wake Nelson Masilingi.
Maafisa wa Ubalozi Swahiba Mndeme pamoja na Alfred Swere wakiteta jambo kidogo.
Mhe Balozi Wilson Masilingi pamoja na Familia yake kwenye picha  ya pamoja na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta.
Mhe Wilson Masilingi alipata fursa kidogo kutembelea mitaa ya jijini akiwa ameongozana na Mwambata wa Jeshi Col. Adolph Mutta

Baadhi ya Wafanyakazi na Maafisa wa Tanzania House wakiwa Hotelini alipofikia Mhe Wilson Masilingi.

   PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI KWA PICHA ZAIDI UNGANA NASI PUNDE.