Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 20 September 2015

BALOZI WA TANZANIA NCHINI MAREKANI AKABIDHI HATI ZA UTAMBULISHO KWA RAIS WA MAREKANI BARACK OBAMA.‏


 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa na Rais wa Marekani Mhe. Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati za utambumbulisho (White House). Washington DC siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.
 Mhe. Wilson Masilingi   Pamoja na Familia yake wakiwa Katika nyuso za furaha mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho  Ikulu ya Marekani(White House) siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.  Kutoka kushoto ni Mtoto wa Balozi ndugu Nelson Masilingi, Rais wa Marekani Barack Obama, Balozi Wilson Masilingi, pamoja na Marystella Masilingi. Mke wa Balozi.
 Wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Wilson Masilingi na familia yake mara baada ya kurudi nyumbani kwake Bethesda, Maryland alipotoka kukabidhi hati za Utambulisho kwa Rais Barack Obama siku ya Alhamisi Septemba 17, 2015.

Wednesday, 16 September 2015

Jikoni Leo;Vilosa ( sweet rice dumplings)


Mahitaji, vipimo kwa vilosa 20

Unga wa ngano mweupe 1/2 Kikombe
Unga wa mchele 1/2 kikombe
Mayai 2
Tui la nza kikombe kasoro ( 3/4)
Hamira kijiko cha chai 1 na 1/2
Hiliki ya unga kijiko 1/4
Zafarani kidogo

Mafuta au samli ya kukaangia


shukrani;Aroma of Zanzibar


"Swahili na Waswahili"Pamoja Daima

[AUDIO]: Kipindi cha JUKWAA LANGU Sept 14 2015


Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 14, 2015
Kutoka Tanzania tuliungana na Jonathan Samiya na Nyakia, ambaye ni mmoja wa wakuu wa Itifaki wa kampeni za Dr Magufuli
Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Clare Ng'owo, Ali Badawy na Shamis Abdulla
Kwenye line tulikuwa na Jeff Msangi, Dr Patrick Nhigula na Arthur

Thursday, 10 September 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU.....Sep 7 2015 (Part One)


JUKWAA LANGU ni kipindi ambacho kitakuwa kikikujia kila Jumatatu, kujadili mambo mbalimbali yanayotokea nchini Tanzania, na zaidi kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

 Hii ni sehemu ya kwanza ya kipindi cha Septemba 7, 2017 ambapo studioni tulitembelewa na Shamis Abdul, kuwezesha mjadala.

Pia, kulikuwa na washiriki kwa njia ya simu, toka pande mbalimbali za dunia

Monday, 7 September 2015

Bin'adam "TENA"....Na maisha KINYUMENYUME. Apumzikaye kusherehekea SIKU YA KAZI


Na Mubelwa Bandio

 Ni SIKU YA KAZI hapa Marekani. Ama niseme kuthamini kazi. Ama siku ya wafanyakazi. Lakini vyovyote iwavyo, ni siku ambayo wengi wetu hapa Marekani tunakuwa na "siku ya mapumziko". NDIO, DAY OFF katika kusherehekea SIKU YA KAZI.

Mmmmmhhh!!! Umeona eeee?


Nilishaandika kuhusu kinyumenyume cha Bin-adamu katika kutenda, kunena na kuwaza. Kuwa kwanini tuwazishwe vitu kwa namna nyingine?


Kwanini nchi nyingi Afrika zisherehekee UHURU kwa staili ya gwaride kama la WAKOLONI WALIOTUTAWALA?


Kwanini siku ya wakulima isherehekewe mjini, na wapatao "day off" ni wale wasio wakulima ilhali wakulima hawapati sherehe yoyote siku hiyo?


Ni kwenye muendelezo huu wa KWANINI, najikuta naleta MASWALI YAFUATAYO, ambayo nilitumiwa na rafiki yangu, na si mawazo yangu.


TUMUWAZE BIN'ADAM NA UNAFIKI WA MAWAZO YA KIMATENDO.


Soma kisha uwaze, "bin'adamu anawaza nini kutenda atendayo?" Japo nilitumiwa NICHEKE, lakini yaliniwazisha pia


-Why do supermarkets make the sick walk all the way to the back of the store to get their prescriptions while healthy people can buy cigarettes at the front?


-Why do people order double cheeseburgers, large fries, and a diet coke.


-Why do banks leave vault doors open and then chain the pens to the counters.


-Why do we leave cars worth thousands of dollars in our driveways and put our useless junk in the garage.




EVER WONDER .......



-Why
the sun lightens our hair, but darkens our skin?


-Why can't women put on mascara with their mouth closed?


-Why don't you ever see the headline 'Psychic Wins Lottery'?


-Why is 'abbreviated' such a long word?


-Why is it that doctors call what they do 'practice'?


-Why is lemon juice made with artificial flavoring, and dish washing liquid made with real lemons?


-Why is the man who invests all your money called a broker?


-Why is the time of day with the slowest traffic called rush hour?


-Why isn't there mouse-flavored cat food?


-Why didn't Noah swat those two mosquitoes?


-Why do they sterilize the needle for lethal injections?


You know that indestructible black box that is used on airplanes? Why don't they make the whole plane out of that stuff?!


-Why don't sheep shrink when it rains?


-Why are they called apartments when they are all stuck together?


If flying is so safe, why do they call the airport the terminal?




HIVI TUNAWAZA NINI?




***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

Wimbo mpya wa UCHAGUZI toka kwa INNOCENT GALINOMA


Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, watu kupitia fani na kazi mbalimbali wamekuwa wakijaribu kuhamasisha wananchi kushiriki kufanya maamuzi yatakayolipeleka taifa letu mbele.

Innocent Galinoma, ni msanii mkongwe wa Reggae anayefanya kazi zake nchini Tanzania.

Naye ametunga wimbo maalum kwa ajili ya uchaguzi huu mkuu. Akisisitiza kuhusu kusikiliza na kuwahoji wagombea ili kujua fika wanalotaka kutufanyia katika kutatua kero zetu

Karibu usikilize kibao....UCHAGUZI