Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje Wapendwa/Waungwana? Tunamshukuru Mungu wetu Muumba wetu Muumba Mbingu na Nchi,Mungu wa Abrahamu Isaka na Yakobo,Baba yetu,Mwokozi wetu,Yeye asiyechoka,Yeye husamehe,Yeye asiye lala wala kunsinzia,Yeye si binadamu hata aseme uongo...
Siku hiyo mtasema: “Nakushukuru, ee Mwenyezi-Mungu, maana ingawa ulinikasirikia, hasira yako imetulia, nawe umenifariji. Mungu ndiye mwenye kuniokoa, nitamtegemea yeye, wala sitaogopa; Mwenyezi-Mungu hunijalia nguvu; yeye mwenyewe ndiye aniokoaye.” Mtachota maji kwa furaha kutoka visima vya wokovu. Siku hiyo mtasema: “Mshukuruni Mwenyezi-Mungu mwombeni kwa jina lake. Yajulisheni mataifa matendo yake, tangazeni kuwa jina lake limetukuka. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu sifa kwa kuwa ametenda mambo makuu; haya na yajulikane duniani kote. Pazeni sauti na kuimba kwa furaha, enyi wakazi wa Siyoni, maana aliye mkuu miongoni mwenu ndiye Mungu, Mtakatifu wa Israeli.”
Asante Baba wa Mbinguni kwa kibali ulichotupa na kutuchagua tena kuiona siku hii,Si kwamba sisi ni wema sana ,Si kwamba wajuaji na wenye nguvu,Sikwamba sisi ni bora sana kuliko wengine,Ni kwa Neema/Rehema zako tuu Baba wa mbingu... Tunaomba ukatulinde,ukatubariki katika kazi,Biashara,Masomo,Hatua zetu zikawe nawe Baba wa Mbinguni,Kuingiakwetu/Kutokakwetu,Vyombo vya Usafri,TutembeapoVilaji/Vinywaji.. Ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Mwokozi wetu Bwana wetu Yesu Kristo vyote tunavyoenda kugusa/Kutumia... na ukatutakase Miili yetu/Akilizetu .. Roho MtakatifuKu akatuongoze kwenye kunena/kutenda.. Ukatutumie na kutupa sawasawa na mapenzi yako... Mfalme wa Amani.. Ukawaponye/Kuwaokoa wote wanaopitia Magumu/Majaribu,Vifungo vya mwovu,Wagonjwa,Wafiwa wakawe mfariji wao,Wajane na Yatima Baba ukawabariki,Wenye shida/Tabu Baba ukawanyooshee mkono wako na kuwagusa
Mungu asema hivi: “Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa wokovu nikakusaidia.” Basi, sasa ndio wakati wa kufaa; sasa ndiyo siku ya wokovu![2Wakorintho 6:2]
Tunarudisha Sifa na Utukufu ni kwako Mungu wetu,Tunajiachilia mikononi mwako, Tukishukuru na Kuamini wewe ni Bwana na Mwokozi wetu... Amina...!!!!
Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze matakwa yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina.[Waebrania 13:21]
|